Muungano wetu, Rais wa Zanzibar anapokuwa waziri

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Yaani rais wa nchi ya Zanzibar anakuwa waziri tena anaapishwa na rais mwenzake.

Kweli huu ni muungano wa pekee na wa kindugu.

Kwamba unakuwa rais Zanzibar na wakati huo huo ni Waziri yaani unakuwa na vyeo viwili wakati mmoja.Hapa kwa mtazamo wangu kuna kuzugana tu na ni dhahiri muungano wetu una matatizo makubwa.

Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inampa mamlaka rais wa Zanzibar ambaye ni waziri wa (JMT) kugawa mikoa kwa kadiri anavyoona inafaa. lakini wakati anafanya hayo yeye ni Waziri wa JMT.

Kuna haja ya jipu hili kupatiwa dawa.
 
kawa waziri wa nini mkuu?
asimsahau jecha kwenye unaibu ikishindikana hata ukatibu mkuu wa hiyo wizara ya Zanzibar.
 
kawa waziri wa nini mkuu?
asimsahau jecha kwenye unaibu ikishindikana hata ukatibu mkuu wa hiyo wizara ya Zanzibar.
Huyu ni waziri asiye na wizara maalum

Tazama maajabu ya Tanzania. Kabla ya kubadilishwa sheria Rais wa Zanzibar alikuwa ndiye makamu wa rais wa JMT na ile dhana ya muungano ilipatikana kwa rais wa zanzibar kuwakilisha nafasi ya Muungano moja kwa moja. (Direct). Lakini watawala wenye dhamira zao walibadilisha hili kwa wingi wa wabunge na mihemko bila kuangalia haki.

Kuna watu kazi yao ni ubishi tu. Kwa hali hii lazima ndugu zetu Wazanzibari walalamikie Muungano huu.
 
Yaani rais wa nchi ya Zanzibar anakuwa waziri tena anaapishwa na rais mwenzake.

Kweli huu ni muungano wa pekee na wa kindugu.

Kwamba unakuwa rais Zanzibar na wakati huo huo ni Waziri yaani unakuwa na vyeo viwili wakati mmoja.Hapa kwa mtazamo wangu kuna kuzugana tu na ni dhahiri muungano wetu una matatizo makubwa.

Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inampa mamlaka rais wa Zanzibar ambaye ni waziri wa (JMT) kugawa mikoa kwa kadiri anavyoona inafaa. lakini wakati anafanya hayo yeye ni Waziri wa JMT.

Kuna haja ya jipu hili kupatiwa dawa.

Ina maana hukumuona Jaji Mkuu?
 
Ingekuw Poa kama jpm naye angeenda kuapishwa kuwa waziri zenj nawaza tu kwa sauti
 
  • Thanks
Reactions: 999
Suala hilo lipo kikatiba.Mbona huulizi na uwepo wa wabunge wa Zanzibar kwenye bunge la Tanganyika na huwezi kuwaona wa Tanganyika kule Zanzibar?
 
Na anaweza baadaye kuja kuwa rais wa JMT kama alivyofanikisha Mzee Ruksa! Mzanzibar yo yote ana haki ya kugombea nafasi ya urais wa JMT - acha upotoshaji wako wa kibwege. Huo ndiyo muungano wa 'a united republic' yetu kama ilivyo 'united states' ya Amerika!
 
Mimi sio mtaalamu wa katiba,nauliza katika kuweka wiano sawa,hivi kama ikitokea raisi wa Tanzania akatoka visiwani,nani kutoka bara ataapishwa kuwa waziri Zanzibar?
 
Suala hilo lipo kikatiba.Mbona huulizi na uwepo wa wabunge wa Zanzibar kwenye bunge la Tanganyika na huwezi kuwaona wa Tanganyika kule Zanzibar?

Yaani si kila suala kuwepo kikatiba kuwa ndio haki. hapa kuna matatizo zaidi wewe umesaidia kuonesha hayo matatizo ya muungano wetu. wabunge wa Zanzibar wapo bungeni wanajadili mambo ya Tanganyika kwa wizara ambazo hata si za muungano.

Halafu hakuna tofauti za vikao vya bunge kwa mambo ya Tanganyika na ya Muungano imekuwa Tanganyika ndio muungano na muungano ndio Tanganyika.

Huu muungano huu''''''
 
Yaaani haya ni maajabu ya Dunia sijapatapo kuona yaani Rais wa Nchi unakua waziri kwa nchi nyengine
Sijui wametumia katiba na sheria ipi mbona hayati Mzee Karume hajaapa kua waziri au aboud jumbe sijaskia kula kiapo hivi ni vituoko kuliko wali wa maji
 
Yaani rais wa nchi ya Zanzibar anakuwa waziri tena anaapishwa na rais mwenzake.

Kweli huu ni muungano wa pekee na wa kindugu.

Kwamba unakuwa rais Zanzibar na wakati huo huo ni Waziri yaani unakuwa na vyeo viwili wakati mmoja.Hapa kwa mtazamo wangu kuna kuzugana tu na ni dhahiri muungano wetu una matatizo makubwa.

Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inampa mamlaka rais wa Zanzibar ambaye ni waziri wa (JMT) kugawa mikoa kwa kadiri anavyoona inafaa. lakini wakati anafanya hayo yeye ni Waziri wa JMT.

Kuna haja ya jipu hili kupatiwa dawa.
Vipi kuhusu mshahara na marupurupu ya huu uwaziri, nayo pia anakomba au ndo vile tena?
 
Ukitafsiri kwa kiswahili Cabinet kuwa ni baraza mawaziri lazima uamini kila mjumbe wa Baraza la Mawaziri ni lazima awe Waziri. Hata Magufuli,Samia na Engineer Kijazi utawaita ni mawaziri kwa kuwa tu wanahudhuria vikao hivyo.
 
Na anaweza baadaye kuja kuwa rais wa JMT kama alivyofanikisha Mzee Ruksa! Mzanzibar yo yote ana haki ya kugombea nafasi ya urais wa JMT - acha upotoshaji wako wa kibwege. Huo ndiyo muungano wa 'a united republic' yetu kama ilivyo 'united states' ya Amerika!

Yaani unaona matatizo hayo. Hata ikitokea Rais wa zanzibar kuja kugombea kuwa rais wa JMT haimaanishi kuakilisha nafasi ya Zanzibar katika huo muungano. Anakuwa ni yeye mwenyewe (personal)

Muungano huu kama unavyouita " United Republic yetu" umekuwa ni kwa maslahi mapana ya Tanganyika. Dhana ya unitred republic imekufa kwa zanzibar. Zanzibar haionekani kwenye muungano na Tanganyika ndio imekuwa Tanzania.
 
Hata Magufuli akienda Zenji anakuwa mdogo kwa rais wa Zanzibar, rais wa Zenji anapigiwa mizinga huku wa Tanganyika akishuhudia.
 
Back
Top Bottom