Mvua zabomoa daraja Katavi, abiria wakwama kuendelea na safari

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,485
54,855
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Katavi zimeleta madhara makubwa baada ya abiria waliyokuwa wanasafiri kati ya mpanda na wilaya ya Nsimbo kukwama kuendelea na safari baada ya maji kujaa katika mto Magamba kubomoa daraja la muda na jipya linaloendelea kujengwa hali iliyowalazimu baadhi ya abiria kukatisha safari baada ya kukosa matumaini ya kuvuka katika mto huo na wengine wakilalamika kuteseka kwa njaa.

Halfani lihundi anataarifa kutoka Nsimbo katavi ITV ilifika katika eneo la mto Magamba na kushuhudia idadi kubwa la abiria waliyo kwama kuendelea na safari wakilalamikia kukaa muda mrefu katika eneo ilo bila msaada na kwamba sehemu hiyo imekuwa ikisumbua kwa miaka mingi na daraja jipya lililo bomoka kwa maji linajengwa kwa muda mre bila kumalizika lakini pia wanamashaka na kiwango cha ujenzi daraja ilo.

Kwa upande wao madereva wa magari ya abiria kutoka Itenka kwenda katika mji wa mpanda wamesema wamepata adha kubwa kwani baadhi yao wamebeba wagonjwa kupeleka hospitali na wameshaa kaa kwa zaidi ya saa sita bila matumaini hivyo wameiomba serikali kuangalia upya ujenzi wa daraja ilo kwakuwa ndiyo tumaini pekee la wananchi kwenda katika huduma za kijamii katika mji wa mpanda.

Chanzo: ITV
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom