Muvi gani ilikufanya uache angalia muvi zilizotafsiriwa?

fungi06

JF-Expert Member
Jul 1, 2020
632
854
Jana nimemka na weekend vibe nikasema embu kwanza nicheki muvi kali niliyo download

Ee bwana kuwasha gafla nakuta kumbe imetafsiriwa nikasema ewaaaaa bora ata nisichoshe akili kusoma sub title. Ghafla muvi imefika dk ya 10 sekunde ya 40 nikaona sub title ya muvi imeandikwa (dont come around me ill kill you" alafu ntafsiri akasema kumbe umefika hapa tokea jana unanisubiria tupambane😐" )

Nilikua nimeshikilia remote ya Mr UK yangu yenye inch 200 kama ukuta wa Mererani nikapiga nayo tv kwa hasira na kikombe cha chai mkononi nacho nikamalizia bamiza kwenye soketi.

Gafla nataamaki Tv haiwaki tena inaonyesha ukungu. Kuwaza nikagundua tv imeshakufa.

Mwenye TV kubwa nzuri ambayo aijamaliza mwezi ni inbox maana ninayo muvi yangu ingine nime download jana pia nataka niiangalie mda huu maana bosi achelewi kazini ata afike mda wa kufunga ofisi usipo niambia bosi umewai basi nabadili system nzima.

Pesa makaratasi hasara roho.
 
Back
Top Bottom