singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
MVUA zinazoendelea kunyesha nchini zimeendelea kuleta madhara baada ya watu wanne kupoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa. Jijini Dar es Salaam mvua iliyonyesha kwa takribani saa tano mfululizo, ilisababisha athari kubwa hasa katika maeneo ya mabondeni pamoja na nyumba na barabara kujaa maji.
Hali ilikuwa mbaya jana majira ya asubuhi kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha tangu saa tisa usiku hadi saa tatu asubuhi. Mvua hiyo ilisababisha maeneo mengi, ikiwemo huduma muhimu kama barabara kujaa maji na kushindwa kupitika vizuri.
Katika eneo la Makumbusho Manispaa ya Kinondoni, njia ya kuingia kwenye kituo cha daladala ilijaa maji, kiasi cha magari kushindwa kupita, hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari katika Barabara ya Morocco - Mwenge.
Aidha, katika maeneo ya mabondeni yaliyopo Barabara ya Kilwa kando ya mto Kizinga Manispaa ya Temeke, kutokana na mvua hizo moja ya madaraja ya barabara hiyo yalikatika na kusababisha maji na michanga kuingia kwenye nyumba zilizo kando na mto huo.
“Kwa kweli hatujalala, daraja hili lilikatika tangu mvua ya mwisho kubwa inyeshe sasa mvua za jana likakatika zaidi na kusababisha maji yote ya mvua kuvamia ndani, hapa unapotuona tumeshindwa kutoa hata vyombo vyetu kutokana na kufukiwa na michanga iliyokuja na maji,” alisema Saida mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wakazi wa bonde hilo, wakihama kutoka katika nyumba zao huku vyombo vyao kama vile magodoro, makochi, nguo, redio na televisheni vikionekana kulowa na maji kutokana na mvua hizo.
Katika bonde la Mkwajuni, pamoja na mvua hizo kunyesha, gazeti hili lilishuhudia takribani familia 12 zikiendelea kuishi kwenye vifusi vilivyofunikwa na mabati chakavu katika bonde hilo, huku eneo hilo likizungukwa na maji na uchafu uliokusanyika kutokana na mvua.
Aliyekuwa Mjumbe wa Nyumba 10 wa bonde hilo aliyekataa kutaja jina lake, alisema familia hizo zitaendelea kukaa eneo hilo na kuvumilia kunyeshewa na mvua kwa kuwa hazina mahali pa kwenda baada ya kubomolewa nyumba zao kutokana na kujenga katika kingo za mto Msimbazi.
Mkoani Pwani, akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchukwi Wilaya ya Rufiji, Ami Lipundundu alisema katika kijiji hicho, mama na watoto wake wawili walikufa huku watu wengine watatu walijeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakati familia hiyo ikiota moto baada ya kuchota maji ya mvua.
Lipundundu alisema tukio hilo lilitokea Januari 18, mwaka huu saa 11 jioni katika kijiji hicho cha Mchukwi B wakati familia hiyo ilipokuwa ikiota moto huo huku mvua ikinyesha. Aliwataja marehemu hao kuwa ni Decilia Simba (42), watoto wake Debora Simba (4) na Amani Matimbwa mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu huku waliojeruhiwa wakiwa ni Maua Ngwande (13) anayesoma Darasa la Sita katika Shule ya Msingi Mchukwi, Suzana Daudi (12) na mdogo wa marehemu aitwaye Mama Tariq.
“Marehemu alitoka kwenye kikundi cha kuweka na kukopa cha Jitegemee ambapo yeye ni mwanachama alipofika nyumbani mvua ikaanza kunyesha akawa anakinga maji ya mvua yeye na watoto wa ndugu yake,” alisema Lipundundu.
Alisema baada ya hapo, waliwasha moto kwenye jiko lao, ambalo liko jirani na mti wa mfenesi na kuota kwani walikuwa wamelowa ndipo radi ilipopiga ikakwepa mti ikawapiga wao.
“Marehemu na wanawe walifia njiani wakati wakipelekwa Hospitali ya Mchukwi kwa ajili ya matibabu na majeruhi bado wamelazwa hospitalini hapo na hali zao zinaendelea vizuri,” alisema Lipundundu.
Mjini Mpanda, wakazi wawili wa Kijiji cha Ilebura wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi, wamekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema mkasa huo ulitokea Januari 19, mwaka huu saa nane na nusu mchana katika kijiji cha Ilebura, Kata ya Kabungu.
Aliwataja marehemu kuwa ni Kupiwa Julius (28) na Lemi Madirisha (30) na waliojeruhiwa ni Tatu Gerald (28), Stella John (38) na Philbert Paschal (29). “Kabla ya tukio, marehemu na majeruhi kwa pamoja walikuwa shambani katika kijiji cha Ilebura wakilima.
…..Wakati wakiendelea kulima ghafla mvua iliyoambatana na radi ilianza kunyesha, wote waliamua kwenda chini ya mti kujikinga na mvua na ndipo radi ilipowapiga,” alisema Kamanda Kidavashari.