Muwe serious, hivi unatoa sadaka Tsh 2000 kweli?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,014
Majitu majinga na yanazidi kuwa majinga kila siku. Na ka elfu mbili kako ka mawazo ulikotoa then unategemea ubarikiwe?

Kama ni muajiriwa unalipwa kuanzia laki 4 basi sadaka ni angalau 10000 na zaka 40000 kila mwezi. Jumla ni 50000 tu.

Watu ndiyo maana ni masikini. Mimi najua kabisa unalipwa 5M then mwisho wa mwezi sioni zaka aisee nakupigia simu utume changu mapema mno.

Jifunzeni kutoa acheni uchoyo... hata nikinunua range na wewe si unabarikiwa? Unapata furaha gani baba yako wa kiroho anatembelea IST au Harrier tako la nyani? Fanya mitikasi ukiweza apate range kali.

Watanzania tuache roho za kichoyo shenzi kabisa
 
Marko 12:41-44​

41 Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha.

42 Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.

43 Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote!

44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”
 
Majitu majinga na yanazidi kuwa majinga kila siku. Na ka elfu mbili kako ka mawazo ulikotoa then unategemea ubalikiwe?

Kama ni muajiriwa unalipwa kuanzia laki 4 basi sadaka ni angalau 10000 na zaka 40000 kila mwezi. Jumla ni 50000 tu.

Watu ndiyo maana ni masikini. Mimi najua kabisa unalipwa 5M then mwisho wa mwezi sioni zaka aisee nakupigia simu utume changu mapema mno.

Jifunzeni kutoa acheni uchoyo... hata nikinunua range na wewe si unabarikiwa? Unapata furaha gani baba yako wa kiroho anatembelea IST au Harrier tako la nyani? Fanya mitikasi ukiweza apate range kali.

WaTZ tuache roho za kichoyo shenzi kabisa
hiyo 2000 ni kubwa mno, watu wanatoa 200 na siku zinaenda. Japo sarafu siku hizi hazitakiwi zinapunguza mapato. Ifike wakati na nyie wachungaji muone aibu kuwa na washirika masikini huku nyie mkiishi maisha ya kifahari na anasa
 
Wachungaji wa siku hizi wamepotoka, unakuta wao ndio wana maisha bora kuliko kodoo zao. Wamejenga majumba mazuri, wana magari ya bei kubwa, wanasomesha watoto wao shule nzuri, wana miradi mikubwa ya kuwaingizia fedha lakini hawana huruma na kondoo zao. Wanawakamua mpaka shilingi ya mwisho. Tena hiyo ni mbali na sadaka ya kawaida. Mara mchungajia anaibuka katikati ya ibada anaanza kukusanya michango ya ghafla akisema mwenye laki, mwenye elfu hamsini, mwenye thelathini, ishirini, kumi, elfu tano, mbili, mwenye elfu moja, mia tano mwenye mia mbili, mwenye hela yoyote alete mbele. Yaani ni vituko vitupu. Ipo siku watajikuta wenyewe ibadani kwa kuchosha waumini kwa michango isiyo na kichwa na miguu. Bado kuna michango mingine ya ujenzi, miradi na changizo. Siku hizi ukitaka kwenda ibadaei lazima mifuko itune kwa hela la sivyo utaombwa michango na huna utaishia kuabika huku umevaa suti kali na tai na utaonekana si mtoaji na una dhambi
 
Majitu majinga na yanazidi kuwa majinga kila siku. Na ka elfu mbili kako ka mawazo ulikotoa then unategemea ubalikiwe?

Kama ni muajiriwa unalipwa kuanzia laki 4 basi sadaka ni angalau 10000 na zaka 40000 kila mwezi. Jumla ni 50000 tu.

Watu ndiyo maana ni masikini. Mimi najua kabisa unalipwa 5M then mwisho wa mwezi sioni zaka aisee nakupigia simu utume changu mapema mno.

Jifunzeni kutoa acheni uchoyo... hata nikinunua range na wewe si unabarikiwa? Unapata furaha gani baba yako wa kiroho anatembelea IST au Harrier tako la nyani? Fanya mitikasi ukiweza apate range kali.

WaTZ tuache roho za kichoyo shenzi kabisa
Sadaka na zaka ni WIZI. Mungu mwenye utajiri kwa nini tena umtolee sadaka?

Yani umtolee Mungu hela halafu umuombe tena upate pesa?
 
Yani na bado nchi inafunguka. Utaanza kupokea sadaka jero jero bora hata hio buku 2 unayotaka sahivi
 
hiyo 2000 ni kubwa mno, watu wanatoa 200 na siku zinaenda. Japo sarafu siku hizi hazitakiwi zinapunguza mapato. Ifike wakati na nyie wachungaji muone aibu kuwa na washirika masikini huku nyie mkiishi maisha ya kifahari na anasa
Na wame kuja na mbinu ya kuweka vitu vya chuma uki dondosha jero kila mtu ana sikia jamaa kaweka jero uhuni mwingi
 
Majitu majinga na yanazidi kuwa majinga kila siku. Na ka elfu mbili kako ka mawazo ulikotoa then unategemea ubarikiwe?...
Ni heri nikatoe sadaka yangu direct kwa Yatima na Maskini ninaokutana nao barabarani kuliko kutoa kwenye taasisi zinazoitwa Makanisa. Huko sadaka yangu haifanyi lolote zaidi ya kutumiwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.
 
Majitu majinga na yanazidi kuwa majinga kila siku. Na ka elfu mbili kako ka mawazo ulikotoa then unategemea ubalikiwe...
Sadaka tunawapa kuku na vikolombwezo tunawapa, na bado mnawala waimba kwaya wenye makalio marefu( kondoo walonona).

Jamani viongozi wa dini hamliziki 🤔🤔
 
Back
Top Bottom