'Mvua ya Lowassa' yazidi kuleta maafa Thailand

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,663
20,418
Kumekuwapo mfululizo wa maafa yatokanayo na mafuriko yanayosababishwa na mvua huko Thailand. Itakumbukwa kwamba waziri mkuu aliyejiuzulu, EL aliwahi kuwaleta wataalamu kutoka Thailand ili waweze kutengeneza mvua, mradi uliokuja kuyeyuka baadaye. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) wakati huo, Philip Marmo alisema bungeni kuwa serikali ilishindwa kupeleka wanafunzi kwenda Thailand kwani gharama kwa ajili ya kufanya zoezi la majaribio ilifikia sh bilioni 1.5 na kwamba endapo mradi mzima wa kutengeneza mvua hizo ungetekelezwa ungegharimu sh bilioni 14.5

Sasa hao wenzetu wametengeneza mvua hadi mafuriko, nadhani kwa ukame wetu hizo 14.5b si kitu.
 
Back
Top Bottom