MV Kikwete inazama?

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,554
1,382
Mwelekeo wa uchumi wa Tanzania baada ya miezi 3 ya utawala wa Rais Kikwete ni mbaya kuliko tulivyohofia! Quartely Econmic Review iliyofanywa na BoT pamoja na wanauchumi wengine wa Afrika Mashariki inaonyesha hali ya umbio wa kudorora uchumi ambao kasi yake ni zaidi ya mategemeo ya watu wote.

JK hana dira ya kupambana na energy crisis iliyojitokeza. Athari zake bado zinaongezeka, na haelekei kujihusisha kikweli na kutafuta jibu.

JK alipokea nchi ambayo uchumi wake ulikuwa unakuwa vizuri, na kasi ya kukua kwake ilikuwa inaongezeka kila mwaka, hata kukiwepo ukame. Alikabidhiwa taifa lenye GDP growth rate ya 7% na ambayo ilikadiriwa kufikia 7.2% mwaka huu. Chini ya uongozi wake, GDP growth rate hiyo imeshuka hadi kufikia 5.8%, na inazidi kushuka.

JK alikabidhiwa taifa lenye inflation rate ya 4%, na kwa kipindi kifupi tu ameiacha ikapanda hadi kufikia 5% sasa, na mwelekeo ni kuongezeka siku za karibuni hadi 6%.

Baraza kubwa la mawaziri wa JK na matumizi yao mabaya yameongeza quartely government spending kwa kiasi cha sh. 157 billion. Hizo ni fedha nyingi sana kwa nchi kama yetu.

Interest rate za Treassury bills zilikuwa 10.4% wakati JK anachukua nchi. Sasa zimefika 14.8%. Hii ni rate kubwa sana (linganisha na Kenya ambapo interest rate on Tbills ni 6.7% only).

Serikali ya JK imetumia fedha nyingi sana, lakini wakati huo huo imepunguza matumizi kwenye vitu muhimu kama mikopo ya wanafunzi! UDSM watoto wanahaha njaa kutokana na kutopewa mikopo.

Kinachoogopesha zaidi ni ukweli kwamba hadi sasa, JK amekuwa na maneno mengi lakini matendo hakuna. Anatoa ahadi kibao, lakini maswala muhimu kama mikakati ya kushughulikia tatizo la umeme (and energy as a whole), na inflation, hana muda nayo.

Ndege ya JK ni nzuri, lakini sio lazima aruke nayo kila siku. Atulie ofisini kidogo ajenge VISION ya namna ya kuongoza nchi.

Kwa maoni yangu, JK angepashwa kuendelea kuwategemea Kigoda na Mramba waongoze uchumi wetu. They have a vision while he doesn't. Hao Waswahili anaoambatana nao hawana dira ya maendeleo! Wanatupeleka kwenye umasikini zaidi na zaidi.

Augustine Moshi
 
Mzee Es,

I beg to differ, Augustine ameuliza na kuleta points za maana sana. Inaelekea mheshmiwa Rais bado anafanya mambo ya kufurahisha jamii. Anaendeleza uuzaji wa magazeti, ukiangalia amefanya mambo mengi ya maana kwenye
1.Utamaduni (michezo) kama mipango ya kuleta kocha wa kigeni, kumpokea Nancy sumary, kusalimiana na kuwaalika Ikulu warembo wa Miss Utalii.
2. Kijamii, anapambana na majambazi kwa kasi sana, anafuatilia mali za viongozi waliopita, anafurahisha na endless ahadi zisizotimizika.
3. Uchumi, amefanya zero. angalia statistics za Moshi hapo juu, jana nilikuwa shocked kusikia hela ya kenya ni mara 17 ya hela yetu!!! Dola ipo 1240 kwa sasa, mafuta Petrol lita moja ni sawa na dola moja etc
4. Kisiasa amefanya vizuri maana anatekeleza baadhi ya sera za vyama vya wapinzani. Anaonyesha nia nzuri ya kushugulikia matatizo ya Muungano.

Mzee Es, Augustino hakuongelea ndege bali ameongelea mobility ya jamaa, amejaza washikaji wengi kwenye baraza lake, wengi wakiwa na kashfa kama David, au naibu waziri wa madini ambaye pia ni mkurugenzi/mwanahisa wa kampuni ya madini!!!!!

Kazi kwelikweli!!

FD
 
Mimi kama kawaida nasema juhudi za ndugu JK nitaanza kuzisemea baada ya miezi 6 ya yeye kuwa ofisini.Nina sababu moja kubwa nayo ni kwamba bado hajaanza kazi rasmi maana anaendelea na ahadi kama vile bado kuna uchaguzi unaokuja mwezi ujao.Hata aliyo yafanya bado ni machache sana hajagusa makubwa kama Mikataba ambayo tayari serikali yake inaanza kupata kashfa kwa kuwa na washikaji wake wengi na leo wanaenda kuangalia mikataba ya madini .Kwa nini JK kama yuko serious na mikataba hiyo asipeleke Tume huru na yenye wataalam hata wa kisheria kujua yaliyo jiri na watu wa Takuru na pia watu wa dini iloi kuhakikisha hakuna kuhongana na kufichiana ubaya ?Hili si swala dogo hata kidogo na hii ni huge test kwa JK .
 
Augustine: Ahsante sana kwa hiyo shule ndugu yangu. Palipo na ukweli uongo hujitenga.

Staili za uongozi zinatofautiana. Lakini hii staili ya bwana misifa JK mimi imeshaniacha hoi. Kila siku ni kutafuta makofi. Na kwa wataanzania tulivyo, tutampigie kweli makofi, lakini in the long run, sijui mungu atusaidie.
 
Msimlaumu JK kwani meli aliyoachiwa ilikuwa na matundu mengi sana na sasamaji yameanza kuingia ndani ,siwezi kushangaa kama meli hiyo itazama na kama kweli akitaka meli hiyo izame basi awarudishe akina KIgoda na Mramba ambao ndio wahusika wakubwa katika kutoboa matundu katika meli yetu.Msiwe na wasiwasi na statistics hizo lengo lake nikupunguza kasi ya JK katika kupambana na majambazi walioiibia serikali yetu na kujilimbikizia mali hali inayojitokezandio matunda ya ujambazi uliofanywa na administration iliyopita .Tusimlaumu JK kwahaya kumbukeni kwamba natural gas itambeba vizuri sana .
Hongera JK endelea na kupambabana na wezi na walioiba mali yetu wote wachukuliwe hatua za kisheria na warudishe mali zetu zote walizoiba kutoka kwetu.Augustine kazungumzia kuhusu wanafunzi kukosa mikopo lakini amesahau kwamba pesa zote zilichukuliwa na baadhi yawatu walioukuwa katika uongozi wa juu na ni watoto wao ndio wanaosomeshwa nje ya nchi,wengine tunakutana naoviwanjani .JK atawanyamazisheni midomo kama ilivyotokeakwenye mbio za urais.

peace!!!
 
Willo,

Serikali iliyopita ilimwachia JK Treassury iliyojaa mapesa. Mwinyi ndiye Rais aliyengia madarakani na kukuta Treassury kweupe, lakini BWM na JK wamekuta hali nzuri. Yeye JK alipokea uchumi ambao ulishaanza kuonja quarterly balance of payements surplus ya $111.8 million, na international reserves za kutosha imports za miezi 8.

Mzee Es,

Ndege nimeitaja kwa maana ya JK kuzunguka zunguka mno akishikana mikono na watu, bila kutenda kazi zake za kuimarisha uchumi vizuri. Bahati mbaya, huko kuzunguka kwake wala hakuinui international profile ya Tanzania. Inazidi kudidimia. Naona hata Rais wa China amefika Nairobi na kuacha kuja kwetu. Yaani hata Wachina wanatuona si wa maana tena.

Zamani tulionekana wa maana kimatiafa, na ilitokana na kuwa na Rais (Mwalimu) mwenye interesting ideas. Mkapa naye alionekana ana ideas za maana, na kwenye mikutano ya kimataifa aliyohdhuria, Tanzania ilitajwa sana na maoni yake yalitafutwa. Huyo JK wenu alipoulizwa na waandisha wa Uingereza kuhusu msimamo wa Tanzania juu ya Zimbabwe, alisema tutaangalia nchi nyingine zitaamuaje kisha ndiyo tuamue. Tangu siku hiyo anaonekana ni mtu asiye na maoni yake mwenyewe.

Hizo hisia kwamba JK anapambana na majambazi mmezileta wapi? Yaani kuteua IGP mpya na kuwahamishia ma RPC makao makuu ndio umeshapambana na majambazi? Mbona majambazi yenyewe yanazidi kushamiri? Tena kuna wasiwasi kwamba ni askari wenzake ndio wanatupora kwa silaha za jeshi. Naona itabidi wajaribu kuficha na kufunika, kwani ni hatari na aibu kama maofisa wa jeshi wanatumia mapanga ya taifa kuwapora wananchi.

Augustine Moshi
 
Mzee Es na willo,
Jamani mwacheni Augustine anapenda vibaya mwenzenu wala halioni chongo!. Hizo takwimu zke nimezipitia toka benki kuu na ajabu hakusoma maelezo ya takwimu za miaka ya nyuma. Tena labda nichukulie kipindi alichozungumzia - Kati ya January hadi kufikia Dec 2005. Kuna vipengele kama hivi:-

1. During the quarter ending December 2005, annual average inflation rose to 4.8 percent, from 4.5 percent, recorded during the quarter ending September 2005. The upward pressure on inflation emanated from increased food demand in the domestic market and in the neighbouring countries which led to acceleration in food inflation from 6.3 percent to 6.9 percent.

Kwa hiyo sioni ajbau kuwepo kwa hilo ongezeko ktk kipindi cha miezi mitatu ya JK.
Fikiraduni, ndugu yangu Hiyo shillingi 17 kwa Kenya moja ipo miaka sasa! Mimi nimewahi kuzungumzia Bcstimes nikifananisha na Mchonga ambaye aliondoka mwaka 1984 tukiwa 1Ksh kwa 10 za Bongo. Imeendelea hiyo pamoja na mabadiliko yote ya Dollar lakini miaka kumi hii ya mwisho ndipo Kenya wameweza kupiga hatua mpya dhidi ya shillingi yetu hali Mkapa na watu wake wanaendelea kudai tunaendelea na hiyo GDP yao. Kumbuka mwinyi aliondoka dollar ni Tsh. 550, yote mmeyafumbia macho!Pia toka Takwimu za BOT mwaka huo 2005 angalia kipande hiki toka benki kuu wakati huohuo wa Mkapa kinasema nini?

2. The Tanzanian shilling on average depreciated by 2.2 percent in nominal terms against the US Dollar, moving from an average of TZS 1,134.8 per US dollar, recorded during the quarter ending September 2005 to an average of TZS 1,160.2 per US Dollar as at the end of December 2005.
Sasa hivi kweli mnafikiri JK ni Yesu wa kuja na kubadilisha vitu kimiujiza?...samaki mmoja ni mmoja tu akishaliwa kipande basi ndio imetoka!
Mwisho kabisa kuna vitu kama hivi yote ktk Utawala wa Mkapa, lakini mwenzetu kayapamba kwa mafuta ya nazi, harufu yake si utuli bali vundo!
4. The overall central government budget deficit (before grants) widened to TZS 651.0 billion from a deficit of TZS 302.1 billion recorded during the quarter ending September 2005. After considering grants, the deficit was reduced to TZS 303.2 billion. Revenue collection amounted to TZS 548.9 billion, being TZS 28.6 billion above the targeted amount for the quarter. Total expenditure amounted to TZS 1,087.2 billion, which was also higher than the budgeted amount of TZS 798.8 billion for the quarter.
Unatengeneza tano matumizi kumi, robo yake hayana supporting documents! kweli tutafika?
5. Total national debt (domestic and external) stood at US$ 9,383.9 million as at the end of December 2005.
 
Mkandara,

Naomba kutoa heshima za dhati kwa kazi uliyotuletea hapo juu, umetumia muda wako na kuweka mambo sawa.
Nakubaliana na wewe kuhusu mheshimiwa Moshi naona hataki ukweli, na anajaribu kukwepa maswali. Ninaomba ajibu yafuatayo(ambayo ameulizwa kwenye topic mbalimbali)

1. Mzee Es ameuliza hiyo mikopo waliyopata ndani ya miaka kumi akina BWM na wenzake inatolewa wapi? na sisi tunataka
2. Nimemuuliza kuwa tukienda TRA kuangalia kodi iliyolipwa na mama BWM itaoana na mali alizonazo? maana kila income au deemed benegit lazima iwe taxed (kama ni employee). Kama anatumia mgongo wa NGO, je mahesabu yapo sawa?

Tuanze na hayo.

FD
 
Acheni kutumia ukame kusawazisha dosari zote. Kenya nao walipata ukame kama sisi, lakini uchumi wao umeendelea kuimarika. Nimekupeni mfano wa low interest rates on Tbills za Kenya, ambazo zimeshuka wakati huu wa ukame hadi kufikia 6.7%, wakati zetu zikipanda hadi 14.8%

Ukame wa msimu mmoja haupashwi kozorotesha uchumi kama ilivyotokea kwetu. Ni uongozi mbaya, sio ukame, ndio unafanya tusiwe na umeme hadi sasa. Uongozi mzuri ungeshatatua hili tatizo.

Mnaniuliza kama mtu anaweza kupata mikopo ya kujenga apartment block. Ndiyo anaweza, mradi awe na mali ya kuweka dhamana. Hata wewe Fikiraduni, kama una mali ya kuweka dhamana ya kutosha, unaweza kupata mkopo mkubwa sana. Sijui kama Mkapa amechukua mkopo, lakini mali ya kuweka dhamana anayo. Ingekuwa ajabu kama baada ya kufanya kazi kubwa kubwa miaka kama 40 hangekuwa na mali ya kuweka dhamana.

Fikiraduni anauliza kama mtu akienda TRA atakuta Mama Mkapa amelipa kodi inayolingana na utajiri wake. Siju kama Marais wastaafu na wake zao wanalipa kodi. Naomba kuelimishwa. Mwalimu alikuwa analipa kodi? Kama wanapashwa kulipa kodi, basi sina shaka Mama Mkapa atakuwa analipa kodi inavyotakiwa.

Haya Fikiraduni, leta maswali zaidi, maana niko tayari kuyashughulikia.

Nimwambie Mkandara hivi: JK hakukuta uchumi mbaya. Alikuta uchumi unaokuwa kwa kasi kubwa (7% per annum), na umbio wenyewe ukiongezeka from quarter to quarter. Ameweza kuubomoa kwa kipindi kifupi sana.

Natabiri kwamba kwa mtaji huu, uchumi wetu utarudi kuwa tena mahututi kabla JK hajamaliza miaka mitano ya Urais.

Augustine Moshi
 
Augustine,
Kwanza hiyo quarterly balance of payment surplus ya $111.8 million ni kitu gani labda tueleze unaposema JK kaachiwa mapesa kibao! nashindwa kuunganisha na madai yako. Unapokopa zaidi mwaka huu kuliko mwaka 1996 na kuagiza zaidi mali toka nje kuliko export zako ina maana ni mahela zaidi?
Pili, Naomba sana ndugu yangu stick na vitu ambavyo unavifahamu kwa uhakika... Unaposema Kenya interest rates zimeshuka wakati wa ukame hali sisi zimepanda una maana ipi hapa kwani navyofahamu mimi interest za karibu nchi ZOTE duniani zimepanda kutokana na kupanda ghafla kwa bei ya mafuta. Na iwapo wao hawakupandisha kutakuwepo na madhara/faida ambayo wachumi wake wameyatazama. Kila Uamuzi wa kupanda na kushuka kwa interest kuna matoikeo tofauti na kila nchi benki yake kuu hutoa maamuzi kulingana na hali. Umekazania Umeme kuwa ni kosa la JK sijui hii imetoka wapi kwani hiyo taarifa ya serikali yako ya mwaka 2004 ilisema hivi:-

The sharp increase in fuel is also attributable to the drought as hydroelectricity was replaced by thermal power produced with petroleum. While there are some concerns about the impact of high oil prices on the
balance of payments, the value and volume of petroleum imports are actually estimated to have fallen in 2004/2005, due to resumption of hydroelectricity production as well as due to the introduction of natural gas as a substitute for petroleum.
As of October 2004, the production of clean, reliable, efficient electricity generated from Tanzania’s indigenous gas reserves extracted
from SongoSongo Island in Kilwa (and transported through a 225 km long pipeline to the Ubungo Power Station) had reached 115 megawatts.
Due to agreements finalised in November 2004, the total capacity of electricity generated from Tanzanian natural gas will increase to
180 megawatts by April 2005, which is enough to meet over one third of Tanzania’s peak demand and the whole of Dar es Salaam’s
power requirements.

Sasa ndugu yangu nambie KULIKONI?.. si mlifikia kufunga kabisa agreement nakutoa ahadi? fedha zimekwenda wapi? maana umeme bado hakuna! ktk estimate hizo za Mkapa na hao IMF kuna kipi kimewasibu! Mkopo mliupata wa kutosha leo yote unayafumbia macho na kumbebesha JK mzigo aliouacha Mkapa. Leo unatazama ahadi za JK kabla hata mwaka haujesha...Mshikaji GDP kwa quaterly hasa toka Jan hadi Mar haijawahi kuwa nzuri ktk historia ya nchi yetu. Huo ni wakati wa kulima na kupanda sio wakati wa mavuno, na biashara zote duniani zina msimu wake -
High na low kwa hiyo usianze kuchanganya vitu, jaribu kupata taarifa kwa nini kumetokea upungufu kabla hatujalaumu. Ikiwa haiingi akilini hapo unaweza kabisa kutupa picha inayoeleweka.
 
Mkandara,

Kama ni kweli huelewi hiyo balance of payments surplus ni kitu gani, basi itabidi ujisomee; kwa sasa sina muda wa kukufundisha hapa.

Unaweza kuangalia kwenye site ya Central Bank of Kenya, kuona kwamba riba kwenye hundi zao za hazina imekuwa ikishuka, kwa wastani. Hili limetokana na ukweli kwamba kwa kipindi cha wiki 16 mfululizo, kiasi cha fedha ambazo serikali ya Kenya imetaka kukopa kwa kutumia Hundi za Hazina ni kidogo kuliko wingi wa fedha za waliotaka kununua hizo hundi. Kwa mfano, kwenye mnada wa Hundi za Hazina wa tarehe 27.4.2006, kiasi cha fedha zilizotolewa ili kununulia hizo hundi zilizidi thamani ya hundi zilizotolewa na serikali kwa asilimia 29.6. Wiki iliyotangulia, kulikuwa na ziada kama hiyo ya asilimia 32.9

Ukusanyaji wa kodi Kenya uliongezeka katika kipindi cha ukame vile vile. Kati ya Julai 1, 2005 na April 20, 2006, mapato ya serikali ya Kenya yalifikia Ksh. 218,460 million (Tsh. 3.714 trillion). Linganisha na Ksh 199, 144 million (Tsh. 3.385 trillion) zilizokusanywa katika kipindi kama hich mwaka wa fedha uliotangulia.

Katika kipindi cha wiki iliyomalizikia April 20, 2006, ukusanyaji kodi wa serikali ya Kenya uliongezeka hadi kufikia Ksh. 7, 876 million (Tsh 133.892 billion). Linganisha na Ksh 5,315 million (Tsh. 90.355 billion) zilizokusanywa wiki iliyotangulia

Sasa ukusanyaji kodi wa JK umepungua kwa silimia 20, na mnasema ni ukame. Mbona ukame haujaharibu ukusanyaji kodi Kenya?

Serikali ya JK si ya UWAZI. Wamekuwa waongo kwenye swala la umeme. Kwa sasa, wanarudisha mgao eti kwa vile maji yameshuka ghafla huko kwenye mabwawa. Maji hayashuki ghafla wakati mvua zinanyesha. Na wanaanza kuonyesha dalili za kutawala kwa intrigue Tunapenda UWAZI alioanzisha Mkapa uendelee. Msifiche majina ya majambazi mliyokamata, hata kama ni wanajeshi. Na toeni taarifa za mapato na matumizi ya serikali, kila mwezi.

Kuna tatizo la umeme, na serikali imeshindwa kulishughulikia ipasavyo.

Augustine Moshi
 
Augustine,
Sina hata la kukueleza maanake naona unalitengeneza FUFU (ugali wa Kighana) ambalo huchanganywa mahindi, nyama ya kuku, ngombe samaki na bila kusahau maharage.
Sasa ebu nikuulize ikiwa Kenya wamekusanya ama ununuzi wa hundi unahusiana vipi na uchumi wa Tanzania. Huwezi kabisa kufananisha nchi kwa nchi ktk maswala ya kiuchumi kwa sababu nyingi sana. pamoja na kuwa GDP yetu ilikuwa imepata kwa asilimia sijui 7, hiyo asilimia wakiiweka kifedha unaweza kukuta kiwango hicho ni asilimia 1 tu ya nchi nyingine. Kenya wanachukua hatua za kiuchumi kulingana na koti walilovaa hatuwezi kuwa sawa hata kidogo na ukitaza hatua za benki zao ni ktk jitihada za kushusha Inflation rate yao ambayo imepanda kishenzi toka 5% dec na sasa imesimama 19% kutokana na kupanmda bei za mazao ya chakula. Lakini wao wanaondoa takwimu zinazoathiriwa na chakula, na mafuta kwa hiyo kinachoonekana ni inflation kuwa chini zaidi yetu ama nchi nyingine zinazoambatanisha mafuta. Haya exchange rate yao imesimama 70 kwa muda wa miaka isiyopungua saba hali sisi ukitazama kiama hiyo kumi iliyopita utaomba ardhi ipasuke! Ukitazama Uingereza, Marekani, Germany, Japan na nchi zote za magharibi... hazichukui hatua sawa za kiuchumi na sababu ni kwamba - Suluali alovaa Marekani haimtoshi kila mtu na wala sio kila mtu anapenda kuvaa mchelemchele!

Nikishuka hapo chini umenakiri ukusanyaji wa Kenya kwa miezi sita (July to Dec) kama kigezo cha kumshutumu JK miezi 3! wapi na wapi? Je, kuna uhakika kiasi walichokusanya Kenya ni kikubwa kulingana na uchumi wao?. Ikiwa wewe Augustine mshahara wako ni millioni na mimi ni laki tano hatuwezi kuwa na matumizi ama mapato sawa pamoja na kwamba sote tuna malengo ya kuendelea. Ukibana kula maharage sii lazima mimi pia nile maharage kuonyesha kwamba laki tano hazitoshi kula kuku. Mwenzako kuku wangu nawatoa huko Mwibara bei poa sawa na kilo ya maharage sokoni Kariakoo.
 
Mkandara,

Hilo la Kenya nililileta mwanzoni kama kielelezo kwamba kukosa mvua msimu mmoja sio lazima kuharibu uchumi. Kenya wamekuwa kwenye ukame kama sisi.

Ukusanyaji wa kodi chini ya JK umeshuka kwa 20%, na wewe na wengine mkasema ni shauri ya ukame. Hapo ikabidi niwaleteeni data kuonyesha kwamba pamoja na ukame, ukusanyaji kodi Kenya umepanda.

Kwa taarifa yako (na kujibu swali lako), ukusanyaji wa kodi Kenya, kama asilimia ya pato la taifa (tax revenue as a fraction of GDP) umezidi Tanzania miaka yote. Sababu ni nyingi, lakini chimbuko la sababu zote ni kwamba Kenya walikazania Elimu tangu miaka ya sitini. Educational levels in Kenya are about four times what they are in Tanzania. Thanks to Mwalimu, hata Waganda wamesoma kama mara tatu zaidi yetu.

Inatisha kuona serikali ya JK imeongeza matumizi kwa kiasi kikubwa wakati ambapo ukusanyaji wake wa kodi umeshuka kwa kasi kubwa. Haingii akilini.

Pamoja na kuanza kuvuruga uchumi kwa hali ya juu kabisa, bado JK anashangiliwa na wananchi wengi. Hili linatokana na hali duni ya Elimu nchini. Watu hawaelewi kinachoendelea. Rais akishakuwa na tabasamu nzuri na akatoa ahadi kem kem kila upande basi wanadhani lazima anatawala vizuri.

Augustine Moshi
 
Augustine,
Vitu vingine mshikaji unaongeza chunvi kutokana na unavyojisikia...
Huwezi kabisa kulinganisha Kenya na Tanzania kwa kila hali. Wao infrastructure imesimama zaidi yetu, viwanda na hata system yao ya ukusanyaji kodi imetumika miaka nenda rudi ukichanganya na kodi ya kichwa wakati sisi bado wajamaa. Huwezi kusema Kenya elimu yao ipo juu mara nne yetu au Uganda na kuunganisha swali hilo na ukusanyaji fedha za kodi. Matapeli wakubwa wa kodi Kenya na Afrika yote ni wasomi haohao, bnado vitu hivi havina uzito. Elimu muhimu sana lakini kurudi miaka 40 nyuma kutafuta sababu hiyo tena umetoka nje. wanafunzi wa Nyerere ndio kweli wanaoiongoza TZ leo hii wao sii wazalishaji tena.. tunasubiri kustaafu. Mtoto aliyesoma darasa la kwanza 1985 wakati wa Mwinyi ndiye anatakiwa kuwa mzalishaji leo hii...Yule aliyeanza 88 hadi 90 anatakiwa kukuta hali nzuri ya secondary wakati wa Mkapa na hivyo hivyo... Sasa ikiwa Mkapa kweli ameweza kufanya la maana mbona hiyo mara nne ipo toka tupate uhuru? tena nachojua hapa unahesabu wingi wa wanafunzi, jukumu la Mkapa kuhakikisha wimbi linalokuja anaweza kukabiliana nalo....Na kwa nini Mkapa asitusogeza mbele kidogo ionekane hata wanafunzi wa Kenya na Uganda wanapenda kuja soma TZ.
Kuhusu Ukame, nimekwisha sema hizo takwimu zako ni makosa kwa sababu Kenya wamekusanya kwa miezi sita 6 hali JK ni miezi mitatu 3. Inflation hawaweki chakula na mafuta ktk kupima inflation yao! Yaleyale tunayokwambia kila siku... takwimu siku zote zina vipengele vyake na sio lazima vifanane. leo hii China wanaibomoa Marekani kwa kila hali lakini utasikia Bush akidai nchi yake pato linazidi kuongezeka!Kuna maendeleo leo hii kuliko wakakti wowote ule na kadhalika yote haya ni lugha za siasa ktk biashara! -Marekani wanafahamu kwamba China imewakalia kooni na hasa kuungana sana kibiashara na waafrika na waarabu. Sudan wameondoa mkataba wa mafuta na Marekani wamewapa China..Darfur imeibuka tena upyaaa hali watu bado walikuwa wakifa ktk kipindi cha miezi sita iliyopita!
 
Mkandara,

Vitu vingine mshikaji unaongeza chunvi kutokana na unavyojisikia...Huwezi kabisa kulinganisha Kenya na Tanzania kwa kila hali
.

Why not? We have a similar background. Walipata uhuru mwaka mmoja baada yetu, na kuna wakati hata sarafu yetu ilikuwa moja. They left us behind when we had a policy of running while they walk!

Wao infrastructure imesimama zaidi yetu, viwanda na hata system yao ya ukusanyaji kodi imetumika miaka nenda rudi ukichanganya na kodi ya kichwa wakati sisi bado wajamaa
.

Sasa hilo ndio linakataze kujilinganisha nao? Na system yetu ya kukusanya kodi iko muda mrefu kama ya kwao. Au unadhani hatukuwa na kodi wakati wa ujamaa?

Huwezi kusema Kenya elimu yao ipo juu mara nne yetu au Uganda na kuunganisha swali hilo na ukusanyaji fedha za kodi
.

Naweza, kwani fedha inayotokana na ukusanyaji mzuri wa kodi ndiyo imewasomesha.

Matapeli wakubwa wa kodi Kenya na Afrika yote ni wasomi haohao, bnado vitu hivi havina uzito
.

Aheri tapeli msomi kuliko tapeli ngumbaru. Tapeli msomi anapoacha kulipa kodi, fedha anafanyia kazi za uzalishaji; serikali inanyimwa fedha lakini nchi inajengeka. Tapeli lisilosoma hutumia fedha zilizotakiwa zilipwe kodi kuolea mke wa pili au hata wa tatu. Serikali inakosa fedha na taifa linabebeshwa mzigo wa kulea watoto wake wengi.

Sasa ikiwa Mkapa kweli ameweza kufanya la maana mbona hiyo mara nne ipo toka tupate uhuru
?

Chini ya Mkapa na Mungai, tulianza kupunguza hilo pengo la elimu kati yetu na Kenya na Uganda, kwaa kasi sana. Hata idadi ya watoto wetu walioona umuhimu kusoma kwao ilianza kupungua. Sasa huyu JK na mwenziye Mama Sitta sio wazuri hata kidogo kwenye nyanja ya elimu. Wameanza kuingilia shule za private. Hawajui kwamba ndizo zilianza kuokoa elimu yetu.

Tena nachojua hapa unahesabu wingi wa wanafunzi

Sasa kumbe nihesabu nini? Wingi wa madarasa? Nehesabu asilimia za wanafunzi zilizopo shuleni vile vile, na asilimia za kufaulu, etc.

Kuhusu Ukame, nimekwisha sema hizo takwimu zako ni makosa kwa sababu Kenya wamekusanya kwa miezi sita 6 hali JK ni miezi mitatu 3
.

Nilikupa vile vile takwimu kuonyesha ukusanyaji kodi Kenya umeongezeka miezi hii ambapo KJ ameshusha ukusanyaji kodi kwetu kwa 20%. Nimekupa takwimu zionyeshazo kwamba Mwezi Aprili 2006, ukusanyaji kodi Kenya uliongezeka kwa 32%. Acha kusingizia ukame kwa kila kitu.

Augustine Moshi
 
Augustine,
Nimesema unapenda kuongeza chunvi panapokupendeza na nitakwambia kwa nini na mifano yake! Unafananisha uzuri wa mke wangu kwa mke wako... wapi na wapi?...kinachotupendeza TZ sii lazima kiwe sawa na Kenya...chongo kwao sii kilema. Nipe mazuri ya baba Mkapa kulinganisha na baba JK! na sio nyumba ya pili Kenya.
Quote yako ya kwanza:-
Kupata uhuru sawa sii hoja kwani kuna watu wamezaliwa siku moja saa moja na dakika moja bado mmoja akawa amezaliwa ktk mazingira bora kuliko mwenzake! Hii ndio hali tuliyokuwa nayo Tanzania, ikiwa utapima basi pima walioyafanya Kenya baada ya Uhuru. Kenya kila kitu wamekikuta kama vile mtoto wa Freeman, Kingunge bila kumsahau Mkapa huwezi kulinganisha mafanikio yao na ya mwanao kama utaweka fadhila na urahisi waliopata toka kwa wazazi wao.

Ya pili, infastructure yao ilikwisha jengwa na mkoloni, wenzetu waliendeleza system ya kodi iliyowekwa na Mkoloni (kodi za kichwa n.k) wakati Tanzania tuliondoa kabisa minyororo hiyo na kutumia UJAMAA kama njia bora ya kukuza maisha ya wananchi. Kenya kila raia wake ana kitambulisho ambacho kinatumika kama social security number kinaitwa - KIPANDE, hii imewasaidi sana hali Mkapa na elimu yake kashindwa kuanzisha kitu hicho zaidi ya kugawa mirathi yetu. Kumbuka pia ukusanyaji wa kodi hauhesabiki kwa total amount ulizokusanya ila ufanisi ktk ukusanyaji wa hizo kodi. Mathlan kuna watu millioni mbili wanaotakiwa kulipa kodi, TZ ikakusanya billioni nne toka kwa wananchi milioni moja na nusu hali Kenya ikaweza kukusanya mara tatu ya kiwango cha TZ lakini toka watu millioni tu. Wao watakuwa na uzembe pamoja na kuwa wamekusanya nyingi zaidi yetu!
Hii yote inategemea walipaji, asilimia pamoja na wingi wa kodi hizo. Kuna kodi ambazo zipo Kenya hatuna TZ na nyingine tunazo sisi Kenya hawana! - nadhani upimaji mzuri wa kodi ni ule unaowahusu viongozi wa nchi moja say..Mkapa na JK katika kipindi cha budget ya rais huyo! Pia kumbuka kukusanya kodi kubwa sio mafanikio ikiwa kodi hizo ni mzigo kwa wananchi, hii sio maendeleo wala sifa wakati mwingi ktk uchumi unafuu wakodi huzidisha uwekeshaji na kuwahamasisha wananchi wazalishaji kufanya kazi na kuzalisha zaidi. Kwa hiyo kila sera ina matokeo tofauti kiuchumi.
Quote ya Tatu,
Ikiwa kweli ukusanyaji mzuri wa kodi ndio umewasomesha Wa Kenya imekuwaje Mkapa kashindwa kusomesha Watanzania hali umedai kwamba ukusanyaji wake ni mzuri?... tazama mada ya elimu!
Quote ya nne,
Tapeli msomi huzifanyia kazi?... mbona wezi wote ktk serikali ya Mkapa ni hao wasomi na billioni zao hazionekani. Akina Sumaye na Mkapa mwenyewe hizo fedha wanalipa kodi gani wakti fedha zao ziko benki ya Uswiss? Tapeli asiyekuwa msomi hana access ya benki hizo kwanza hajui kama zipo. Hawezi kuiba kodi isipokuwa msomi wa TRA ambaye anaweza kucheza na figures ndani ya PC... wameyafanya haya na bado wanayafanya wengine wanakimbilia nchi za nje baada ya kulipua. Tapeli asiyekuwa msomi ofisi yake ni Kongo street! Akikamatwa kwa tuhuma tu hana bond, maisha yake jela bila hukumu hali msomi ataweka wakili na kutoka nje hata kama ushahidi unamfunga...kesi yake itachukua miaka na mwisho wake kufa, ndio ya akina Mkapa hayo utumiaji nguvu kuondoa report ya Warioba na kuita wananchi wavivu na wajinga!..ATC,TTCL, NBC yote yamefanywa na wasomi na itachukuwa miaka kumi ijayo kuweza kukusanya hata robo ya fedha tulizopoteza.
Quote ya nne,
tupe hesabu ya kutosha kuhusu mafanikio ya Mkapa... For the first time TZ tumeweza kuwa na watoto wanaoitwa CHOKORAAA!.. majambazi ni dalili kubwa ya watu kutokuwa na mbinu za kimaisha kwani elimu hawana ktk ulimwengu wa biashara. Darwin's nightmare na hao World vision ni dalili kubwa ya umasikini wa ELIMU. Elimu sii wingi wa kukaa darasani ila uwezo wa kuanzisha na kuendesha miradi ya uzalishaji.
Quote ya tano,
Ubora wa elimu tazama tena mada yako ktk ELIMU...jibu unalo mwenyewe.
Quote ya sita,
Bado unalinganisha wingi wa machungwa na ndimu ndani makapu mawili!...Kenya wakikusanya mara kumi yetu bado haina maana wanafanya vizuri ikiwa hatufahamu ni kiasi gani kinatakiwa kukusanywa kwao pia kama kodi hizo zinaongezauzalishaji nchini mwao ama zinaathiri!..Kupanda kwa kodi 30% unakokuzungumzia Je, unaweza kutupa umezipata wapi?..I mean toka Jan to March 2006.
 
Naomba ninukuu sehemu ya taarifa iliyoko kwenye magazeti ya leo (ippmedia.com)

Serikali ya JK yajenga shule

2006-05-03 14:34:36
Na Badru Kimwaga, Jijini


Serikali ya awamu ya nne iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete (JK) imefanikiwa kujenga shule mpya za sekondari 381 nchini kote ndani ya kipindi cha miezi minne tu tangu Januari hadi April mwaka huu.

Kadhalika, shule nyingine 70 zimeomba kuongeza mikondo na kufikia 87 katika kipindi hicho.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa itaongeza kiwango cha elimu nchini kwa wastani wa asilimia 50 na wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza, kupata nafasi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi. Margareth Sitta Jijini Dar es Salaam katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Elimu, Bi. Hidaya Mohammed. ...

Nadhani wana maana kwamba kati ya shule alizoanzisha Mkapa kujenga mwishoni mwa uongozi wake, wao (JK and company), wamemalizia 381.

JK alihitaji muda mwingi kupindukia kutaja mawaziri wake. Mtu wa mbio hizo hawezi kujenga shule kuanzia mwanzo hadi kuikamilisha kwa miezi 4. Kujenga shule mpaka ikamilike kunachukua karibu mwaka mzima. Sasa Mama Sitta anaamini kuna Watanzania watakaokubali kwamba yeye na bosi wake wameweza kujenga shule mpya 381 katika kipindi cha miezi 4?

Kama kuna mtu hapa ameamini hiyo danganya toto ya hali chini kama hii, basi naomba ajitokeze ili atueleze tuone kama kinaeleweka.

Nasikitika vile vile kuona kwamba JK ameamua kutumia fedha zilizokusudiwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa shughuli nyingine. Kwa nini wanafunzi UDSM wasipewe mikopo yao ambayo ipo kwenye bajeti?

Kama inabidi JK apunguze matumizi ya serikali ili kulipia kudorora kwa ukusanyaji kodi, basi aangalie upya idadai ya mawaziri. Hatuhitaji mawaziri 60. Ishirini au hata kumi na tano wangetosha kabisa. Mbona nchi kubwa kama Ujerumani zinafanya kazi zake vizuri kwa kutumia mawaziri chini ya 20?

Kuhudumia mawaziri 60 ni Msalaba mkubwa ambao JK amewabebesha Watanzania. Asidanyike mtu kwamba tunahitaji mawaziri 60.

Augustine Moshi
 
Moshi,

Naona unamuonea bure JK. Mwaka huu kumekuwa na mkazo mkubwa
kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi kwenye shule za secondari za serikali.

Kuna shule nyingi sana zimejengwa mwezi wa kwanza kufuatilia tamko la serikali.

Binafsi sikubaliani na suala la uwingi wa shule kwani naona ubora ni muhimu zaidi ya uwingi lakini bado naona kwa hili la kujenga shule
JK na serikali yake wamejitahidi sana.

JK na Lowassa walitoa order kwa serikali za wilaya kuhakikisha kila aliyefaulu anapata shule na ndio imesababaisha hizo shule kuongezeka ghafla na wala sio matokeo ya serikali ya BM.

BM alikuwa hana mpango na wananchi wanyonge. Angelikuwa yeye hizo shule za watoto wa vizito na matajiri ndio zingeongezeka au angeendelea
kutaka kupeleka watoto Uganda, Kenya na hata SA.
 
Back
Top Bottom