Muungano watawala Kigoda cha Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano watawala Kigoda cha Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtwana, Oct 16, 2012.

 1. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Myerere, Profesa Issa Shivji, amewapa angalizo Watanzania kuhusu Muungano kwamba changamoto zinazoukabili zisipotafutiwa ufumbuzi yanaweza kutokea matatizo makubwa.

  Msomi huyo alitoa angalizo hilo juzi kwenye mdahalo wa kigoda cha Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa.

  Profesa Shivji alisema Muungano unapaswa kujadiliwa kwa kina vinginevyo zinaweza kutokea athari kubwa kwa nchi zikiwamo vurugu. Shvji alitoa angalizo hilo baada ya wachangiaji kadhaa kusema wazi kwamba Muungano uvunjwe.

  Kwa mujibu wa Shvji, changamoto za Muungano zikiachwa bila kujadiliwa na wananchi kutishwa wasiujadili fursa hiyo inaweza kutumiwa na maadui kuuvunja.

  Aliongeza kuwa kuna umuhimu wa kuwashirikisha wananchi kuujadili Muungano huo kwa kuwa wakati wa kuasisiwa kwake walihusika viongozi peke yao.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, alisema muungano huo una faida kubwa kwa pande zote, lakini hakuna mfuko wa pamoja wa fedha zinazopatikana.

  Alisema kuwa Ingwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema uundwe mfuko wa pamoja na kuwe na akaunti ya kuweka fedha zatokanazo na muungano, lakini hadi leo hakuna kitu hicho.

  Alifafanua kuwa kuna ripoti inaonyesha kuwa mapato yanayotokana na muungano ni mkubwa, lakini upande wa Tanzania Bara unakataa ripoti hiyo kuwekwa wazi.

  Akizungumza katika mhadalo huo, mwanahabari nguli, Jenerali Ulimwengu alikubarina na Mzee kuhusiana na kuwepo kwa fedha katika serikali ya Muungano, lakini zinaliwa na viongozi.

  Aliwataka wananchi kuendelea kuujadili Muungano ili baadaye upatikane wanaoutak badala ya kuuvunjaa.


  Nu Uvunjike Muungano tumechoka Wazanzibari maana tunadhulumiwa haki zetu hatupati hata nafasi nzuri za kazi kila nafasi wanachukua watu wa bara tumechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huu muungano huu. Ipo kazi. kama hatutatumia fursa ya katiba mpya kuuimarisha sijui?
   
 3. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Tena kazi ipo kweli maana tusipoziba ufa tutajenga ukuta sasa na nyufa zenyewe hawataki kuziziba sasa ndio mana sisi wazanzibari tunasema hatuutaki muungano wenye manufaa kwa pande moja tuu
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Binafsi nawachukia kweli kweli wanao ung'ang'ania huo muungano 'fake'

  Wee uliona wapi 'sungura' kuungana na 'tembo' kama si kuburuzana tuu
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hahaaa. poleni sana wazenji, uliopo ni muungano wa nyerere na karume na si wa watanganyika na wazanzibari
   
Loading...