Mvua ikinyesha umeme unakatika, hii nayo ni kero

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Toka saa 3 hatuna umeme huku Kijichi na mvua inaendelea, kazi zimesimama swali kwa ndugu zetu TANESCO, kwanini hakutafuti suluhisho la kudumu kwa tatizo hili la kutoweka kwa umeme mvua inyeshapo?

Maana ni miaka mingi sasa tunashuhudia hali hii ina maana Shirika hawalijui hili? Na wanaweza kutupa sababu yake? Hii hasara nani wa kutufidia na Luku tunalipia? Ni vema tujuzwe sababu na suluhisho la kudumu.

Asante.
 
Hali kadhalika na tabata hali ni hiyo hiyo, ingawa wakati naandika huu Uzi umerudi baada ya mvua kupungua
 
Toka saa 3 hatuna umeme huku Kijichi na mvua inaendelea,kazi zimesimama swali kwa ndg zetu Tanesco kwanini hakutafutwi suluhisho la kudumu kwa tatizo hili la kutoweka kwa umeme mvua inyeshapo?maana ni miaka mingi sasa tunashuhudia hali hii ina maana Shirika hawalijui hili?na wanaweza kutupa sababu yake?hii hasara Nani Wa kutufidia na Luku tunalipia?ni vema tujuzwe sababu na suluhisho la kudumu,Asante.

Kumbe inanyesha Dar nzima
 
Tujiongeze wakuu si kila kitu Kulaumu tanesco umeme huwa unakatwa kunusuru majanga mbalimbali kutokana na baadhi ya maeneo hususani dsm kuwa na ubovu wa miundombinu na mtu mmoja mmoja kama wiring systems na miundombinu kwa u jumps.
 
Tujiongeze wakuu si kila kitu Kulaumu tanesco umeme huwa unakatwa kunusuru majanga mbalimbali kutokana na baadhi ya maeneo hususani dsm kuwa na ubovu wa miundombinu na mtu mmoja mmoja kama wiring systems na miundombinu kwa u jumps.
Ujue kuna nchi hawalijui tatizo la kukatika kwa umeme,sasa yatupasa tuelekee huko,kama ni miundombinu mibovu basi waweke ya kisasa pesa wanazo,unataka kunambia mvua ikinyesha Siku tatu mfululizo basi na Sisi tukose umeme na tuwe gizani Siku tatu nzima?lazima tulaumu mkuu kwa hili
 
Inaelezwa kua Tokyo ilipopatwa na ile Tsunami,mvua Kali upepo na mafuriko umeme ulikatwa maeneo yalioathirika tu kwa maana palipoanguka majengo na nyaya za moto,maeneo mengine umeme haukuzima!
 
Back
Top Bottom