Mvomero: Ofisi ya kijiji cha Mlali yachomwa moto, vitu vyote ndani vyateketea

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,422
2,000
Ina maana hao "Watu Wasiojulikana" sasa wamebadili gia angani hawateki watu tena au kuwajeruhi kwa risasi ila sasa wanachoma nyumba kwa moto.
This is terrible.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
19,875
2,000
Wilayani Mvomero mkoani Morogoro ofisi ya kijiji cha Mlali imechomwa moto usiku wa kuamkia leo, nyaraka zote muhimu zateketea.

Watu wasiojulikana, wameichoma moto Ofisi ya Kijiji Cha Mlali kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo Jumatatu Novemba 11, 2019.

Aidha ofisi hiyo imechomwa moto pamoja na nyaraka zote zilizokuwa ndani ya ofisi hiyo zimeteketea kwa moto.

Uongozi wa mkoa wa Morogoro akiwemo Mkuu wa mkoa Loata Ole Sanare pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa wako eneo la tukio wakifuatilia sababu za kuchomwa moto ofisi hiyo.

Mwananchi limemtafuta Sanare kuhusu taarifa hizo ambapo amesema yuko kwenye kikao eneo la tukio na kwamba atazungumza baadaye na waandishi wa habari.

Diwani wa Mlali, Frank Mwananziche amesema ofisi hiyo ilichomwa majira ya saa nane usiku na watu wasiojulikana.

Hii ni ofisi ya pili inachomwa moto baada ya watu wasiojulikana usiku wa kumakia jana Jumapili Novemba 10, 2019 kuichoma moto ofisi ya mtendaji wa kata ya Soweto katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Chanzo: Mwananchi
Maccm majinga sana ya achoma moto ofis kupoteza ushahidi wa kuiba kura na kuvuruga uchaguzi.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
19,875
2,000
Ina maana hao "Watu Wasiojulikana" sasa wamebadili gia angani hawateki watu tena au kuwajeruhi kwa risasi ila sasa wanachoma nyumba kwa moto.
This is terrible.
Maccm haya tumeyaacha yajipitishe bila kupingwa bado hayaridhiki yanachoma ofisi za wananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom