Mvua iliyoanza kunyesha jijini DAR yaleta ahueni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvua iliyoanza kunyesha jijini DAR yaleta ahueni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mhache, Jan 26, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mvua iliyoanza kunyesha jana katika jiji la Dar es Salaam imekuwa ni ahueni kwa tulio wengi. Wengi tulikuwa tukilala nje ya nyumba zetu kutokana na joto kuwa kali na watu kuwashwa kutokana na joto kali. Watoto walikuwa wakishindwa kupata usingizi kutokana na joto kali. Pia mvua hiyo imetupa ahueni kwani tumepata maji ya kutumia hata siku mbili kama sio tatu kwa wale wenye vyombo vya kutosha. Mvua hii iwe ni ahueni kwelikweli sio watu waanze kuzibua vyoo vyao na kumwaga uchafu/takataka ovyo . Kinyume chake tutapata magonjwa ya milipuka kama kuhara na kutapika.

  Vombo vya hali ya hewa sijasikia vikisema lolote kuhusiana na mvua hii. Au nyie wanajamii mmesikia chochote kuhusiana na mvua hii. Je mvua hii itaendelea kwa muda mrefu au ni ile ya kusafisha mwezi na kuingia mitini. Ninasema hivyo ili sisi watu wa mabondeni tuangalie ustaarabu au tuanze kuagiza mitumbwi?
   
 2. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Du bongo bwana, ahueni itakuwa kwa wasanii dawasa na dawasco maana nasikia Ruvu ipo karibu kuwa historia, tuombe mungu mvua ifike na huko pia kama bado haijatia timu!!Maji ni uhai.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hao hali ya hewa si mpaka waone mafuriko ndio watangaze eeh!!!! kesho mvua za hapa na pale!
   
 4. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Wao ni watabiri, hawajapiga ramli bado
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mvua kuendelea kwa siku tatu
  Gloria Tesha
  Daily News; Monday,January 26, 2009 @21:15

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema mvua zilizoanza jana katika mikoa ya Pwani ya Kaskazini zitaendelea mfululizo kwa siku tatu katika maeneo hayo, lakini hazitakuwa na madhara makubwa kwa binadamu japo tahadhari inapaswa kuchukuliwa.

  Aidha, TMA imesema mvua hizo zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam, Pwani, Zanzibar (Unguja na Pemba), Tanga na Morogoro Kaskazini, si za vuli wala za kila mwaka, bali zimetokana na mabadiliko ya mfumo wa hali ya hewa katika maeneo ya Arebia na Kaskazini Magharibi mwa Bahari ya Hindi.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Philbert Tibaijuka, alisema jana kuwa mabadiliko hayo yamekuwapo baada ya kupunguka kwa mgandamizo wa hewa katika maeneo hayo na kusababisha ukanda wa mvua za msimu katika Bahari ya Hindi uliokuwa Kusini, kusogea Kaskazini na kuwa karibu na pwani ya Tanzania.

  Tibaijuka alisema mvua hizo zitaendelea mfululizo kwa siku tatu, lakini kulingana na kiwango chake, haitakuwa na madhara makubwa kwa binadamu na baada ya siku tatu hali ya ukame na jua itarudi kama ilivyokuwa kabla ya jana.

  “Hizi mvua za vuli wala masika, hizi zimetokana na mabadiliko hayo ambayo yamesababisha upepo unaokuja mashariki kuwa na unyevunyevu na hivyo kutakuwa na ongezeko la mvua kwa siku tatu mfululizo na baada ya hapo hali ya ukame iliyokuwa awali itarudi katika pwani yote ya Kaskazini,” alisema Tibaijuka.

  Alisema hadi jana saa 3.00 asubuhi, vituo vya Hali ya Hewa vya pwani viliripoti viwango vya mvua ambapo Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kilikuwa na milimita 6.6, Mamlaka ya Bandari Tanzania milimita 21.6, Kibaha milimita 19.5, Morogoro milimita 6.6, Pemba 1.2 na Zanzibar milimita 53.3 ambacho ni cha juu kuliko vituo vingine.

  Alisema hali hiyo siyo ya madhara na kutolea mfano Zanzibar ambako kwa mwezi hupata milimita 96 na kwamba kiwango hicho cha milimita 53.3 ni kikubwa kwa siku moja ingawa hakina madhara labda kikifikia milimita zaidi ya 150 kwa siku. Katika maeneo ya Dar es Salaam, mvua zilianza kunyesha juzi kuanzia saa 7:15 usiku na hivyo kusababisha msongamano wa magari baadhi ya maeneo kama, Mbagala Kizuiani na Mto Kizinga, Mtoni-Mtongani kulikuwa na matope yaliyosababisha magari kupita kwa shida.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...