Muziki na Siasa ya Wasafi Tour 2020. Eti Wamesahau

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,009
2,000
Ninapokumbuka muziki na siasa namkumbuka msanii aliyevuma sana nchini , wakati huo hapakuwa na Diamond wala nani , huyu ni MARLAW alikuwa na kipaji sana na kuelekea kampeni za urais 2010 nyimbo zake zilikuwa HITS kwenye radio top ten zote
Mwaka 2010 alipata deal la kampeni akazunguka nchi nzima akiimba nyimbo zake HIT kwa kubadilisha na kuweka maneno ya kisiasa

Alipata pesa nyingi na kampeni zikaisha , kufikia mwaka 2011 mambo yalikuwa ni tofauti kwani hakuna mtu aliyetaka kusikiliza nyimbo zake wala show zake taratibu alipotea kwenye ramani ya muziki na kubakia zilipendwa. Bahati mbaya waliomtuma hawajamkumbuka kwani hata kampeni zilizofuatia za 2015 na sasa 2020 hakuna aliyekumbuka kumpa deal MARLAW

Tunayo tasnia yetu ya Bongo Movie ambayo kati ya mwaka 2005 hadi 2015 ilikuwa kwa kasi ,tatizo likaanza mwaka 2015 pale Bongo movie walipoanza kutumika kisiasa ..walipata deal kubwa sana na wakadhulumiana pesa ..kampeni ziliisha na wengi bongo movie wana miaka sita hawajatoa movie hata moja ...wanaishi kwa kuuzana , kupiga mizinga , kula pesa za rambi rambi na kusubiri kampeni ....leo tasinia ya filamu imefika sehemu mbaya kabisa ..hakuna maendeleo yoyote ..wakati ilikuwa inakuwa kwa kasi na walifikia hadi kupewa maeneo ya viwanja kwa ajili ya maendeleo yao.

Tunapoangalia haya basi ni vigumu kuacha kumuangalia DIAMOND na wasafi yake anayoimiliki kwa ubia na wafanyabishara wengine .., imegeuka kituo cha propaganda na yeye mwenyewe kageuka "capt john komba " tunatambua kuwa kalipwa vizuri na moja ya deal ni kukubaliwa kufungua vituo vya radio mikoani kwa kasi ya moto ..kwani ndani ya kampeni za mwaka huu pekee kafungua mikoa minne ndani ya siku 60 ikiwamo Mwanza , Mbeya na Arusha. Hii sio kawaida wakati vituo vingi tu vyenye uwezo maombi yao ya kufungua kwenye mikoa mingine yamekaliwa kwa miaka sasa yeye ndani ya miezi miwili kafungua vituo kama uyoga ili vitumike kwenye propaganda

Naona Kampeni zimeisha na anatangaza tena kuanza ziara nchi nzima ya "FIESTA" Wenyewe wanaita WASAFI TOUR ...Tofauti na ziara hii na ile ya kampeni ni kuwa wakati kwenye kampeni aliimba bure hii sasa atalipisha kiingilio....

MABIBI NA MABWANA KARIBUNI KWENYE WASAFI TOUR 2020

MUZIKI NA SIASA !!!
 

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
10,480
2,000
Mtoa post nimekuelewa sana.Imeandikwa "Hakuna jipya chini ya jua", Kwa hiyo ni suala la muda tu. Wahenga wetu wakatuonya wakisema " Hakuna marefu yasiyo na ncha" na "Mbio za sakafuni huishia ukingoni";Wengine wakasema " Ivumayo haidumu",si hivyo tu wako waliosema "Ngoma ikivuma sana,mwisho wake hupasuka". Ni suala la muda.
 
Oct 26, 2019
74
125
Ulicho fanya ni personal attack hujaonyesha analysis ni kwanini MARLOW ali drop kimziki na pia ni kwanini Tasinia ya BONGO MOVE imedrop? Unapo husisha wasanii na siasa ni kivipi wanadrop kwenye gemu ni kwanini? Hilo ujaliweka wazi.

Jaribu kuangalia mizizi ya Marlow kimziki kabla ya mwaka 2010 je alikuwa na tuzo ngapi? Ndani na nje ya Tanzania na pia uwekezaji wake kimziki ulikuwa wa level gani huku ukimlinganisha na DIAMOND PLATNUM mizizi yake kwenye mziki imedeep kiasi gani uwekezaji wake kwenye mziki ni wakiwango gani na pia amepokea tuzo ngapi?

Leo hii una mshambilia DIAMOND kisa alikuwa kwenye campaign za 2020. Mbona mwaka 2015 alizunguka nchi nzima na nyimbo zake zimetumika sana mwaka 2015 lakini toka hiyo miaka hadi leo anaendelea kuzoa tuzo kama anaokota maembe hajachuja na bado ni moja ya watu wenye mvuto zaidi Tanzania na afrika kwa ujumla.

Kama hujui katika siasa, kuna techniques nyingi sana ili kufanya mvuto wa chama cha siasa au mwanasiasa awe na mvuto ndani ya jamii yake kuna kitu kinaitwa PROPAGANDA by wagon hii ni mbinu inayo tumia watu maharufu kama ni upande wa siasa wanatumiwa na chama au mwanasiasa kumnadi au kunadi chama lengo ni hiule mvuto wa huyo mtu maharufu kuwavuta wafuasi wake waunge chama au wamuunge mwanasiasa anaye mnadi.

Pia hii propaganda inatumika kwenye bidhaa na makampuni mbali mbali kunadi biashara yao kwa kutumia hawa watu maharufu ndio maana diamond utamkuta kwenye mabango mbali mbali ya biashara au matangazo.

Hivyo CCM ilicheza na akiri za watu unapo sikia wanatumia sayansi katika campeni hii ni sayansi moja wapo (sayansi ya jamii) ya kuwatumia wasanii ni mbinu moja wapo iliyo fanya watu wavutike kuja kwenye mikutano.

Siasa siyo chanzo cha anguko la msanii kwa msanii anaye jitambua na ambaye anatazama miaka mitano ijayo hiyo ndio furusa ya kuitumia ili kudeep mizizi ya kazi yake na kudeep uwekezaji wake kwa mgongo wa siasa.
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,009
2,000
CCM wanashindwa kumsadia MR NICE naye walimtumia sana wanabaki kusema diamond anafanya vizuri how about others
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,407
2,000
Uzi wa hovyo Sana huu, Diamond yupo kwenye Kampeni since 2010 , mbona hajadrop? Ni mwehu Tu anayeweza Amin Lissu alishinda kwenye uchaguz mwaka huu..... Kura feki uliziona, ?? Zilete peleka mahakamani kama ushahidi
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,582
2,000
Ulicho fanya ni personal attack hujaonyesha analysis ni kwanini MARLOW ali drop kimziki na pia ni kwanini Tasinia ya BONGO MOVE imedrop ?
unapo husisha wasanii na siasa ni kivipi wanadrop kwenye gemu ni kwanini? Hilo ujaliweka wazi...

Atakuwa na personal issues na diamond.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom