muwapende mahausigeli!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

muwapende mahausigeli!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanaizaya, May 24, 2008.

 1. m

  mwanaizaya Senior Member

  #1
  May 24, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hausigeli amnyonga bosi wake

  2008-05-24 09:24:43
  Na Romana Mallya


  Mfanyakazi za ndani aliyefahamika kwa jina moja la Maria, anadaiwa kumuua mwajiri wake, Bi. Lina Capuolalho, nyumba namba 116, mtaa wa Kitonga na Upanga, jijini Dar es Salaam.

  Hausigeli huyo ambaye alikuwa na siku nne tu tangu aanze kibarua, anadaiwa kuwa, baada ya kumuua bosi wake huyo, alimfunga kamba miguuni na mikononi na mwili akautelekeza kwenye uvungu wa kitanda na kutokomea kusikofahamika.

  Aidha, kichwa cha marehemu huyo, kilikutwa kikiwa kimefungwa kwa taulo hadi karibu na mdomoni.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Bw. Faustine Shilogile, alisema jana kuwa, mwili wa mwanamke huyo uligundulika juzi mchana na mlinzi wa mlangoni wa nyumba hiyo, Bw. Mwaluka Matonya.

  Kamanda Shilogile, alisema kwa mujibu wa mlinzi huyo, aligundua kuuawa kwa mwajiri wake baada ya kuingia chumbani kwake na kuukuta mwili huo ukiwa kwenye uvungu wa kitanda chake.

  Alisema mwili huo ulikutwa ukiwa umewekwa chali huku miguu na mikono vikiwa vimefungwa kamba.

  Kamanda Shilogile alisema wanamtuhumu hausigeli huyo kuhusika na mauaji hayo kwa kuwa walikuwa wakiishi wawili tu ndani ya nyumba hiyo.

  Alisema juhudi za kumtafuta msichana huyo zinaendelea wakati mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   
Loading...