Mvua ndizo zitakazomaliza mgawo wa maji Dar, asema Prof. Mwandosya

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Mwandosya%2811%29.jpg

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya



Serikali imesema haina uwezo wa kumaliza tatizo la mgawo wa maji uliolikumba jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani na badala yake inasubiri mvua zinyeshe
Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani imekumbwa na mgawo wa maji tangu juzi kutokana na kuharibika kwa mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu chini na kupungua kwa kina cha maji.
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, alipozungumza na NIPASHE baada ya kutembelea ofisi za Dawasco, jijini Dar es Salaam.
Profesa Mwandosya alisema wanatarajia mvua zikinyesha ndizo zitakazotatua tatizo la kuwepo mgawo wa maji kwa kuwa kina cha maji Ruvu chini kimepungua kutokana na ukame.
Aliongeza kuwa mgawo uliotangazwa na Dawasco juzi unaweza kuendelea kuwepo kwa kuwa hakuna vyanzo vingine vya maji vya akiba ambavyo wanaweza kuvitumia kama njia mbadala ya kutatua tatizo la maji.
Kuhusu utendaji wa watumishi wa Dawasco, Profesa Mwandosya aliwaasa kufanya kazi na kujiepusha na vitendo vya kuomba rushwa kutoka kwa wateja ili wawape huduma.
Alikiri kuwa kuna baadhi ya watendaji wachache wanaotumia vibaya jukumu walilopewa la kuwapatia maji Watanzania na kuamua kujikita katika vitendo vya rushwa.
Aidha, aliwataka watumishi kuwa wepesi wa kukagua maeneo yote ilipopita miundombinu ya maji kubaini mabomba yaliyopasuka ili waweze kuyaziba haraka.
Aliwaambia kuwa maji mengi ya Dawasco yanapotea njiani kabla ya kumfikia mteja hatua ambayo alisema inazua mgogoro mkubwa kati ya wateja na shirika hilo.
Aliwaka watumishi hao kuacha tabia ya kuwapa Ankara za malipo wateja kila mwezi huku hawawapatii maji kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwaibia.



CHANZO: NIPASHE

Watanzania Ngojeni Mvua anayoteremsha Mwenyeezi Mungu inyeshe ndio huo mgao wa Maji utakwisha kazi kweli Waziri huyo anasema hivyo ? Kazi kweli Nchi yetu hiyooo imekufaaaaaaaaaaa
 
Bora amesema ukweli: ile ahadi ya mkulu ya kuchimba maji kimbiji iliishia wapi? Au ilikuwa ni kutaka kula(kura)!
 
Bora amesema ukweli: ile ahadi ya mkulu ya kuchimba maji kimbiji iliishia wapi? Au ilikuwa ni kutaka kula(kura)!

ilikuwa ya kutaka Mumpe kura zenu tu hakuna cha kuchimba Visima wala nini. Waziri anasema Eti Serikali yake haina uwezo wa kutatuwa Matatizo ya Upungufu wa Maji najiuliza kwanini Rais J.Kikwete Kampa huyu Prof. Mwandosya Uwaziri? Hatufai kabisa kutoongoza Waziri mzima anasema Eti Serikali haina uwezo wa kutatuwa

tatizo hili la maji Tungojee Mvuwa zikinyesha. Nauliza Je kama Mvuwa hazikunyesha ndio tutakosa Maji? Huu ndio Uungwana jamani? Hatuna Serikali hatuna Viongozi wote ni Mafisadi asanteni.
 
:redfaces::redfaces:
Hii ni hatari,tumekuwa na viongozi wasiofikiri kabisa hata kidgo. hivi huko nchi za jangwani wanaishije? mbona tunaingiza mazezeta kutuongoza jamani? kwa hiy kama mvua isiponyesha..we will all perish maana waziri hana alternative zaidi ya mvua...This is terrible...
 
Hapa ndio uone viongozi wenye kufikiri miguuni tu na hawana tabia ya kujishughulisha? Kweli Upatikanaji wa maji utategemeana na Mvua je zisipo nyesha? Watanzania bado tunasafari ndefu sana.

Tanzania inayozungukwa na maji kila kona inasubiri Mvua inyeshe? Bora nisiendelee maana na weza tukana bure.......
 
Duh! Tena aliesema ivyo ni profesa (no wonder wakiendaga nchi za watu,uwa hawajitambulishi ka professors,wanasema Iam Dr.....). Hii ni hatari kwakweli. Na haya matabia nchi yanavyobadilika watu wa Dar imekula kwao.
 
Hivi kweli baada ya miaka yoote hiyo ya uhuru haya ndo majibu kuwa tusubiri mvua? Na isiponyesha je? Hivi haya majibu rahisi tunayapendea nini? Yaani hata prof asome ulaya na us bado akirudi bongo anakuja kuwa kama mtu ambaye bahati mbaya hakuweza enda shule.

Hiyo mihela wanayobofoa kwenye ufisadi si wangeelekeza katika maeneo ya maji? Inawezekana kabis ila mi nadhani hata hawa donors sijui, waache kabisa kutusaidia maana hamna tunachopata jamaa ndo wanabofoa kama hawana akili nzuri vile mh.
 
Hivi kule DUBAI, U.A.E NA DOHA QATAR, ETHIOPIA huwa na wao wanasubiri mvua zinyeshe????
 
Heheheheheheh loh sad

Na sie wa kiburugwa tusiojua maji ya dawasco yanafananaje nini kitamaliza hilo tatizo? Radi au kimbunga??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom