Mvua kubwa inanyesha Dar es Salaam

Andfaru

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
221
148
Habari zenu wakuu,

Tangu asubuhi mvua kubwa inaendelea kunyesha sehemu mbalimbali za Dar es Salaam.

Mvua kubwa hii imesababisha usumbufu, baadhi ya barabara hazipitiki kwa watembea kwa miguu na wenye magari.

Eneo la Mnazi mmoja kwenye barabara ya Bibi Titi, magari yamepaki sababu barabara hazipitiki baada ya maji kutuama barabarani.

Pia kufuatia hali hiyo maeneo ya Kariakoo baadhi ya biashara za watandika bidhaa pembezoni mwa barabara wamefunga biashara zao kufuatia mvua hii inayoendelea kunyesha.
Hata hivyo tulishaambiwa=>TAHADHARI: Mamlaka ya Hali ya Hewa yataadharisha uwepo wa mvua hatarishi

Naomba tuendelee kupeana updates ya madhara ya mvua hii, kama tujuavyo ni kawaida ya mvua ikianza kunyesha Dar es Salaam huambatana na kadhia mbalimbali.

Karibuni.
157a2e45-6ddc-4dbb-ac1e-acace9231ecd.jpg
cebc21ef-da83-4aea-8ae9-81046fcec6f7.jpg
1277e29a-47e3-468d-8d56-e4637c994c6a.jpg
8f02b5d4-029c-4c43-93cd-057015c8fb4c.jpg

15181685_1154678824622900_5342085442876059008_n.jpg

15181286_1154678257956290_4823622795642223720_n.jpg

 
Habari zenu wakuu

Tangu asubuh mvua kubwa inaendelea kunyesha sehem mbalimbali za Dar es Salaam

Naomba tuendelee kupeana updates ya madhara ya mvua hii,kama tujuavyo ni kawaida ya mvua ikianza kunyesha Dsm huambatana na kadhia mbalimbali

Karibuni
Kumbe hii mvua imenyesha Dar yote eeh .....??
 
Kumbe hii mvua imenyesha Dar yote eeh .....??
sehem nyng sana hii mvua inayesha mkuu....kwa taarifa za watu mbalimbali nlioongea nao! lkn pia kupitia huu uzi tunaweza fahamu mengi hasa kuhusu hii mvua na madhara yake
 
bugurun pakavu kabisa hamna tope japo mvua ipo ni vimajimaji vichache barabaran tu
 
bugurun pakavu kabisa hamna tope japo mvua ipo ni vimajimaji vichache barabaran tu
mkuu.....ndo maajabu ya Dsm wakati mwingine! kama akili yako haina ushirikiano mzuri waweza dhani kuna harufu ya uchawi hv
 
Back
Top Bottom