Muziki Zaidi: Vipi JB Mpiana, Werason, & Koffi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muziki Zaidi: Vipi JB Mpiana, Werason, & Koffi

Discussion in 'Entertainment' started by Field Marshall ES, Apr 10, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wakuu tunaendelea tena vipi hawa nao magwiji wa huko Zaire au Congo-Kinshasa, yaani Suveree Mukulu Jibe, Maison Mere Werason "Step-forward", na Kintonzengu Koffi Olomide vipi nao nani ni bingwa?

  - Nawasilisha.

  FMES!
   
 2. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  FMES, Koffi Olomide ni kiboko yao mkuu. Pub zote hata na bar za uchochoroni Kinshasa, Goma na Lubumbashi, ni nyimbo za huyu papa mukulu kulu. Na katoa album mpya, ni moto usipime
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Mkuu una maana Mukulu Jibe hana bao huko kwa sasa? Duh! Lakini nilimuona miezi michache iliyopita ameondokewa na wapigaji wengi sana yaani imekua aibu tupu, sasa vipi Maison Wera?

  FMES!
   
 4. D

  DawaKali Member

  #4
  Apr 11, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hawa watatu, Werrason ndio mkali.
   
 5. GP

  GP JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  inategemea wakuu kwenye category gani unazungumia!, mfano JB Mpiana kwa rhumba zenye akili, rhumba zilizotulia jamaa ni funika bovu!, werrason yeye ni mkali kwenye sebene sawa na fally ipupa. koffi yeye yuko fit kati ya rhumba na sebene, coz yule ana bendi, JB Mpiana mostly yupo kama solo, although ana bendi, yaani anatoa kazi binafsi na bendi at the same time.
  kuna kitu ya JB Mpiana inaitwa Feux de l'amour, hii rhumba ni hataaaaari, ilikua mega hit enzi zake, still now inakuna kinoma ukiisikiliza.
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  FMES, Papaa Olomide ni mwanzo mwisho. Mukulu Jibe kwa sasa ameshatupwa hata na Fally Ipupa
   
 7. D

  DawaKali Member

  #7
  Apr 11, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Koffi enzi za Tchao Tcho alikua anafunika ulimwengu mzima, siku hizi ana-recycle tu album nyimbo zile zile.
  Siku hizi sisikilizi sana kina JB, Werra au Koffi.
  Ukiachia ma-commercial success kama kina Fally Ipupa, wakali wakweli ni kama kina Ferre Gola, hapo tunaweza kuanza kuongea.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu huyo Ipupa aliwahi kuwa na Jibe kule BCBG au?
   
 9. C

  Chrisant Madubu Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Kwa mtazamo wangu Werason ni zaidi ya JB Mpiana na Kofii Olomide wanachomzidi wao ni majivuno tu
   
 10. D

  DawaKali Member

  #10
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fally Alikua kwenye bendi ya Koffi kabla kuibuka.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu ni kwamba:-

  - Between hawa watatu, Mukulu Jibe ndiye the big talent kuliko Wera na Koffi, lakini tatizo ni tabia za Jibe hazifai, matokeo yake wapigaji wake wamekwua wakimkimbia mara kwa mara na kumfikisha mahali kwamba hata talent yake tena hainga'ri kama zamani.

  - Jibe alipokuwa Wenge Musica, akishirikiana na kina Wera, Bleize Bula, Dominguez, General Qweck, Afande, Robero Atalaku, Philipo, Alain Makaba na hata kutoa ile Album yao ya kwanza ya "Kalai Bwinge", ukweli ni kwamba effort karibu yote ya utungaji wa nyimbo ilikuwa ni yake Jibe na hata walipoachana njia pandaa na Wera kuanzisha bendi yake, Domingues yake, Bleizebula ya kwake, Makaba ya kwake, na General Qweck ya kwake, Jibe alibaki Wenge BCBG na Mkulu Afande, na mambo yalikuwa moto kama kawaida na hasa ile Album ya "Anti-Terror", Wera alichofanya ni kukusanya talents zaidi yake na ikalipa big time na hata sasa kuanza kuwa samba samba na Jibe, lakini na yeye Wera akaanza yale yale ya Jibe wapigaji wakaanza kujiondoa kila siku, wote wakaishia kuwa level moja, sio ya juu sana wala ya chini sana.

  - Lakini as much as I like Jibe, bado kwa sasa naamini kwamba Wera yuko juu kuliko yeye, kwa sababu kitendo cha kutoka kwa Afande, mpaka leo bado hajaweza ku-recover that was a big talent na kwa kweli pamoja na kwamba amejaribu kum-replace na Freddie Kasombo, lakini bado Jibe amekwama, yuko chini chalii! Nilipomuona mara ya mwisho miezi kama miwili iliyopita ilikuwa aibu tupu!

  - Koffi, huyu jamaa huwa simuelewi sana maana kwangu huyu ni mtu wa msimu, mara juu mara chini, lakini one thing ni siwezi kumuweka level moja na Jibe au Werason, wanampita kwa mbali sana, ingawa ndani ya Zaire anaweza kuwa na mashabiki wengi kuliko wenziwe yaani Jibe na Wera.

  Kwa hiyo kwa maoni yangu, Werason Maison Mere, ndiye aliye juu kwa sasa kuliko hawa wote, yaani Jibe na Koffi, kwa sababu hata dau la kuwaalika kupiga ni la Wera ndio kubwa kuliko wengine.

  Respect.


  FMES!
   
 12. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  JB Mpiana na Werrason ni vijana wa kizazi kipya(ish), wote wako fiti sana katika utungaji na upangiliaji wa mambo ila kama kuna mkuu ukurasa wa kwanza alivyodokeza, JB ni mtaalamu wa marhumba ya nguvu. Werra hayupo nyuma sana ila anajua kuajiri marepa "atalaku" wakali, akina Davide, Prince na Celeo Scram (miaka ya nyuma) hivyo masebene yake yanakuwaga si mchezo.

  Koffi ni babu lao, yeye si mtunzi mzuri sana kama JB ila anajua sana kupangilia, kuibua, kujenga na kulea vipaji. Muziki wa Congo siku hizi umepoteza mvuto wake kidogo kwa sababu ala zote ni za umeme na umetawaliwa na waimbaji na marepa tu katika bendi badala ya wanamuziki halisi.
  Wapiga ala kama akina Awilo, Daly Kimoko na Mboka Liya "Burkina Faso" wamekuwa superseeded na wapiga kelele na hata baadhi yao wamekuwa wapiga kelele wenyewe (Awilo).

  For the record, album ya kwanza ya Wenge haikuwa Kalayi Boeing, Bouger Bouger(1988) iliyokuwa na kitu kitamu Kiitwacho Mulolo na kufuatiwa na Kin E Bouge ya 1991 ziliitangulia Kalayi Boeing.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Papaa Koffie Olomide ndo baba lao kwa sasa kuwa music wa kwa Mucongoman ...
   
 14. D

  Dingituka Member

  #14
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  George-Porjie umenikuna kwa kunikumbusha hicho kitu cha JB Mpiana a.k.a bina adam.. Feux de l'amour hiki kitu si mchezo toka nikisikie for the first time wakati ulee i've never stopped loving it, one of the classic rhumbas i've evr heard, it is surely a bomb!! Period! Kinafanana na kibao kimoja matata alikipiga Sam Mangwana Fatimata... weeeh acha mchezo
   
 15. radiation

  radiation Senior Member

  #15
  Aug 27, 2015
  Joined: May 28, 2013
  Messages: 188
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  jB Mpiana yuko vizuri zaidi kuliko Werrason
   
 16. orangutan

  orangutan JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2015
  Joined: Mar 21, 2014
  Messages: 765
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 180
  Ferre Gorra aongezwe kwenye list ya hawa watumbuizaji mahiri. 'diki diki', 'maboko pamba' 'noire eyindaka' ni moto wa kulotea kumbali aisee..
   
Loading...