MV Kigamboni ilituletea hofu iliposhindwa kutia nanga leo

Namba7

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
223
250
Leo alfajiri ya saa 04:15 kivuko cha MV Kigamboni kilishindwa kutia nanga kutokana na mawimbi makali sana.

Ilikuwa hivi; Mv Kigamboni iling'oa nanga saa 04.05 kutokea upande wa Ferry kuelekea Kigamboni.

Hali ya bahari haikuwa shwari kwani kulikuwa na upepo na mawimbi makubwa kiasi.

Tulipokaribia Kigamboni ilionekana maji yamejaa sana hadi kukaribia sehemu ya abiria kupumzika wakisubiria kuvuka hali amabayo sijwahi kuona. Slops ambapo jembe au flat surface ya kivuko hugusa ili watu washuke na kupanda zilionekana kidogo sana hasa ya kushoto.

Tulipokaribia kutia nanga kivuko kilipeperushwa na upepo kupelekwa uelekeo wa bandari, taharuki ilitanda na kuna kijana alitaka kuruka majini akadhibitiwa na walonzi na ilichukua kama dk 10 kivuko kuanza upya kwenda mbele hatimaye ikifanikiwa kutia nanga.

Ndani ya hizo dk 10 nililazimika kutoka kwwnye gari na kuanza kusogolea maboya na matukio yote ya kuzama majini yaliyonijia

Maji shikamoo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom