Mvomero: Ofisi ya kijiji cha Mlali yachomwa moto, vitu vyote ndani vyateketea

CHADEMA wako jela kutumikia kifungo cha kisiasa usiwasingizie,kuchoma moto ofisi na uharibifu wa mali mbalimbali ni cherekochereko za CCM kusherehekea ushindi wa kishindo.
Ndo wachome ofisi.😁😁😁
 
Yalikuepo ya kibiti kuuwa viongozi hasa na yakaisha sembuse haya ...
 
Inatakiwa ipigwe attack kila ofisi ichomwe watakubali mapatanisho tu, saa zingine inabidi ulazimishe mambo yaende
 
Nyaraka zimechomwa na wananchi wamekimbia kijiji kwa kuhofia kukamatwa na police. police wamethibitisha kutokea kwa tukio ilo.
1573534484893.png


=====

Morogoro. Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro nchini Tanzania Wilbroad Mutafungwa amesema watu watatu wanashikiliwa kwa mahojiano akiwemo Diwani wa Mlali (CCM), Frank Mwananziche.

Watatu hao wanashikiliwa kwa mahojiano kufuatia watu wasiojulikana kuchomwa moto ofisi ya serikali ya mtendaji wa kata ya Mlali na kusababisha nyaraka mbalimbali kuteketea kwa moto.

Mutafungwa amesema hayo leo Novemba 11, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea kati ya 8 hadi saa 10 usiku wa kuamkia leo Jumatatu. katika kijiji hicho ambapo moto huo ulibainika kuwaka.

Mutafungwa amesema kufuatia tukio hilo polisi mkoani Morogoro polisi inaendelea kuwasaka watu hao wasiojulikana ili kukomesha matukio kama hayo kuendelea ndani ya mkoa ili ubaki salama.

Amesema anawashukuru wananchi wenye nia njema walitoa taarifa na wao kujitoa kuzima moto huo na kusaidia jengo kutoteketea kabisa.

Akizungumzia tukio hilo, mtendaji wa kata ya Mlali, Alusiasa Mpina amesema alistushwa na simu kutoka kwa raia mwema kuwa ofisi yake inaungua moto naye kuelekea eneo la tukio na ndipo alipokuta ikiendelea kuungua.

Mpina amesema hafahamu nini chanzo cha moto huo kutokana na yeye kuwa amelala na kwamba anahisi unasababishwa na masuala ya kisiasa kufuatia kupokea vitisho hapo awali.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro (RC), Loata Ole Sanare ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wote waliohusika wanapatikana kwani ni suala la uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya wananchi ambalo halipaswi kufumbiwa macho.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom