Mvua iliyoambatana na upepo mkali yasababisha maafa kata ya Bujela wilayani Rungwe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,239
Zaidi ya wanafunzi 70 wa shule za sekondari za Bujera na Mwaji wamenusurika kifo baada ya vyumba vitatu vya madarasa pamoja na jengo la maabara kuezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali wakati wakiendelea na masomo darasani, huku kaya sita za wakazi wa kijiji cha Nsongola, kata ya Bujela wilayani Rungwe wa kikosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa.

Mvua kubwa ambayo imeambatana na upepo mkali imenyesha katika kijiji cha Nsongola kilichopo kata ya Bujela wilayani Rungwe na kusababisha maafa makubwa baada ya kuezua vyumba vitatu vya madarasa na baadhi ya nyumba za wananchi ambao sasa hawana mahali pa kuishi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nsongola, Ambokile Asukile Mwaikuju amesema mvua hiyo imesababisha janga kubwa kijijini kwake kutokana na kuwafanya wananchi ambao nyumba zao zimeboka kuishi maisha magumu.

Diwani wa kata ya Bujela, mheshimiwa Amnoni Mchapi mwamalala amesema mvua hiyo imesababisha hasara kubwa ambayo itajadiliwa na kamati ya maendeleo ya kata ili kuona namna ya kukabiliana na madhara hayo huku akiomba wahisani kujitokeza kusaidia waathirika wa janga hilo.

ITV
 
Pole kwao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom