OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,176
- 103,656
MV Bukoba ilikuwa feri iliyokuwa ikitoa huduma ya kubeba mizigo na abiria katika Ziwa Viktoria kati ya bandari za Bukoba na Mwanza. Tarehe 21 Mei 1996 ilizama kwenye njia ya kuelekea Mwanza. Abiria wengi walikufa na idadi yao imekadiriwa kuwa 1,000 hivi, lakini idadi iliyotangazwa rasmi ilikuwa 894.
Mwaka huo nilikuwa darasa la pili huko kijijini. Time keeper alinituma nikapige kengere Mwalimu Mkuu anataka kuhutubia. Hatukuwa tunajua kuna nini. Mwalimu akatueleza kwa masikitiko makubwa na kuruhusu kurudi nyumbani kuomboleza.