Mvomero: Ofisi ya kijiji cha Mlali yachomwa moto, vitu vyote ndani vyateketea

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Wilayani Mvomero mkoani Morogoro ofisi ya kijiji cha Mlali imechomwa moto usiku wa kuamkia leo, nyaraka zote muhimu zateketea.

pic+moto+moro.jpg

Watu wasiojulikana, wameichoma moto Ofisi ya Kijiji Cha Mlali kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo Jumatatu Novemba 11, 2019.

Aidha ofisi hiyo imechomwa moto pamoja na nyaraka zote zilizokuwa ndani ya ofisi hiyo zimeteketea kwa moto.

Uongozi wa mkoa wa Morogoro akiwemo Mkuu wa mkoa Loata Ole Sanare pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa wako eneo la tukio wakifuatilia sababu za kuchomwa moto ofisi hiyo.

Mwananchi limemtafuta Sanare kuhusu taarifa hizo ambapo amesema yuko kwenye kikao eneo la tukio na kwamba atazungumza baadaye na waandishi wa habari.

Diwani wa Mlali, Frank Mwananziche amesema ofisi hiyo ilichomwa majira ya saa nane usiku na watu wasiojulikana.

Hii ni ofisi ya pili inachomwa moto baada ya watu wasiojulikana usiku wa kumakia jana Jumapili Novemba 10, 2019 kuichoma moto ofisi ya mtendaji wa kata ya Soweto katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Chanzo: Mwananchi

Zaidi, soma;


 
CCM wameamua kuchoma kila kitu hasa pale penye ufisadi kupoteza kumbukumbu kisha watawasingizia chadema ili wapate kuwabambikia kesi

Hata mimi nina imani kama wewe. Sijui ni kwa nini! Maana haileti mantiki, yaani mtu ameamua kwa hiyari yake mwenyewe kususia huo uchaguzi, halafu aende tena akachome ofisi! For what?

CCM waache kutuchezea akili.
 
Wilayani Mvomero mkoani Morogoro ofisi ya kijiji cha Mlali imechomwa moto usiku wa kuamkia leo, nyaraka zote muhimu zateketea.

Jiografia ya Mvomero bomoa kichwa, kwanini Mlali ipo Mvomero na siyo Morogoro Mjini ambako ni rahisi kupata huduma za serikali kuliko Mvomero?
 
Back
Top Bottom