Muungano waibua mpasuko CCM Zanzibar

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2][/h]


Na Mwinyi Sadallah



4th August 2012











Ameir.jpg

Mwanasiasa Mkongwe Zanzibar, Ali Ameir Mohamed



Wanasiasa wawili wakongwe visiwani Zanzibar wanatoafautiana kimtazamo katika muundo wa Muungano uliyoyaunganisha mataifa huru mawili ya Tanganyika na Zanzibar Januari 12, mwaka 1964 imefahamika.

Wakiongea kwa nyakati tofauti toka vyanzo mbalimbali vya maoni yao, wanasiasa hao ni Hassan Nassor Moyo na Ali Ameir Mohamed ambao waliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Matamshi ya Moyo na Ameir yanajitokeza wakati huu huku kukiwa na vuguvugu kubwa la ajenda ya utoaji na ukusanyaji wa maoni ya wananchi ya uundwaji wa katiba mpya ya Tanzania ulioibuliwa na Seriikali ya awamu ya nne Tanzania chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Wakati Mzee Moyo akitaka uwepo Muungano mpya wa mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar, Ameir alisema nje ya muundo wa Serikali mbili kuna mwelekeo unaogofya wa kuyasaliti Mapinduzi ya 1964 ili kuviza historia ya chama cha ukombozi cha Afro Shiraz Party.

Ameir aliyewahi pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, alieleza kuwa dhana ya Muungano na Mapinduzi ni kama watoto waliozaliwa wakiwa wameungana viungo vyao hivyo ni vigumu kuwatenganisha ghafla.

"Ukiwatenganisha bila ya utaalam watoto hao, maumbile ya maisha yao yanaweza kuleta hatari zaidi, uzoefu wangu kidogo unanionyesha hilo jambo mazingira yake ni magumu kutimia," alisema Ameir.

Ameir alisisitiza haja ya msingi kwa mataifa hayo kubaki na muundo wa sasa wa kikatiba ili kulinda misingi ya umoja, udugu na utengamano aliyodai ulianza tokea miaka 48 iliyopita.

Ameir alisema nje ya Muungano kuna mkakati utakaotoa mwanya kwa maadui wa ndani na walioko nje ili kuhatarisha umoja wa kitaifa na kuleta mgawanyiko utakaovitikisa visiwa vaya Unguja na Pemba.

Moyo kwa upande wake anapingana na mtazamo huo akisema haja ya kuendelea na Muungano wa kikatiba imepitwa na wakati huku akitaka wanachama wenye fikra mbadala ndani ya CCM wapewe nafasi ya kusilizwa bila ya kutishwa.




CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni




lg.php

<a href='http://www.ripoti.com/openx/www/delivery/ck.php?n=a5793a20&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE' target='_blank'><img src='http://www.ripoti.com/openx/www/delivery/avw.php?zoneid=267&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE&n=a5793a20' border='0' alt='' /></a>









Habari Zaidi

[h=3]Articles[/h]Mgomo:Ngoma nzito


Lissu shahidi mkuu rushwa ya Wabunge


Papaa Msofe mbaroni kwa tuhuma za mauaji


Mgomo wa walimu wafungisha shule


Maofisa elimu, wakaguzi, Arusha wahaha
 
Tatizo hapa sio Muungao ni kuona chama cha ccm kinapokonywa hatamu ya kujifanya wao ndio Serekali na mamuzi yao yawe ndio yao tu kwa elani za chama chao, hawa wanajihisi kuwa Watanzania wote ni ccm.
 
Back
Top Bottom