Mvua zimerejea kwa kasi, ngoja tuone watakuja na kisingizio gani tena

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,199
2,000
'Mvua zinazoendelea kunyesha ni za Dar es salaam ambazo hazina uhusiano moja kwa moja na vyanzo vya Mabwawa yetu ya Mtera na Mto Ruvu,Ruaha na Pangani hivyo tunashauri Wananchi waendelee kuwa wavumilivu kipindi hiki Serikali yenu ya Visiwa vya Carribian ikiendelea na mchakato wa kupata mzabuni wa kukodisha majenereta ya kuzalisha Umeme ili kuhakikisha hakuna Mnyonge atakaekosa Umeme''
Michooro bado ipo mapangoni ya kutuletea mvua ya kutengeneza
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,199
2,000
Makombora ya kuzalisha mvua za kujaza mabwawa ya Umeme toka Vietinum sijui mchakato wa ununuzi wa Makombora hayo uliishia wapi?
Chini ya ccm hakuna kitu kinawezekana kwa manufaa ya watanzania
 

kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
4,777
2,000
Dikiteta hakuruhusu ukarabati alilazimisha machine ziwe oni mwanzo mwisho mpaka ikachakaa,sasa tutatengeneza
 

Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
3,410
2,000
Waliosema upinzani uko rohoni mwa wananchi walipatia vibaya sana.

Mkuu umechukua vizuri sana nafasi iliyoachwa wazi na CHADEMA kuihoji na kuikosoa serikali ya chama tawala. Congratulations. Kazi iendelee kwa kweli ๐Ÿ˜….
 

citizensindevelopment18

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
1,157
1,500
Leo ukanda wote wa Pwani mvua kubwa sana inanyesha, pia kanda ya ziwa kwa muda wa wiki nzima mvua imenyesha sana.
Sasa ngoja tuone Tanesco na Dawasa watakuja na visingizio gani tena.

Maana Tanesco walifikia kusema mvua imegoma kunyesha mwaka huu sababu ya hayati Magufuli alikata miti millioni 4 kwenye pori la Selous!!
Hoja zao mfilisi. Tuwe tunachunuza uwiano wa hoja zao na historia zao. Wengine malinda mh
 

mbwewe

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
3,244
2,000
Utoto mwingine raha sana. Eti mvua zinanyesha ukanda wa Pwani na kanda ya Ziwa. Sijui hayo maji ya mvua za kanda ya ziwa na pwani yataimgia katika mito yetu ya Ruaha na Pangani kuliko na mabwawaya kuzalisha umeme.
Hujui kwamba pangani ipo pwani?
 

TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
2,035
2,000
Hujui kwamba pangani ipo pwani?
Maji ya Mto Pangani yanatoka Arusha na Kilimanjaro. Yanaingia Bwawa la Nyumba ya Mungu. Then yanaingia Mto Pangani. Mto hauanzii mlangoni mwa Bahari. Huku Moshi na Arusha bado hatuna mvua. Ili Mto Pangani ujae maji mvua zinatakiwa kunyesha huku nyanda za juu Kaskazini Mashariki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom