MUWASA wafanya maajabu, wazungu watua Moshi kuja kushangaa

Katika hali isiyo ya kawaida lakini sio kawaida zaidi kwa nchi ya Kiafrika kufanya hivyo, mamlaka ya maji safi na maji taka mji wa Moshi (MUWAS) imeamua kuzima mtambo wake mmoja baada ya kuzalisha maji ya ziada kwa asilimia 270%.
Hali hiyo ilizishitua mamlaka nyingi za maji duniani ambapo mamlaka zinazohusika na maji Cape Town na California ,ambazo kwa kiasi kikubwa zimekumbwa na uhaba wa maji walifunga safari hadi Moshi kuja kujifunza ni hasa watu hawa wamewezaje.

Bila hiana MUWSA iliwapa elimu muhimu ya kuweza zalisha maji ya ziada katika maeneo yao ambapo walisema siri kubwa ni utanzaji wa vyanzo vya maji pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanya na serikali katika mitambo na miundombinu mingine.
Mamlaka nyingine mbili nazo kuzima mitambo kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Mkuu utakua unaongelea moshi bar ya huko kwa bashite,moshi inashida ya maji sana japo mito ni mingi ila muwasa hawana jipya wapo tu kusubiri mishahara,ukienda pasua,rau,majengo,soweto maji ya shida yanatoka mara moja au mbili kwa wiki.
Muwasa hawana plan wangekua na plan maji yangefika mpka majengo
 
Moshi kuna mengi sana ya kujifunza
1) ufugaji ( intensive husbandry )ngombe watatu tu wamaziwa mtu anajenga na kusomesha watoto private school
2) usafi wa mazingira
3)maji kwa jamii
4)demokrasia
5) utunzaji wa mazingira
6) matumizi ya muda
7)kujituma hasa kiuchumi
NB tuache tuki na hawa watu !!! Njooni mjifunze kuna mengi
 
Katika hali isiyo ya kawaida lakini sio kawaida zaidi kwa nchi ya Kiafrika kufanya hivyo, mamlaka ya maji safi na maji taka mji wa Moshi (MUWAS) imeamua kuzima mtambo wake mmoja baada ya kuzalisha maji ya ziada kwa asilimia 270%.
Hali hiyo ilizishitua mamlaka nyingi za maji duniani ambapo mamlaka zinazohusika na maji Cape Town na California ,ambazo kwa kiasi kikubwa zimekumbwa na uhaba wa maji walifunga safari hadi Moshi kuja kujifunza ni hasa watu hawa wamewezaje.

Bila hiana MUWSA iliwapa elimu muhimu ya kuweza zalisha maji ya ziada katika maeneo yao ambapo walisema siri kubwa ni utanzaji wa vyanzo vya maji pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanya na serikali katika mitambo na miundombinu mingine.
Mamlaka nyingine mbili nazo kuzima mitambo kabla ya mwisho wa mwaka huu.
So cape town na California serikali zao zitakua hazijaweka hela kwenye sekta ya maji.....
 
Amini usiamini, California tatizo ni kubwa kiasi kwamba wanatumia hiyo teknolojia kubwa waliyo nayo kupangia kila nyumba iliyoko kwenye eneo lenye uhaba kiasi cha maji kinachoingia. Sasa humo ndani ndio mnapanga mtumie eje hicho kiasi cha maji, kuoga ni shower sio kujaza tub n.k.
Nimepitia makala za California water group wameandika hakuna shortage na wanaweka mfumo mpya wakuhifadhi maji unaendelea kujengwa hapo Hawaii........ Labda wewe unaongelea California love ile kama jangwa kwenye wimbo wa 2pac
 
Uchaggani kuna mengi ya kujifunza bila shaka!
Ukweli mtupu!
Mambo mengi sana yalikuwa poa kabla hata ya uhuru! Nakumbuka mimi wakati nakuwa ulikuwa una uwezo wa kupiga simu ya dharura na polisi wanafika fasta(kama sikosei, namba mojawapo ilikuwa ni 999). Fire brigade ilikuwa very reliable!

Darasani tulifundishwa umuhimu wa kuchemsha maji ya kunywa, lakini uchaggani kule sikumbuki kuchemsha maji ya kunywa. Maji ya bomba safi kabisa!
Kilmanjaro ndio lango la baraka za hili taifa na kupitia huu mkoa hili taifa litaneemeka na kubarikiwa "Viva Kilmanjaro "
 
mi nashangaa hao wanaotoka capetown na california wanakuja kujifunza nini hasa,wao hawajui kutanza maji au miundo mbinu mizuri ya maji inazalishwa tz? mi nnachokiona tafauti ni kuwa inawezekana eneo la moshi kuna maji mengi na watumizi wa maji ni kidogo kulinganisha na maeneo mangeni,hilo labda ndio la ajabu
Hapo ndipo utaona tofauti ya Mzungu na Mwafrika mzungu hata kama anajua anakuzidi ila yupo tayari kujifunza kutoka kwako akiona una jambo ambalo anahisi anaweza jifunza Mwafrika hawezi na ndiyo maana unawashangaa....japo nimeshangaa S.A nao waafrika wenzetu kuwa na akili ya mzungu
 
Moshi_Kilimanjaro! Wamejitahidi kwa mambo mengi hasa maji elimu na afya!
 
Mkuu utakua unaongelea moshi bar ya huko kwa bashite,moshi inashida ya maji sana japo mito ni mingi ila muwasa hawana jipya wapo tu kusubiri mishahara,ukienda pasua,rau,majengo,soweto maji ya shida yanatoka mara moja au mbili kwa wiki.
Muwasa hawana plan wangekua na plan maji yangefika mpka majengo
Jamaa angu acha uongo wewe sehem zote hizo nimekaa na ninaishi moja ya sehem.tajwa hakuna siku maji yamekatika hata nusu saa na.yakikatika lazima taarifa itolewe sasa wewe sijui.unazungumzia.mwaka gani
 
Uongo unakusaidia nini? Soweto ipi unayoizungumzia hapa! Na Padua ipi? Hiyo matindigani na kalimani ni uswahilini full vichochoro lakini Maji ni 24/7 sembuse Soweto na Pasua kwa J, rahibu?
Sehemu nyingi maji ya shida,soweto,majengo,rau,pasua ni majanga matupu
 
Wewe Habari Zako Zina chunvi nyingi.. Jana tu umetuaminisha tbc wamefunga mitambo bora Africa nzima hakuna.. Lakini tbc bado mbovu vilvile
Mwandishi nae kakupongeza. Hii inaonesha aina ya uandishi anayotumia. Anayoyasema si anayokusudia. Read between the lines and you will understand the message.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom