Mvua kubwa ya mawe imeharibu zaidi ya ekari 100 za mashamba yenye mazao wilayani Tarime

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Mvua kubwa ambayo imeambatana na mawe makubwa imesababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu mashamba yenye ukubwa wa ekari zaidi ya mia moja ya mazao mbalimbali katika vijiji viwili wilayani Tarime mkoani Mara.

Baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo vya Nyakalima na Ntagacha katika wilaya ya Tarime, wamesema mvua hiyo kubwa ya mawe ambayo imenyesha kwa zaidi ya saa sita katika kata ya Ganyange, imeharibu sehemu kubwa ya mazao katika mashamba hayo.

Naye mweyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime Bw Glorious Luoga, akizungumza baada ya kufika katika vijiji hivyo kwa ajili ya kukagua athari ambazo zimesababishwa na mvua hiyo, amesema licha ya serikali kutangaza kuwa haiwezi kutoa chakula cha njaa cha msaada, lakini wananchi hao watahitaji msaada kutokana na hasara ambayo imesabishwa na mvua hiyo.

Chanzo: ITV
 
Mvua kubwa ambayo imeambatana na mawe makubwa imesababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu mashamba yenye ukubwa wa ekari zaidi ya mia moja ya mazao mbalimbali katika vijiji viwili wilayani Tarime mkoani Mara.

Baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo vya Nyakalima na Ntagacha katika wilaya ya Tarime, wamesema mvua hiyo kubwa ya mawe ambayo imenyesha kwa zaidi ya saa sita katika kata ya Ganyange, imeharibu sehemu kubwa ya mazao katika mashamba hayo.

Naye mweyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime Bw Glorious Luoga, akizungumza baada ya kufika katika vijiji hivyo kwa ajili ya kukagua athari ambazo zimesababishwa na mvua hiyo, amesema licha ya serikali kutangaza kuwa haiwezi kutoa chakula cha njaa cha msaada, lakini wananchi hao watahitaji msaad a kutokana na hasara ambayo imesabishwa na mvua hiyo.

Chanzo: ITV
picha ni muhimu kwa taarifa kama hii..
 
Mashamba ya bangi yatakuwa miongon mwa mimea iliyoharibiwa na mvua ya mawe
 
Poleni sana wahanga, nilipata kusikia kuwa siku alipozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere pia ilinyesha mvua ya ajabu, very likely hii ya jana ina jambo nyuma yake
 
Back
Top Bottom