Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 7,620
- 16,365
Hapa naandika baada ya muda mchache baada ya kukatika kwa mvua kubwa na yenye upepo mkali.
Sijatoka kutembea kuona mtaani hali ikoje lakini nikiwa nyumbani naweza kuona madhara makubwa yaliyojitokeza kutokana na mvua hii, makazi yameharibiwa sana, miundombinu ya umeme iko hoi kabisa.
Kwa taarifa nilizopata Ni kuwa huko mtaani nyumba zimepunyupiwa hadi sio poa. Na kulingana na asili ya Dodoma hatujazoea mvua kubwa kiasi hiki basi hata makazi yetu siyo imara kivile kwa hiyo kwa sasa wingu likitanda tu basi watu wanajawa na taharuki.
Kwenye mashamba nako hali sio shwari, watu hawalima Sana kutokana na mvua, huko kwenye mashamba ya mpunga mazao yanazolewa na maji.
Faida pekee tunayopata ni kuokota visamaki kwenye maji yanayopita majumbani mwetu.