Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,785
Sijawahi kuona wala kusikia Dunia hii watu wakiwa ,,obsessed” na Elimu ya Sekondari kama nchi zetu za English monarchy i.e Kenya, Uganda na TZ, hakuna mahali pengine Dunia hii Shule za Sekondari hushindanishwa na kutoa mshindi utafikiri football, hakuna mahali Dunia hii eti kuna Mwanafunzi bora aliyepata alama za juu kuliko wote, halafu baada ya hapo ni nini kinafwata?
Dunia nzima watu washatoka kwenye Elimu ya Sekondari na wanawekeza Elimunya juu, kutoa Wahandisi, Wanasayansi, Madaktari, Wachumi, Wanasaikolojia, na hata Wanafalsafa, sisi bado tumeganda alipoachoa Muzungu eti tunashindanisha Shule za Sekondari huu ujinga uko Kenya, Uganda na Tanzania tu labda na Afrika nyingine ya English monarchy, Mwanafunzi nchi anatangazwa na vyombo vya habari, baada ya hapo hatujui anaenda wapi na wala hatujamtayarishia chochote huko mbele.
Elimu ya Sekondari inapaswa kuwa nzuri na ni jambo la kawaida hatuhitaji mwanafunzi bora, hata sijawahi kusikia eti kuna Shule ya sekondari bora Duniani bali nasikia University ranking.
Yaani hakuna kitu kipya tunachofanya na wala hatuendi na Dunia, alipoachia Muzungu ni hapo hapo tumeganda na Shule za Sekondari, tunatumia fedha nyingi eti kukarabati Shule kongwe ili iweje?