Mvua yaleta Maafa Tanga: Watu watano wapoteza maisha, daraja la Lukozi lakatika..

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Watu watano wamekufa wakiwemo wawili wa familia moja baada ya kusombwa na maji ya mvua katika matukio mawili tofauti yaliyotokea katika wilaya za Handeni na Lushoto Mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Edward Bukombe amesema matukio hayo yametokea katika kipindi cha siku tatu zilizopita kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

BALAA LA MVUA MLALO - LUSHOTO:

Mvua kubwa inayonyesha tangu juzi wilayani Lushoto mkoani Tanga imesababisha athari kubwa ikiwemo Daraja la Lukozi kubomoka na hivyo kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya Jimbo la Mlalo na Lushoto.

Kufuatia hali hiyo wananchi wa Mlalo wanaotegemea Lushoto kwa ajili ya kujipatia huduma muhimu za kijamii zikiwemo hospitali pamoja na manunuzi ya bidhaa mbalimbali za vyakula na mazao.

Aidha kukatika kwa mawasiliano kati ya maeneo mawili hayo pia kumesababisha usumbufu na kuwatia hofu wafanyabiashara wa Mlalo wanaotegemea kuvuka kwa ajili ya kusafirishia mazao yao kwenda katika mikoa mingine nchini kupitia Lushoto.
FB_IMG_1520921895947.jpg
FB_IMG_1520921891251.jpg
 
Mwenyezi mungu awafanyie wepesi waathirika na wapumzike kwa amani marehemu.
 
Vipi hiyo picha mliyoweka mmeruhusiwa na mamlaka husika!?
Ni angalizo tu msije ishia kwenye makosa ya mtandao maana nchi ilishakuwa ya kufuata sheria bila shuruti.
 
Back
Top Bottom