Mvua ndani ya kanda ya Kaskazini,Hasa niliyoishudia ndani Jiji la Arusha!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,216
Mvua kubwa iliyoendelea kunyesha Kanda ya Kaskazini tangu juzi tar 20/04/2012 iliyokua ikianza kwa kusuasua na hata kukatisha tamaa kwa wafugaji na wakulima,Sasa imeanza tangu jana kwa kasi ya ajabu hasa jana jioni ikinyesha Wilayani Monduli na hata W/Arumeru Magharibi bila shaka Wanainchi walioko mabondeni hawatakuwa na makazi!

Na hata hivyo mpk hapa nikiendelea kuchat hapa jamvini,hakika mvua ya uhakika inanyesha hapa A town haswa!
Mvua ilianza kwa kusuasua vile tangu majira ya saa kumi na mbili jana jioni na ilipotimia majira ya saa sita usiku na kuendelea mvua isiyo na mawimbi wala ngurumo inanyesha takrban masaa mawili sasa!

Na nilipojaribu kurudisha kumbukumbu nyuma,ndipo nikakumbuka hata ule mwaka wa ELNINO mwaka 1998 ilianza kwa mfano huu huu, Nawashauri ndg zangu walioko mabondeni tuwe macho kwani hali ya hewa mwaka huu bila shaka ina ishara ya mwaka tajwa hapo juu!

Bado cjapata taarifa rasmi toka ktk Wilaya hizo mbili nilizozishudia mvua ile ya jana jioni ilyofanya majira ya alasiri kuwa kama saa moja jioni kama itakuwa imeleta madhara yoyote!

Ila ntafuatilia na ntarudi baada ya!

MUNGU BARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!

MUNGU IBARIKI AFRIKA NA WATU WAKE!

Source ni Mi mwenyewe!
 
Mkuu nimetoka moshi mjini mvua si nyingi,lakini kuanzia maili sita,machame,boma inaonyesha imenyesha usiku
 
Kwenye kituo chetu cha Arusha kimeweza kurekodi kiasi cha mvua iliyonyesha jana ni (mm 68).
So ikiendelea hivi itweza sababisha madhara.
 
Kwenye kituo chetu cha Arusha kimeweza kurekodi kiasi cha mvua iliyonyesha jana ni (mm 68).
So ikiendelea hivi itweza sababisha madhara.

Mpaka hv sasa najaribu kumseach mwenyeji mmoja wa Wilaya ya Monduli hasa wa pale makazi ya mti mmoja maana nina hofu na mvua iliyopiga anga ile jana na hata hapa wilaya ya Arumeru magharibi mtaa wa Kisongo bila shaka wana la kusema kuhusu mvua ya jana!

Ntarudi mara niwapatapo maana kama kweli wameifanyia vipimo hakika inaweza ikawa zaidi ya milmita uliyotaja hapo.
 
Habari nilizopata kwa raia aliyekutwa jana na mvua ile amesema imemlazimu jana kula ng'ambo ya boma yake kwa ajili ya mvua ile iliyonyeesha bila ya kukatika kwa takrban masaa manne wilayani Monduli.

Akielezea mvua ilivyoanza kunyesha amesema ilianza mithili ya wingu jeusi kushuka na ikanyesha kimya kimya kwa muda tajwa hapo juu!
Na mabonde makubwa na madogo kujaa pomoni.
Na hata hivyo hajadodosa madhara yoyote ya mvua hiyo ila alitoa tahadhari ya kwamba hakika mvua imekuja wakati inahitaji lakini ametoa mtazamo ya kwmb inaweza ikawa ile ya mwaka tajwa hapo juu (1998).

Na dalili ya kunyesha tena kwa siku ya leo iko wazi kwa mtazamo wetu wa kibinadamu!
Ni hayo tu ndiyo nimebahatika kuzinyaka toka kwa huyu ndg.
 
Hapa mwanza, baada ya mvua ya kawaida iliyonyesha jana mchana, usiku huu saa moja unusu Tanesco wamekata umeme, kuna giza sana maana wingu jeusi limefunga anga kuna dalili ya mvua kubwa kunyesha, na muda si mrefu imepiga radi moja kali sana hadi kufanya baadhi ya watu kuweweseka, ngoja nizime kasim kangu maana tunaambiwa simu kwa radi ni hatari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom