Muziki ni kazi ya kustaafu mapema, wasanii kuweni makini

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
9,767
21,338
MUZIKI NI KAZI YA KUSTAAFU MAPEMA, WASANII KUWENI MAKINI.

Mwaka 1992 kundi la muziki la Boyz II Men toka Philadelphia, USA waliachia wimbo wao, End of the road, ulioshika namba moja kwa wiki 13 kwenye chati za Billboard. Wakati kumbukumbu za huo wimbo hazijaisha kundi hilo kwa mara nyingine mwaka 1994 wakavunja rekodi yao Billboard kwa kuingiza wimbo, I'll make love to you, uliokaa namba moja kwa wiki 14. Ila wakaishangaza dunia kwa kuingiza wimbo mwingine, on bended knee, hapohapo namba moja baada ya hizo wiki 14. Ni kitu ambacho kabla ya hapo kilikuwa kimefanywa na Elvis Presley na kundi na Beatles. Mwaka uliofuatia 1995 kwa mara nyingine Boyz II Men wakavunja rekodi yao kwenye chati za Billboard kwa kuingiza namba moja kwa wiki 16 wimbo wao mwingine, One sweet day, waliomshirikisha Mariah Carey.

Kuanzia mwaka 1997 ndo matatizo yalipoanza kutokea ndani na nje ya kundi la Boyz II Men.. Kukawa na kupanda na kushuka kwa kundi hili. Ingawa waliendelea kutoa mawe makali kama vile 4 seasons of loneliness, a song for mama, color of love, na kadhalika. Kufikia mwaka 2001 kundi lilijitoa chini ya usimamizi wa Universal Music Group. Hii ndo kampuni iliyowatambulisha na kuwafanya wawe mastaa wa dunia. Mwaka 2002 kundi likaingia mkataba na kampuni ya Arista. Lakini bado haikuwezekana hadi leo kurudi kwenye ufalme wao wa mwanzo wa miaka ya 90. Kundi bado lipo na linajitahidi kutoa kazi ikiwamo kufanya tour kabla ya corona, pia wanajihusisha na TV shows.

Mimi nilichojifunza kwenye stori ya hili kundi ni kwamba kazi ya muziki sio ya kudumu, ina kustaafu tena mapema tu. Wateja wa kazi za muziki hununua bidhaa kulingana na mahitaji ya wakati huo. Kwahiyo msanii kustaafishwa haipingiki kwa jinsi atakavyokuwa mzembe kwenda na hitaji la wakati huo. Miaka ya mwanzoni mwa 2000 kulikuwa hakuna cha 50cent wala kina Chris Brown. Wafalme walikuwa kina Sisqo (unleash the dragon), R Kelly, na kina Aaliyah. Ila saa hii Sisqo yupo na imekuwa ngumu kurudi mainstream.

Nidhamu na maelewano pia ni jambo la muhimu sana kwa msanii ili aweze kudumu. Kuwavimbia waliokuinua ni sababu kubwa mno ya kustaafishwa mapema. Tukiangalia hitsongs karibu zote za Boyz II Men kuna uhusika wa mtu aitwaye Babyface. Ila baada ya kutengana nae walikaa miaka kadhaa bila kurudi kwenye peak. Mwaka 2002 ndo Babyface akashiriki tena kwenye wimbo COLOR OF LOVE na majamaa wakarudi tena kwenye ubora. Mwaka 2007 baada ya kuachana na UMG walirudi tena kundini na kusaini mkataba mpya na UMG baada ya kutengana mwaka 2001. Kimsingi msanii kubali kabisa kuna watu lazima wale ili na wewe ule. Kwa mfano mtu kama Diamond kuendelea kufanya kazi na kina Tale ni sababu kubwa ya yeye kuendelea kubaki juu.

Kingine pia ili msanii azidi kuwa vinywani mwa watu huku akipiga hela ni kuwekeza kwenye mambo mengine yanayohusiana na yasiyohusiana na muziki. Kina Dre, Didy, Master P, na wengine wa kariba hiyo hawajawahi kuwa wasanii bora sana ila ndo mabilionea wakubwa kwasababu ya kufanya biashara mbalimbali. Hata hapa nchini tuna AY na MwanaFA ambao wao ni kama Kagera Sugar kwamba hawajawahi chukua ubingwa wala kushuka daraja kwasababu ya kujichanganya pia kwenye mambo mengine ya kuwaingizia kipato.

Mwisho niseme wanamuziki fanyeni kazi sana ili mpate mafanikio. Acheni mambo ya kipuuzi mnayoita kiki ili mjulikane. Toeni kazi nzuri. Mwaka 2003, Koffi Olomide alishinda tuzo nne za Kora kwa mara moja kupitia albamu yake ya Efrakatta. Ila nyuma ya pazia ile albamu ilikuwa na CD1 na CD2, yaani ni kama albamu 2 ndani ya moja. Jamaa alifanya kazi kubwa mno. Hakukuwa na kiki wala nini.
 
Umesema ukweli mtupu,msanii akijisahau anaishia kuwa katika hali mbaya sana,mifano ya wasanii wetu waliostaafishwa wamejitahidi kujitutumua lakini wapi,mziki umeshawapa mkono wa kwaheri.
 
Mfano mzuri msanii CAZ T mwana wa komba baada ya kupiga pesa za ablam ya nakuitaji uyo kaingia kwenye mambo mengine

Ona leo juma nature, inspector harun nk wanalazimisha kutuimbia wakati mitindo yao ni old school na siye old school tushaacha sikiliza miziki mda wote

Ujumbe huu umfikie prof Jay bro kama za kinua mgongo bado zipo mfute mista ticha marekani mkabebe box huu mziki soon unakudharirisha
 
MUZIKI NI KAZI YA KUSTAAFU MAPEMA, WASANII KUWENI MAKINI.

Mwaka 1992 kundi la muziki la Boyz II Men toka Philadelphia, USA waliachia wimbo wao, End of the road, ulioshika namba moja kwa wiki 13 kwenye chati za Billboard...
Umechanganya files sijui hata unataka kuzungumzia nini?

Wasaniii kuwekeza?

Wasanii kutowavimbia waliowatoa kimuziki? Na ulipomtaja Babu Tale ndio umepoteza maana, huyo Babu Tale tangu aanze kusimamia wasanii, kamsimamia huyo Diamond peke yake?

Wengine waliokuwa chini ya babu tale mafanikio yao yako yapi?

Umewataja AY na FA na wao walikuwa chini ya babu tale?

In short kama unaongelea mafanikio ya muziki kwa maana hits, mada iwe moja maana,

Hata watu wakiajiriwa pamoja na misharaha wakawawanapokea inafanana, mwisho wa siku maendeleo yao hayawezi kufanana.
 
Umechanganya files sijui hata unataka kuzungumzia nini?

Wasaniii kuwekeza?

Wasanii kutowavimbia waliowatoa kimuziki ?
Na ulipomtaja Babu Tale ndio umepoteza maana, huyo Babu Tale tangu aanze kusimamia wasanii, kamsimamia huyo Diamond peke yake ?

Wengine waliokuwa chini ya babu tale mafanikio yao yako yapi ?

Umewataja AY na FA na wao walikuwa chini ya babu tale ?

In short kama unaongelea mafanikio ya muziki kwa maana hits, mada iwe moja maana,

Hata watu wakiajiriwa pamoja na misharaha wakawawanapokea inafanana, mwisho wa siku maendeleo yao hayawezi kufanana.
Wewe pia hujakatazwa kuandika. Na sijaandika ili kukidhi matakwa yako.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom