Mvua yaua watatu, yakata mawasiliano ya Songwe, Rukwa na Katavi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
WhatsApp%20Image%202020-01-11%20at%2012.04.12.jpeg


Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Rukwa, zimeendelea kusababisha maafa baada ya kusomba madaraja manne katika barabara kuu ya Kasansa-Kilyamatundu inayounganisha mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi iliyopo bonde la ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga huku ikisababisha vifo vya watu watatu katika wilaya ya Kalambo na Nkasi mkoani humo.

Mvua hizo zimesomba madaraja katika vijiji vya Muze, Kifinga, Lwanji na Msia vilivyopo wilaya ya Sumbawanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya kata na kata, kijiji na kijiji pamoja na mikoa hali iliyoleta taharuki kwa wananchi wanaoishi katika bonde hilo lenye kata 13.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Rukwa Mhandisi Masuka Mkina amesemam tayari wamekwisha omba fedha za matengenezo ya Dharura.

Hali hiyo imepelekea mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo kutembelea maeneo yote yaliokumbwa na maafa hayo na kuwatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kulazimisha kupita sehemu zenye mafuriko.

Barabara hiyo ya Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa kilomita 178 ni kiungo muhimu kwa kuunganisha mkoa wa Rukwa na mikoa ya Songwe na Katavi hasa katika shughuli za kiuchumi.
 
Poleni Ndugu zangu wa Rukwa kwa maafa haya ila kuna haja ya upembuzi yakinifu Wakati wa ujenzi wa madaraja yetu tukiachana na athari za Mvua hata ubora wa madaraja yetu bado Ni changamoto hasa yaliyopo vijijini Kuna haja ya kuyafanyia tathimini kabla ya kuanza kuyatumia vinginevyo Kila Mvua zinapoanza kunyesha tutaendelea kupata maafa
 
Back
Top Bottom