Muuza magazeti aliyedaiwa kuuawa maandamano Chadema aibuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muuza magazeti aliyedaiwa kuuawa maandamano Chadema aibuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 24, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muuzaji magazeti aliyedaiwa kuuawa wakati wa maandamano yaliyosababisha vurugu baina ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na askari wa Jeshi la Polisi, maeneo ya Msamvu mjini Morogoro hivi karibuni, Kasim Mdangu ameeleza namna alivyonusurika katika vurugu hizo.

  Agosti 27, 2012 iliripotiwa na vyombo vya habari nchini kuwa askari wa jeshi hilo mkoani humo walifyatua risasi za moto na na mabomu ya machozi kwa wanachama na wafuasi wa
  CHADEMA waliokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kuelekea kwenye mkutano wa chama chao na mtu mmoja aliyesemekana kuwa muuza magazeti aliuawa.

  Akizungumza na NIPASHE katika eneo analouzia magazeti lilolopo Mtaa wa Msamvu Kata ya Mbuyuni mjini Morogoro, Mdangu alikanusha taarifa hizo na kusema aliyeuawa ni mbeba mizigo, Ali Zona.

  "Watu wengi walishangaa baada ya kuniona kwa sababu walipata taarifa kuwa nimeuawa katika vurugu za
  CHADEMA na Polisi, ukweli ni kwamba aliyeuawa ni ‘kuli' (mbeba mizigo) Ali," alisema Mdangu.

  Alieleza kuwa Ali alikuwa akiishi mtaa wa Modeko ambao uko jirani na mtaa wao wa Msamvu na alikuwa akifanya kazi katika kituo cha magari ya mizigo yanayotoka mkoani Iringa kilichopo takriban mita 25 kutoka anapouzia magazeti.

  Alisema wakati wafuasi wa
  CHADEMA wakikimbizana na polisi, yeye alikuwa kwenye ofisi yake hiyo akiuza magazeti na baadaye marehemu (Ali) alifika kununua maji mahali hapo.
  "Marehemu alikuja kununua maji maana kipindi hicho pia tulikuwa tukiuza maji hapa.

  Gari la Polisi lilifika hapa likasimama, polisi wakaanza kutugombeza kwanini tumefanya mkusanyiko ilhali kulikuwa kumetolewa amri ya kutofanya maandamano, tukawaambia sisi hatukuwa na nia ya kuandamana wakaondoka," alisema Mdangu.

  Alisema "baada ya kuondoka baadhi ya watu waliokuwa hapa wakaanza kuwazomea…kwa jinsi lile gari la Polisi lilivyogeuka, nilijua kabisa kwamba kinachofuata ni kichapo nikaamua kukimbia.

  Ali hakukimbia maana tulimwacha hapa akipitia magazeti. Ghafla tukasikia mlio kama wa risasi hivi, tuliporudi tukamkuta ameanguka chini na kichwa chake kilikuwa kimeharibika vibaya."

  Mdangu alisema alishangaa kuona vyombo vya habari vikiripoti kuwa aliyefariki katika tukio hilo ni muuza magazeti katika eneo ambalo anauzia huku baadhi ya watu wakishtuka na wengine wakikutana naye wakiamua kumkimbia kwa sababu walipata taarifa kuwa ameuawa.

  "Jambo hili limekuwa likinikosesha raha, lakini kaka yangu Mohamed amekuwa akinifariji na kunisihi niachane nalo kwa sababu mimi si wa kwanza kuzushia kifo," alisema Mdangu.

  Awali ilielezwa kuwa wakati
  CHADEMA ikisisitiza kufanya maandamano kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na polisi, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.

  Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba ilikuwa ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.

  Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano hayo, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.

  Ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.

  Katika tafrani hiyo, kijana Zona, ambaye alikuwa anasoma magazeti aliuawa wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa
  CHADEMA.

  Polisi walidaiwa kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji.

  Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwendesha baiskeli, Hashim Seif ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni akiwa anapita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda, Frank Valimba aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni.

  Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, jeraha lililokutwa kwenye kichwa cha marehemu huyo lilitokana na kurushiwa kitu kizito.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wameua basi na yeye aliona, hicho ndio muhimu. Jina lake halikutajwa. Issue inabaki ni muuza magazeti au msoma magazeti. Lakini haisaidii kitu. Shilogile ajiuzulu.
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kumbe Polisi walighadhabika baada ya wafuasi wa CDM kuwazomea? kazi kweli kweli.
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndio maana tunahitaji tume huru, kuondoa utata, kila kitu kitajulikana na waliohusika wachukuliwe hatua.
   
 5. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,749
  Trophy Points: 280
  huyu naye alikwina (alikuwa wapi) muda wote huu? yanataka kuwa kama ya ngoswe haya..
   
 6. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ningeshangaa kama ungekosekana hapa!
   
 7. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ama kweli njia ya mwongo ni fupi. Walisema kuwa walikuwa wanabishana nao juu ya kuandamana! Kumbe walizomewa wakakasirika, wakaamua kugeuka na kuua kwa bunduki ya serekali. Mwema na Nchimbi hiyo haitoshi kuwaondoa kazini? Hata kumwondoa huyo Rpc Shilogile? Shame on police force!
   
 8. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwani alolazimisha kuandamana wakati polisi wamezuia ni nani? Tafakari,chukua hatua,usiwe unapenda kila unachokiona!
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mungu ni mwema,kwa kuwa huyu bwana hajafa basi tusiuane jamani kwanini tumwage damu kwa sababu ya siasa????
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu mwandishi wa hii habari ana udhaifu mkubwa sana. Aliyeuwawa na polisi ni Zona na hata huyo anayesema 'hakufa' anakiri aliyeuwawa ni Zona. The only pieace of infomation ya kusahihisha ni 'occupation' ya merehemu. Alichotakiwa kusema ni kwamba 'ajira' ya marehemu Zona haikuwa kuuza magezeti bali kubeba mizigo.
   
 11. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,478
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Unatakiwa ubongo wako uwe kamili ndugu, unatakiwa ujue mazingira ya mauaji hayo
  - Maandamano yariruhusiwa kwa makubaliano ya awali
  - Maandamano yalizuiriwa kwa shinikizo la kisiasa (CC Ikulu)
  - Aliyeuawa halikuwa akijisomea magazeti na hakuwa mwandamanaji.
  - Polisi wameua baada ya kuzomewa na raia je ukizomewa inakupa amri ya kuuwa?
  - Shilogile kwa hili alitakiwa awajibike kwani yeye ndio mtoa amri na inaonyesha dhahiri kila kitu kilipangwa mauaji yafanyike katika kila mkutano wa CDM, mfano Iringa na kama CDM wangeendelea baada ya ile ya Iringa inawezekana yangetokea zaidi ya yaliyotokea.
  *** Usipende kutukana bila kuushirikisha vizuri ubongo wako na mishipa yako ya fahamu.
   
 12. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hilo ndo tatizo lako! hushughulishi huo mpira wa duara juu ya shingo yako,mwenyewe unaita kichwa,kufikiri na kuona beyound bounderies! unaamua moyo wako ukubali unachohisi ww kuwa ni sahihi! Think twice!
   
 13. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Whatever the case, haijalishi kazi ya aliyeuliwa, cha msingi hapa ni kwa nini mtanzania aliuawa bila kufikishwa mahakamani kujitetea kama alikuwa na kosa??? tusibadili mjadala, bado tunataka kujua mazingira na uhalali wa huyo mtanzania kuuliwa na " kitu chenye ncha kali kinachopaa" kinyama vile na hakuna aliyechukuliwa hatua mpaka sasa. kujadili jina au kazi yake sidhani kama ni muhimu, la muhimu hapa ni kwa nini mtanzania anyang'anywe haki yake ya kuishi na hatua hazijachukuliwa kwa wauaji???
   
 14. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ukombozi lazima hata kama wanafiki mtatukatisha tamaa, Viva M4C
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Nimeupenda upembuzi wako wenye ladha.
   
 16. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kuliona hilo.Uchambuzi wako ni makini kamanda
   
 17. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Sijaona jambo kubwa sana hapa.....ni makosa tu ya maelezo ya marehemu ambayo ni kuhusu kazi yake.....bado haitabadilisha hoja kuu ya mauaji....cha msingi hapa inayakiwa umakini wa wanahabari katika kuchukua maelezo..... si vibaya wakawa na uharaka lakini na umakini unahitajika pia
   
 18. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwa akili yako ndogo kosa la kuandamana adhabu yake ni kifo?
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Kikwete hataki kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza wimbi la muda mrefu la mauaji ya raia. Lakini iwe sasa au baada ya miaka 10....tutachunguza na kuwafikisha wote waliohusika ili ukweli ujulikane na haki itendeke.

  Hivyo basi kadiri mshale wa sekunde unavyozunguka, basi wahalifu muda wao kusimama mahakamani ndivyo unavyokaribia.

  Badala ya kuhangaika kuizuia CHADEMA ningewashauri CCM na serikali ya Kikwete wafanye mojawapo ya haya hapa chini:

  1) Walipaswa kuzuia mshale wa saa usizunguke

  2) Walipaswa kuzuia dunia isijizungushe ktk mhimili wake.

  Kama hayo hawayawezi basi hawa akina Mwema (?), Chagonja, Kamuhanda, Shilogile, Zombe, Mahita na wengine lazima watasimama ktk vizimba vya mahakama. Wako wapi akina Pinochet? Mpaka kesho wauaji wa kimbari Rwanda wanasimama vizimbani kila kona ya dunia
   
 20. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hiyo habari ilivyoandikwa imekaa mno kiudanganyifu kuuza habari.Ukweli mchungu unabaki pale pale polisi waliua na walikuwa wakitii aina fulani ya amri haramu.Aliyewatuma anasema waliua kwa kitu kizito,wakati ambapo risasi haifichi chochote.Hawataweza kutuua sote kabla ya kuumbuka.Yule homeboy aliyekuwa akiwanyang'anya wafanya biashara mali na fedha na kuwaua akidai ni majambazi si alifika mwisho ikasanuka?Yule mwingine kule kanda za kaskazini aliyemwua baba wa watu kwa ajili ya ugomvi unaohusu matiti ya mwanamama akamsingizia jambazi naye 40 yake si ilifika na sasa ni desk officer hapa town? pia na majinamizi yanamwandamisha!Hata walindane namna gani mauti itawaumbua na hakuna cha Daktari wa Falsafa wala mzee wa polisi sjamii wala mzee wa inteligensia,WAMESHASHINDWA!WAMESHAKUFA WAKIWA HAI,NI WAOGA WA MABADILIKO!
   
Loading...