Muungano wa Zanzibar na Tanganyika unaacha maswali mengi

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
Habari wajumbe! Natumai mu-buheri wa afya
Binafsi Kuna jambo linanitatiza sana kila nikifikiria

Historia Inatuambia Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuwa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

kwamba Tanganyika iliungana na Zanzibar kuunda TANZANIA lakini Baada ya Muungano huo Tanganyika haipo tena , ila Zanzibar ipo na inajiendesha

Tanganyika + Zanzibar = Tanzania + Zanzibar

Tanganyika iko wapi Baada ya Muungano mbona Zanzibar naiona tusaidiane
 
Muungano wa kupe na ng'ombe

Kiufupi ni muungano wa hovyo kuwahi kutokea duniani.

Cha ajabu walamba asali wapo kimya..muda utaongea.

Ataibuka farao ambaye hakumjua Yusufu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tanganyika mbona bado ipo mkuu, kama upo Dsm njoo mitaa ya Lumumba pale ukiona majengo yana bendera za mboga mboga tu ingia ndani tukupe maelezo.
 
huu Muungano faida yetu kubwa ni usalama wa bara, ni ngumu sana kulinda mipaka ya bahari, endapo hatutaicontrol Zenji na kujua kila kinachoingia kutoka Usalama wetu utakuwa shakani sana. Itikadi zao na mwamko wao umeelemea mahali flani ambapo bila kuwazuia wanaweza kuruhusu masuala mengine ambayo kutokana na upana wa bahari yanaweza kuja kutuletea madhara huku bara
 
Hili la ulinzi lingetufanya tuwe macho na mambo ya msingi.
 
tushaongea mpaka makoo yatakauka sasa...

Zanzibar wapewe nchi yao maana watanganyika wanaulalamikia ila wao ndio wameungangania hawataki kuuachia.
 
Swali mojawapo mtambuka na linalofikirisha sana ni ukatwaji wa kodi x2.

1. Inakuwaje ninunue bidhaa Znz nikiingiza bara niilipie tena kodi!?

I think something fishy is going on.
 
Muungano ulikuwa na umuhimu miaka sitini na sabini tu
Lkn kwa sasa huu muungano ni kupe, tanganyika ananyonywa na wale watu wa kule
Na imebaki faida kwa wanasiasa tu
 
huu Muungano faida yetu kubwa ni usalama wa bara, ni ngumu sana kulinda mipaka ya bahari, endapo hatutaicontrol Zenji na kujua kila kinachoingia kutoka Usalama wetu utakuwa shakani sana. Itikadi zao na mwamko wao umeelemea mahali flani ambapo bila kuwazuia wanaweza kuruhusu masuala mengine ambayo kutokana na upana wa bahari yanaweza kuja kutuletea madhara huku bara
Hiyo ni hoja nyepasi mno!
 
Swali mojawapo mtambuka na linalofikirisha sana ni ukatwaji wa kodi x2.

1. Inakuwaje ninunue bidhaa Znz nikiingiza bara niilipie tena kodi!?

I think something fishy is going on.
Zanzibar wanalipa 60% kodi kama hawajabadilisha; hivyo ukileta hicho kitu huku lazima ukilipie ile asilimia 40%
 
Back
Top Bottom