MV Dar es salaam bado haijakabidhiwa serikalini imekabidhiwa vipi jeshini?

evangelical

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
4,897
7,961
Leo asubuhi katika kikao cha maswali na majibu Bungeni Naibu waziri wizara ya mawasliano na uchunguzi Eng Ngonyani alieleza kwamba meli ya mv Dar es salaam bado haijakabidhiwa serikalini baada ya kurudishwa kwa mkandarasi ambaye anairekebisha baada ya kurudishiwa kutokana na mapungufu makubwa iliyokuwa nayo.

Juzi Mhe Rais alitangaza kwamba anaigawa meli hiyo kwa Jeshi.

Sasa mimi nashangaa inakuwaje rais anagawa kitu ambacho bado hakijakabidhiwa rasmi Serikalini baada ya Serikali hiyo hiyo kumrudishia Mtengenezaji.

Inaonekana hii serikali haina mawasiliano au ndio kutaka kufunika kombe mwanaharamu apite
 
Kila sifa zinatakiwa zimuendee yeye mkuu.
Haijalishi wataalam wameelekeza nini.
 
Mkuu hili kabuli lilishazikwa kwa vyuma vizito na concrete grade 1000 unawezaje kuanza kulifukua?? unapata wapi huo ujasiri???
 
Leo asubuhi katika kikao cha maswali na majibu Bungeni Naibu waziri wizara ya mawasliano na uchunguzi Eng Ngonyani alieleza kwamba meli ya mv dar es salaam bado haijakabidhiwa serikalini baada ya kurudishwa kwa mkandarasi ambaye anairekebisha baada ya kurudishiwa kutokana na mapungufu makubwa iliyokuwa nayo.
Juzi Mhe Raisi alitangaza kwamba anaigawa meli hiyo kwa Jeshi.
Sasa mimi nashangaa inakuwaje rais anagawa kitu ambacho bado hakijakabidhiwa rasmi Serikalini baada ya Serikali hiyo hiyo kumrudishia Mtengenezaji.
Inaonekana hii serikali haina mawasiliano au ndio kutaka kufunika kombe mwanaharamu apite
Jeshi letu linakabidhiwa MKWECHE
 
Awamu hii pana vituko vingi sana.... haya mambo yanayofanyika sasa ni utalii tosha....
 
Ukizunguzungumzia MV DSM sasa hivi unazungumzia kifaru cha JWTZ. So tuwe makini maana jamaa ameshawapa kisu.
 
Kwani hujui sasa hivi mchezaji ni yeye kila upande kwa kauli ya kunyoosha? Aliipokea yeye alipokuwa waziri na sasa anaigawa yeye kama raisi, one man show, vitu vingine visubiri kwanza.. ananyoosha.
 
Back
Top Bottom