Muungwana Wakati ni huu Tunaitaka Tanganyika yetu

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,609
1,250
Wakati tukiwa na Raisi Kikwete ambae yeye ndie aliekuwa mpiganiaji wa jambo hili alipokuwa akisota bungeni ,kinachohitajiwa ni kusituliwa tu na kuambiwa ule wakati ndio huu.
Tunaitaka Tanganyika.
Tunataka kufuta kasoro za Muungano.
Tunataka Raisi wetu.
Tunataka Bendera yetu.
Tunataka Serikali Tatu.
1 ) Mkataba wa Muungano, 1964, ulitoa sura ya kuwepo kwa shirikisho la serikali tatu ambapo hapangekuwa na serikali moja iliyo na mamlaka makubwa kushinda nyingine.

2 ) Mkataba wa Muungano ulitaka kuwepo kwa serikali tatu au mamlaka ambazo zingeundwa kiuunganishi ambazo katika waraka huo zilitajwa kuwa ni mmoja wa mamlaka kuwa ni Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano.
Hicho kifungu hakikuitaja CCM na wahafidhina wake kuwa ndio wamiliki wa nchi mbili hizi hivyo inatakiwa kutojihusisha kabisa na madai na kujifanya wao ndio walindaji wakubwa kumbe ni mafisadi wakubwa.

3 ) Serikali ya Muungano unapoilinganisha na kuipima na Zanzibar au Tanganyika ambayo haipo, ni salio la uzawa wa nchi hizo na haiwezi kuwa na mamlaka yake wenyewe, isipokuwa kwa yale mamlaka iliyomegewa. hapa kunaifanya Zanzibar iwepo kama Nchi yenye maamuzi yake na Tanganyika haina.

Sasa ni mfumo wa Vyama vingi na hivyo hivyo ili mambo yaende sambamba kunahitajika serikali nyingi , kwa vile Muungano wetu unashirikisha nchi mbili kunahitajika serikali Tatu , ili kuvutia nchi nyengine nazo ziweze kujiunga ,jirani zetu wanataka kujiunga lakini wazo la kupoteza serikali yao ndio kikwazo kikubwa naamini kabisa ikiwa tutaamua kuweka serikali Tatu basi Muungano huu utakuwa na kuzivutia nchi nyingi jirani na hivyo kuweza kupata East African Block.
Hivi tujiulize kama Burundi atataka kujiunga na Muungano wa Tanzania atatakiwa afanye nini ? Na tutazame mfano wa European countries how they manage to get on top of their union na kuifanya fedha yao kuwa juu kuliko dola.
Leo Tunajulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania japo siku hizi neno Muungano limeondolewa kinyemela nyemela na Chama tawala ambacho kimejitangazia kushika hatamu ,sasa ukiangalia kuna Muungano wa East Africa
,imewezekanaje kuwepo kwa Muungano huo wakati ndani yake kuna nchi mbili nazo zina Muungano ,ndio nikasema huu Muungano tulio nao sio sahihi kwa hapa tulipo ni lazima kuwepo na Tanganyika ili kuweka sawa mambo ya Muungano kwa eneo zima la East Africa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom