Muwaza wataka kesi ya wapinga Muungano ifutwe

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Posted on April 26, 2012 by zanzibaryetu
Wananchi wakiwa katika mhadhara ulioandaliwa na taasisi za kiislamu katika harakati za kuhamasisha wananchi watoe maoni yao juu ya kuutaka au kuukataa Muungano jambo ambalo linapigwa na serikali na kutakiwa wasubiri kutoa maoni yao katika tume iliyoundwa na Rais Kikwete

JUMUIYA YA WAZANZIBAR (MUWAZA) inasikitishwa zaidi kuona kuna baadhi ya Viongozi wetu wa juu katika Serikali wakitowa kauli za vitisho kwa Viongozi wa dini na vikundi mbali mbali vinavyo vinawaelimisha Wananchi udhalimu wa huo unaoitwa eti Muungano ambayo ni haki yao kufanya hivyo maana huo unaoitwa Muungano haukutoka mbiguni kwa Mwenyezi Mungu ila umeanzishwa kwa mabavu na watu wawili waliojifungia kwa siri bila ya ridhaa ya Wananchi wa pande mbili ya ilokuwa Tanganyika na Zanzibar ambao tokea awali umeonesha kuwa hauna nia njema wala maslahi ya Wananchi ila una maslahi kwa Viongozi wachache waliopo madarakani.
YAH: UDHALILISHAJI WANAOFANYIWA WANANCHI KWA KISINGIZIO CHA KUULINDA MUUNGANO
Kwa heshima tafadhali husika na mada ya hapo juu.
Itakumbukwa hivi karibuni kumeanzishwa Tume ya kuratibu maoni juu ya katiba mpya ambayo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano ambayo inatarajiwa kufanya kazi zake wakati wowote kuanzia sasa. Kwa upande wa Zanzibar, wapo Wananchi wengi ambao wanaonelea kuwa kwanza ifanyike kura ya maoni kwa kuulizwa kama wanautaka au hawautaki huo unaoitwa eti Muungano na ikiwa kama watakubaliana na hilo ndio ufanyike huo mchakato wa kukusanya maoni juu ya katiba mpya.
Hakuna asiyejuwa ukiwemo na wewe kuwa huo unaoitwa Muungano umeanzishwa kimabavu na Madikteta wawili ambao ni Karume na Nyerere bila ya ridhaa za Wananchi wa pande mbili yaani ilokuwa Tanganyika na Zanzibar na kusababisha kuipora Zanzibar kila kilicho chake kutoka Uraia, Uchumi, Siasa … n.k.
Hivi karibuni tumeshuhudia udhalilishaji mkubwa unaofanywa ma Jeshi la Polisi kwa vikundi mbali mbali ambavyo vimeonesha hisia zao za kupinga UKOLONI WA KITANGANYIKA katika ardhi za Zanzibar kwa kisingizio cha kuwa eti wanaupinga huo unaoitwa Muungano.
MUWAZA inasikitishwa zaidi kuona kuna baadhi ya Viongozi wetu wa juu katika Serikali wakitowa kauli za vitisho kwa Viongozi wa dini na vikundi mbali mbali vinavyo vinawaelimisha Wananchi udhalimu wa huo unaoitwa eti Muungano ambayo ni haki yao kufanya hivyo maana huo unaoitwa Muungano haukutoka mbiguni kwa Mwenyezi Mungu ila umeanzishwa kwa mabavu na watu wawili waliojifungia kwa siri bila ya ridhaa ya Wananchi wa pande mbili ya Tanganyika na Zanzibar ambao tokea awali umeonesha kuwa hauna nia njema wala maslahi ya Wananchi ila una maslahi kwa Viongozi wachache waliopo madarakani.
Kutokana na hayo, Jumuiya ya MUWAZA inakuomba kuliingilia kati suala hili haraka kwa kuwaadhibu Viongozi wako wanaotowa kauli za vitisho kwa Wananchi wa Zanzibar ili tusiweze kuridishwa huko tulikotoka ambapo hatupataki kurudi. Pia, MUWAZA inakuomba kuwa Wananchi wote waliokamatwa kwenye Viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuonesha hisia zao juu ya huo Muungano wafutiwe kesi zao mara moja kwani tunaamini walilolifanya ni haki yao ya kupinga kitu ambacho kinawadhalilisha kwa miaka mingi.
MUWAZA inatarajia barua hii utaipa mashirikiano makubwa
Tunakutakia kila la kheri
KATIBU
Jumuiya ya MUWAZA
UK
Nakala: Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – UK
Balozi wa Kenya – UK
Balozi wa Rwanda – UK
Balozi wa Uganda – UK
 
Sasa mimi nashindwa kukuelewa,yaani hii barua,sijui ni habari. Imeandikwa katika mfumo ambao tayari jibu unalohitaji linaonekana.
Jumuiya inataka watu waruhusiwe kutoa maoni yao na wakati huo huo unakuja na majibu ya kujionyesha kabisa kuwa nyie kama jumuiya hamtaki muungano. Na kuonyesha hali ya kukosa busara unawaita Nyerere na Karume ni madiktekta. Mimi sina nia ya kuutetea muungano au kuwatetea Nyerere na Karume. Ila njia ambayo mnaitumia sidhani kama ni sahihi.
 
TISS utawajua tu huwa wako tofauti kabisa na mandhari husika.

attachment.php
 
Back
Top Bottom