Mv Bukoba Vs Safari Leo

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Nimehojiana na baadhi ya abiria waliopona katika ajali ya Mv Bukoba na hata wale wa 'Spice Mlenda' iliyozama majuzi kule Zanzibar.

Nani anakumbuka tarehe,mwezi na mwaka wa ajali mbaya ya basi la SafariLeo iliyoua makumi ya abiria wakiwemo maharusi katika eneo la Amujuju nje ya Bk.Naomba hata majina ya manusura na mawasiliano yao kwa anayeweza.
 
Ndiyo kwanza tunaisikia kwako. Wewe unahitaji habari zao uzifanyie nini?
 
mutafute alieimba wimbo wa safari leo na ni zaidi yamiaka 25iliopita kwa nini usitafiti Mv Bukoba VS MELI Iliyozama juzi znz kwanza zinarelate
 
Utafiti wangu pia unahusisha maafa makubwa ya ajali za barabarani.
 
Hiyo ajali ilitokea eneo la Hamgembe na wala siyo Amjuju. Mimi niliijua kupitia wimbo ambao baadaye Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Alhaji Rugusha aliupiga Marufuku kwani ulikuwa unawakwaza wafiwa. Namfahamu mwanajamii forum mmoja ambaye alifiwa na jamaa zake ambao walikuwa maharusi na jamaa wengine wa karibu. Hata hivyo akiona kuna umuhimu wa kuwasiliana nawe atafanya hivyo vinginevyo unaweza kutonesha kidonda chake.
 
Inauma sana. MV bukoba ilizama mwezi wa 9 hii nyingine nayo imezama mwezi huo huo wa 9. Poleni wafiwa manake najua kila mnapozikumbuka hz tarehe mnapata uchungu sana.
 
ktk ajali ya safari leo maharusi hawakufa. isipokuwa gari hilo jana yake lilibeba maharusi hao na kesho yake ndo likapinduka. maharusi walikuwa kwenye fungate. Bi harusi mpaka sasa yu hai na yuko Nzega Tbr. Bw. harusi kafa mwak juzi kwa ugonjwa. No. za simu ya bi harusi zipo ukizitaka sema kwa uatfiti wako.
 
Back
Top Bottom