Muziki wa bongo fleva

Gabraison jr

Member
Sep 7, 2011
21
1
2kiwa kama wadau wa muzik huu wa bongo fleva hebu 2jadili ukuaj wake.wapo wanaosema bongofleva inaelekea shimon na wapo wanaosema inakua ukiwa kama mdau una maon gan?
 
Asante sana kwa swali lako. Kwa mtazamo wangu naona miaka kumi iliyopita imeshuhudia upigwaji wa hatua kubwa sana kwenye muziki wa bongo fleva. Kuongezeka kwa studio, malipo ya album kuboreka, club nyingi kupiga bongo fleva, wanasiasa kutumia wanamuziki, wanamuziki kupata shows nje ya nchi ni baadhi ya hatua ambazo haziwezi kubezwa. Hata hivyo tasnia ya muziki kwa ujumla bado haijapewa umuhimu sana na serikali. Serikali imeshindwa kabisa kuwasaidia wanamuziki kutokana na kudhulumiwa mapato au kupewa mapato kiduchu na wenye dhamana ya kuuza kazi zao. Nadhani tatizo hili likipata utatuzi tutarajie kuona wanamuziki wa bongofleva nao wakiishi kama wenzao wa Uganda ambako kuna mfumo mzuri wa mauzo ya kazi za wasanii.
 
poa lakini studio nyingi ambazo zpo ni uchwara
 
Binafsi naamini Bongo fleva itabaki hapo ilipo kwa ufinyu wake wa bongo fleva.
Watangazaji Bongo fleva.
DJ Bongo fleva.
Mtayarishaji Bongo fleva.
Meneja Bongo fleva.
Msambazaji Bongo fleva.
Msanii Bongo fleva.
Kadhalika.... Nk...nk..!!

Wamebaki kuiga tu midundo ambayo wenzao imewachukua miaka dahari kuitangaza kwa taabu na ustahimilivu mkubwa, mfano Kwaito, Kwela, Zouk, Rhumba nk..! Ukisikiliza msanii wa Bongo fleva anahojiwa na mtangazaji wa Kibongo fleva ndo utajua namaanisha nini. Kwa yeyote ambaye ni mfuatiliaji mzuri wa muziki na mahadhi mbalimbali atakubaliana nami kuwa kuipenda Bongo flava ni lazima uwe mchache wa ufahamu ktk muziki kwa upana wake. Vinginevyo utabakia kuvutiwa na msani mmoja mmoja kwa aina ya Sauti, muonekano au zaidi vituko vyake (hii imo ktk muziki) si kuipenda Bongo fleva.
Pia wengi wao ni wepesi mno! hawana ujazo wa haja ktk ufahamu wa mambo mbalimbali yanayowazunguka ktk maisha ya kila siku na miongoni mwa jamii inayowazunguka. Mfano si ajabu kukuta msanii hajui historia au asili hata ya kabila lake sembuse taifa.
Binafsi naamini Sanaa inategemea zaidi fikra na uelewa wa msanii husika ktk mambo mbalimbali ktk fani yake na hasa yale yaliyo nje ya fani yake na ufahamu huo ndiyo huzaa sanaa kwa upana wake. Na ktk muziki ufahamu wa mambo ndicho kitufe cha umahiri na ufanisi hatimaye mafanikio huja hima bila simile wala hiyana.
Ni mtazamo binafsi wakuu!
 
mi sielewi au vp inamaana bongo fleva ndo mziki w etu sisi watanzania kama vile congo na bolingo, afrika kusini na kwaito au tumeamua kuwekana ujinga tu vichwan mwetu
 
unakufa kwa kasi ya taratibu sana,.mi nataka ufe kwa kasi ya kimbunga ili tuwe na mziki wetu utakaolitambulisha taifa...bongo flavor ni rap ya kimarekani kwa kiswahili period...halafu wanamziki wengi wa hiyo bongo flavor hawana hata ufahamu wa hiphop,..misingi yake hawaijui
kuna mwanamziki mmoja(mpumbavu)aliwahi kughani with his whack style eti hiphop ni uhuni..ice t angemsikia mpuuzi kama huyu angemshoot like a dog...
mapenzi mengi meseji za ukombozi chache na zisizo na maana
let it die for f***in good
iam out
 
Asante sana kwa swali lako. Kwa mtazamo wangu naona miaka kumi iliyopita imeshuhudia upigwaji wa hatua kubwa sana kwenye muziki wa bongo fleva. Kuongezeka kwa studio, malipo ya album kuboreka, club nyingi kupiga bongo fleva, wanasiasa kutumia wanamuziki, wanamuziki kupata shows nje ya nchi ni baadhi ya hatua ambazo haziwezi kubezwa. Hata hivyo tasnia ya muziki kwa ujumla bado haijapewa umuhimu sana na serikali. Serikali imeshindwa kabisa kuwasaidia wanamuziki kutokana na kudhulumiwa mapato au kupewa mapato kiduchu na wenye dhamana ya kuuza kazi zao. Nadhani tatizo hili likipata utatuzi tutarajie kuona wanamuziki wa bongofleva nao wakiishi kama wenzao wa Uganda ambako kuna mfumo mzuri wa mauzo ya kazi za wasanii.

sorry nafikiri nimepotea hapa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom