Muwe makini na Wahitimu wa vyuo hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muwe makini na Wahitimu wa vyuo hivi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kamongo, Jul 13, 2009.

 1. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Napenda kuwajulisha watanzania wenzangu kwamba tuwe makini na wahitimu wa University Computing Centre-Mwanza Branch na Instititute of Accountancy Arusha kwani kwenye vyuo hivi viwili kuna watu wengi wanajiunga wakitumia vyeti feki au vyeti vya ndugu zao,na ushaidi tunao tunaomba uongozi wa vyuo hivi wawe makini wanapofanya selection
   
 2. Mau

  Mau Senior Member

  #2
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mzee ninachoamini ni kwamba mtu anapoingia chuo kwa cheti cha mwenzake ikiwa yeye hana uwezo basi lazima ataumbuka hapo katikati. mtu huyu akiweza kumaliza na kuifanyia kazi inavyotakiwa profession aliyoisomea bila malalamiko ya watu wanaomzunguka basi hatuna budi kuitumia taaluma ya huyu mtu ili kuliendeleza taifa letu.
  Hayo uliyoyaandika hapo juu me nayaona kama majungu tuu pia inaonyesha ni jinsi gani shule yako ina utata au mlipeleka vyeti feki wengi chakwako kikashtukiwa wengine wakaingia sasa ndo unataka kuchafua majina ya vyuo.

  Kaka kwanza unatakiwa kuelewa enrolment ya vyuo vya elimu ya juu sio kama ya chekechea baada ya kuchaguliwa na chuo husika kuna taasisi nyingine maalum inayopitia tena majina na uwezo wa kielimu walionao wahusika (TCU)

  acha mboke kaka fanya kazi utaingiliwa na umasikini
   
 3. K

  KiboGold New Member

  #3
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swala la vyeti feki ni kosa la jinai, kama wamjua alipata usajili kwa mtindo huo ni vema kumripoti panapohusika badala ya kuharibia wale wanaliosoma na wanaoendelea kusoma katika vyuo hivi. Hapa ni case by case, samaki mmoja akioza haiwezi kufanya kazi katika mazingira kama haya. Wote tunawajibika kupambana na hawa wapenda dezo wanaofanya mchezo huu mchafu kwa gharama yeyote.
   
 4. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Kumbe pia admissions za Institute of Accountancy Arusha zinapitiwa na TCU!
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
   
 6. b

  bnhai JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Ni NACTE kaka bwana Mau nadhani hana uzoefu na vyuo vyetu
   
 7. Robweme

  Robweme Senior Member

  #7
  Jul 13, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mnamatatizo sana, mimi nadhani serkali imeweka watu kwa kuwaamini ambao wanaangalia na kukagua vyeti vya wanafunzi kabla hawajajiunga chuo chochote.Sasa leo utasemaje kuwa huwaamini watu hao,waliopewa hiyo kazi.
  Acheni majungu fanyeni kazi ongezeni kipato, waachie waliopewa hiyo kazi ya kukagua vyeti wafanye kazi yao.Why watanzania hatuaminiani kwenye kazi?.Mwenzako kapewa kazi ya kukagua vyeti na serikali leo unasema humwamini ni vipi.Piga kazi songa mbele, waza maisha yako yakoje tangia umemaliza shule unamafanikio, au unatumika tuuu.Na kama unatumika tu, hamna mafanikio tafuta kazi pengine, kama alivyosema mchangiaji mmoja,ukifoji vyeti hutafika mbali, utaishia njiani.
  "Acheni wafanye kazi yao na tuwaamini bwana"
   
 8. b

  bnhai JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Waache watu wahoji unaogopa kivuli chako nini? Wanasiasa kuhojiwa sawa, wengine je? kama utendaji ni mbovu lazima vidole vinyooshwe
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwanza naomba heading ya post hii ibadilishwe. Angalau isomeke kukithiri kwa vyeti bandia kwenye vyuo vifuatavyo
  Pili, Jamani tusifurahie hii post bila ya kuwa na ushahidi wa haya anayoyasema mwenzetu, huyu jamaa anaweza kuharibia watu wote waliosoma pale bila kujali wana vyeti feki au la. Namuomba kwa heshima na taadhima muweka mada aweke kwanza ushahidi ndio watu wakae waanze kukiponda chuo na products yake.

  Mtoa mada akumbuke kuwa hata UDSM, MZUMBE, TUMAINI, SAUT na kwingineko kuna vyeti feki vingi sana lakini sio sahihi kusema kuwa msiwamini wahitimu wa vyuo husika, uko ni kuwanyima wengine soko hata wasiohusika.
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Good Comment!!! Huu ni uchafuzi wa sifa za vyuo na kuharibu nafasi za kazi kwa Watanzania wenzetu!!! Huyu sijui Mmbuga wa wapi??? Atoe vielelezo basi amekaa kimya kama aliyefumaniwa na mke wa mtu
   
 11. c

  chuku Member

  #11
  Jul 16, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha umbea wa kuharibu majina ya hivyo vyuo,ninawasisi na wewe kwamba la inawezekana ulisoma kwa cheti cha kufoji,acha watu wasome wa kikamatwa wewe hauta kuwepo,pilipili usiyo ila omba kazi PCB,
   
 12. Zilla The G

  Zilla The G JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2017
  Joined: Dec 26, 2014
  Messages: 477
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  kumekucha!!
   
Loading...