"MV PROBO KOALA" meli ya Sumu, iliyoleta maafa Ivory Coast

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,947
12,517
MV PROBO KOALA hii ilikuwa ni meli ya kubeba mafuta iliyokuwa imekodiwa na kampuni ya Traffigura yenye makao makuu nchini Singapore. Meli hii ilikuwa na usajili wa nchi ya Panama na kumilikiwa na kampuni ya wagiriki Prime Marine Management Inc.

Meli hii ilikuwa imebeba petrol yenye ubora wa chini kutoka nchini Mexico na kupeleka ulaya ambapo petrol hiyo ilikuwa na kiwango kikubwa cha sulphur na silica.

images (5).jpeg

JINSI UMWAGAJI WA UCHAFU ULIOKUWA NA SUMU ULIVYOTOKEA.
Mnamo tarehe 2/7/2006 meli hii ilipofika bandari ya Amsterdam ilitakiwa kwenda kumwaga uchafu utokanao na kusafisha matenki ya mafuta melini (slop tank). Kampuni na mamlaka ya bandari ya nchini uholanzi walishusha nusu ya uchafu huo, kisha wakaleta pendekezo la kuongeza bei baada ya kutambua uchafu ulikuwa na Sumu Kali zenye madhara. Gharama zilikuwa ni £27 Kwa tani walipopandisha ilitakiwa £1000.

Nahodha wa meli alikataa na meli ikaenda nchini Estonia kushusha mzigo wa petrol, lakini mamlaka za Uholanzi ziliwapa taarifa Estonia kuhusu hii meli hivyo hapo hawakuweza kutupa huo uchafu.

13/07/2006 meli ikasafiri kwenda Lagos na kushusha mzigo hapa nahodha alikataa kutupa uchafu uliobaki, Tarehe 17/08/2006 meli ilikuwa imefika nchini Ivory Coast na tarehe 19/08/2006 meli ikaanza kumwaga uchafu huo katika Bandari ya Abidjan Kwa kutumia Maroli ambayo yalikuwa yakienda kumwaga katika sehemu za kutupa uchafu karibu na makazi na nje kidogo ya mji.

Uchafu huo wa mafuta wa tani 500 ulikuwa na kiwango kikubwa cha Sulphur na silica,kutokana na meli kusafisha mafuta ya coker gasoline na caustic soda na hivyo kuleta Sumu kama sodium hydroxide, sodium sulfide na phenols ambazo zina athari kubwa kwa binadamu.

MADHARA BAADA YA KUTUPWA UCHAFU
Baada ya uchafu huo kutupwa usiku huo watu walianza kusikia harufu Kali na wengine walikuwa wakizimia, kupumua Kwa shida, wengine walipelekwa hospital na watu wapatao 17 walifariki. Wengi walidhurika kwenye ngozi kutokana na phenol na jumla ya watu 30,000 walidhurika. Siku ya Kwanza wananchi walipoona magari yanamwaga mafuta yenye Sumu waliandama na kuzuia magari kwenda kwenye eneo la umwagaji maji taka hayo.Maandamano yalifanyika mji mzima wa Abidjan kupinga tukio Hilo na kuripotiwa na vyombo vya habari nchini kwao na duniani.
images (3).jpeg

MADHARA KUWA MAKUBWA
Baada ya madhara kuwa makubwa serikali ikatoa Tangazo watu wote walio athirika namna moja au nyingine kutibiwa hospital ya taifa ya Ivory Coast.
Umoja wa mataifa na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yakaingila Kati kutetea wahanga na kupelekea kufunguliwa kesi.

images (6).jpeg

images (7).jpeg

SERIKALI YA MPITO BAADA YA TUKIO
Baada ya skendo hii kubwa na serikali ya Ivory Coast kuingia gharama zote za kuwatibu wahanga, Viongozi wakubwa serikalini akiwepo Waziri mkuu Bwana Charles Konan Banny alijiuzuru Kwa hiyari na kusababisha kuwa na serikali ya mpito nchini Ivory Coast.Pia baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa mamlaka husika walijihudhuru.

HUKUMU
Baada ya tukio kiongozi wa Traffigura ukanda wa Africa Magharibi alisafiri kwenda kusaidia wahanga na kujionea madhara, alipofika Ivory Coast yeye na mwenzake wakakamatwa na Serikali ya Ivory Coast Ila waliachiwa baada ya kufikia maridhiano baadae.

Kesi hii ilisikilizwa na mahakama kuu ya Uingereza chini ya mawakili wa kampuni ya Leigh Day & Co na mwisho ikaamuliwa Traffigura walipe kiasi cha £100million Kwa Serikali ya Ivory Coast.

Pia Kwa kila raia aliyedhurika ilibidi apewe fidia, jumla ilikuwa ni USD46 million na kila raia alitakiwa apate USD 1546 Kwa idadi ya watu 31000. Lakini kwenye taasisi zilizoshughulikia ugawaji matukio ya ujanja kama kuandika majina ya uongo mpaka kufikia idadi kubwa iliyozidi na ela nyingine ikaishia Kwa waroho wachache.

ADHABU NA VIFUNGO
Traffigura walilipa fidia kubwa ya mamilioni na walilipa faini ya £67000 ili viongozi wake wawili waliokuwa maboss wa kanda ya Africa Magharibi waweze kufutiwa kesi na kuachiwa.

Wamiliki wa Campagne Tammy kampuni iliyofanya kazi ya kuchukua tenda ya kumwaga mafuta machafu walifungwa, baadhi ya wahusika wa mamlaka za bandari na Captain na msaidizi wake.

NYUMA YA PAZIA
Kila upande ulitoa idadi tofauti ya watu waliodhurika na Kuna habari hii meli ilikataliwa na nchi nyingi za ulaya Ila Traffigura walipofika Ivory Coast kuna viongozi walikubali baada ya kupewa pesa. Traffigura mahakamani walikiri meli ndiyo ilikuwa na kemikali ambazo ni Sumu,Ila lawama wakawapa Tammy kwamba hawakuwa na uwezo wa kukinga na kutoa uchafu wenye Sumu. Wengi waliamini rushwa ndio iliyopelekea Ivory Coast kupata hii skendo iliyoleta madhara makubwa.

Meli hii ilipewa majina kama "Death Ship" na "Toxic Ship" Kwa waswahili ilijizolea umaarufu kama "Meli ya Sumu".

Hii ni link ya Traffigura yenye maswali 13 kuhusu iyo kesi na matukio.

Probo-Koala-toxic-ship.jpg

images (4).jpeg
 
Hapo nilijua tu lzm mlungula umetumika. Baadhi ya weusi wenzetu ni walafi Sana lijapo suala la pesa ni wadhaifu Sana. We cheki watawala wa kiafrica kila mmoja akipata madaraka awakumbuki kuboresha maisha ya watu wao ni kutaka Pesa zote ziwe zao wanakimbizana kuwa tajiri wa kwanza duniani kwa kuiba Kodi za wananchi, kuhongwa rushwa na madalali wanufaike raslimali zetu.
 
MV PROBO KOALA hii ilikuwa ni meli ya kubeba mafuta iliyokuwa imekodiwa na kampuni ya Traffigura yenye makao makuu nchini Singapore. Meli hii ilikuwa na usajili wa nchi ya Panama na kumilikiwa na kampuni ya wagiriki Prime Marine Management Inc.

Meli hii ilikuwa imebeba petrol yenye ubora wa chini kutoka nchini Mexico na kupeleka ulaya ambapo petrol hiyo ilikuwa na kiwango kikubwa cha sulphur na silica.

View attachment 1665618

JINSI UMWAGAJI WA UCHAFU ULIOKUWA NA SUMU ULIVYOTOKEA.
Mnamo tarehe 2/7/2006 meli hii ilipofika bandari ya Amsterdam ilitakiwa kwenda kumwaga uchafu utokanao na kusafisha matenki ya mafuta melini (slop tank). Kampuni na mamlaka ya bandari ya nchini uholanzi walishusha nusu ya uchafu huo, kisha wakaleta pendekezo la kuongeza bei baada ya kutambua uchafu ulikuwa na Sumu Kali zenye madhara. Gharama zilikuwa ni £27 Kwa tani walipopandisha ilitakiwa £1000.

Nahodha wa meli alikataa na meli ikaenda nchini Estonia kushusha mzigo wa petrol, lakini mamlaka za Uholanzi ziliwapa taarifa Estonia kuhusu hii meli hivyo hapo hawakuweza kutupa huo uchafu.

13/07/2006 meli ikasafiri kwenda Lagos na kushusha mzigo hapa nahodha alikataa kutupa uchafu uliobaki, Tarehe 17/08/2006 meli ilikuwa imefika nchini Ivory Coast na tarehe 19/08/2006 meli ikaanza kumwaga uchafu huo katika Bandari ya Abidjan Kwa kutumia Maroli ambayo yalikuwa yakienda kumwaga katika sehemu za kutupa uchafu karibu na makazi na nje kidogo ya mji.

Uchafu huo wa mafuta wa tani 500 ulikuwa na kiwango kikubwa cha Sulphur na silica,kutokana na meli kusafisha mafuta ya coker gasoline na caustic soda na hivyo kuleta Sumu kama sodium hydroxide, sodium sulfide na phenols ambazo zina athari kubwa kwa binadamu.

MADHARA BAADA YA KUTUPWA UCHAFU
Baada ya uchafu huo kutupwa usiku huo watu walianza kusikia harufu Kali na wengine walikuwa wakizimia, kupumua Kwa shida, wengine walipelekwa hospital na watu wapatao 17 walifariki. Wengi walidhurika kwenye ngozi kutokana na phenol na jumla ya watu 30,000 walidhurika. Siku ya Kwanza wananchi walipoona magari yanamwaga mafuta yenye Sumu waliandama na kuzuia magari kwenda kwenye eneo la umwagaji maji taka hayo.Maandamano yalifanyika mji mzima wa Abidjan kupinga tukio Hilo na kuripotiwa na vyombo vya habari nchini kwao na duniani.
View attachment 1665615

MADHARA KUWA MAKUBWA
Baada ya madhara kuwa makubwa serikali ikatoa Tangazo watu wote walio athirika namna moja au nyingine kutibiwa hospital ya taifa ya Ivory Coast.
Umoja wa mataifa na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yakaingila Kati kutetea wahanga na kupelekea kufunguliwa kesi.

View attachment 1665591

View attachment 1665598

SERIKALI YA MPITO BAADA YA TUKIO
Baada ya skendo hii kubwa na serikali ya Ivory Coast kuingia gharama zote za kuwatibu wahanga, Viongozi wakubwa serikalini akiwepo Waziri mkuu Bwana Charles Konan Banny alijiuzuru Kwa hiyari na kusababisha kuwa na serikali ya mpito nchini Ivory Coast.Pia baadhi ya mawaziri na viongozi wengine wa mamlaka husika walijihudhuru.

HUKUMU
Baada ya tukio kiongozi wa Traffigura ukanda wa Africa Magharibi alisafiri kwenda kusaidia wahanga na kujionea madhara, alipofika Ivory Coast yeye na mwenzake wakakamatwa na Serikali ya Ivory Coast Ila waliachiwa baada ya kufikia maridhiano baadae.

Kesi hii ilisikilizwa na mahakama kuu ya Uingereza chini ya mawakili wa kampuni ya Leigh Day & Co na mwisho ikaamuliwa Traffigura walipe kiasi cha £100million Kwa Serikali ya Ivory Coast.

Pia Kwa kila raia aliyedhurika ilibidi apewe fidia, jumla ilikuwa ni USD46 million na kila raia alitakiwa apate USD 1546 Kwa idadi ya watu 31000. Lakini kwenye taasisi zilizoshughulikia ugawaji matukio ya ujanja kama kuandika majina ya uongo mpaka kufikia idadi kubwa iliyozidi na ela nyingine ikaishia Kwa waroho wachache.

ADHABU NA VIFUNGO
Traffigura walilipa fidia kubwa ya mamilioni na walilipa faini ya £67000 ili viongozi wake wawili waliokuwa maboss wa kanda ya Africa Magharibi waweze kufutiwa kesi na kuachiwa.

Wamiliki wa Campagne Tammy kampuni iliyofanya kazi ya kuchukua tenda ya kumwaga mafuta machafu walifungwa, baadhi ya wahusika wa mamlaka za bandari na Captain na msaidizi wake.

NYUMA YA PAZIA
Kila upande ulitoa idadi tofauti ya watu waliodhurika na Kuna habari hii meli ilikataliwa na nchi nyingi za ulaya Ila Traffigura walipofika Ivory Coast kuna viongozi walikubali baada ya kupewa pesa. Traffigura mahakamani walikiri meli ndiyo ilikuwa na kemikali ambazo ni Sumu,Ila lawama wakawapa Tammy kwamba hawakuwa na uwezo wa kukinga na kutoa uchafu wenye Sumu. Wengi waliamini rushwa ndio iliyopelekea Ivory Coast kupata hii skendo iliyoleta madhara makubwa.

Meli hii ilipewa majina kama "Death Ship" na "Toxic Ship" Kwa waswahili ilijizolea umaarufu kama "Meli ya Sumu".

Hii ni link ya Traffigura yenye maswali 13 kuhusu iyo kesi na matukio.

View attachment 1665608

View attachment 1665610
Hao walioandamana wangekutana na polisi wa Tanzania wangeona cha mtemakuni.
 
Naomba kuuliza, hivi haiwezekani meli ikaenda katikati ya bahari (maji ya kimataifa), na kumwaga uchafu wote? au kuna sheria inabana?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Haiwezekani ukatupa uchafu baharini, Kuna Sheria zinazosimamia uchafuzi wa mazingira baharini (Marine Pollution- Marpol 1973/79).

Uchafu unaoruhusiwa kutupwa ni ule uliokuwa treated na hauna madhara kwa viumbe baharini, na ukitupa lazima utoe taarifa wapi umetupa na utunze katika katika kitabu Cha kumbukumbu ukiwa katika meli.
 
Back
Top Bottom