Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zazidi kusababisha maafa. Mtoto wa miaka 3 afariki kwa kusombwa na mafuriko Arumeru

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
746
3,057
Mvua zinazoendelea kunyesha mikoa mbalimbali ya Tanzania imezidi kusababisha maafa mbalimbali kama vifo, mawasiliano ya miundombinu kukatika nk.

Huko Arumeru mkoani Arusha watu wawili wamefariki dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku tatu mfululizo.

Akitoa taarifa za hali ya mwenendo wa mvua hizo baada ya kushiriki shughuli za uokoaji, Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe. Jerry Muro amesema, mvua hizo zimeleta madhara makubwa.

Waliofariki kwa mafuriko ni Terevaeli Mirisho Nasari (65), mkazi kijiji cha Mulala. Amefariki asubuhi baada ya maporomoko ya udongo toka mlimani kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala na kufariki dunia papo hapo, tayari mwili mwili wake umepatikana.

Kifo kingine ni cha mtoto aliyetambuliwa kwa majina ya Tumaini Simon (3) mwenyeji wa kijiji cha Valeska ambaye amesombwa na mafuriko wakati akiwa katika harakati za kuokolewa na mzazi wake. Mwili wa Tumaini umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.

Mafuriko.jpg
 
Yaani hizi mvua ni balaa, tangu jana asubuhi hazijakatika hadi leo. Karantini ya lazima hii.
 
Back
Top Bottom