Mvua kubwa kunyesha tena Tanga, Dar na Pwani, wananchi washauriwa kuchukua tahadhari

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) nchini imewashauri wananchi wa mikoa ya kanda ya Pwani kuchukua tahadhari stahiki ya kutokana na vipindi vya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika maeneo yao kwa muda wa siku tatu.

Ukanda huo wa Pwani ambao utapata mvua kubwa ni mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja. Mvua hiyo inatarajiwa kusambaa katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Lindi kuelekea siku ya Ijumaa ya tarehe 3 Novemba 2017.

Wananchi wa mikoa iliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA kwa sababu mvua inatarijiwa kuwa kubwa inayozidi milimita 50 kwa kiwango cha asilimia 80 kuanzia usiku wa jana Oktoba 31.

Hali hii inatokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter Tropical Convergency Zone –ITCZ) katika maeneo hayo. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

Mvua kama hiyo ilinyesha wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kuleta maafa ikiwemo uharibifu wa makazi ya watu, miundombinu ya barabara na madaraja. Hali hiyo ilisababisha hadha ya usafiri kwa wananchi wanaoingia na kutoka katika mikoa hiyo.
 
Tunawapongeza TMA kwa tahadhari wanayoitoa, hakika tujipange maana mvua iliyonyesha siku mbili wiki iliyopita zilikuwa na maafa makubwa. Tusipuuze tahadhari hii ili tujiweke upande ulio salama.
 
Back
Top Bottom