Muungano wa Upinzani Umekwamishwa na Nini?

mzanganyika

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
257
6
Zile harakati za kuwa na Muungano ama ushirikiano wa vyama vya siasa katika chguzi umekwama wapi?

Wapinzani walivyoanza kuzungumzia swala hili nilikuwa na matumaini makubwa sana kwamba sasa tutakuwa na ushindani wa kweli wa siasa.

Nikiwa kama Independent nilifarajika, sasa sisikii lolote. What happened?
 
Ni vigumu sana vyama ya upinzani kuwa na muungano wowote sustainable kwa sababu zifuatazo.
1. Conflict of interest: Kiongozi wa chama "A" ana taka kuwa raisi pia kiongozi wa chama "B". Nani amuachie mwenzie? Chama "X" kina taka vimbo fulani lakini chama "Y" ina litaka jimbo hilo pia. Yupi amuachie mwenzie? Na vitu vingine kama hivi.

2. Different policies & philosophies: Kila chama kina policies zake ambazo zina taka ziwe incorporated na pia zina falsafa tofauti. Za nani zipewe kipaumbele?

3. Different power and influence: Hata kwenye upinzani kuna vyama vyenye nguvu kuliko vingine. Vikiungana kuna vyama vidogo vitakavyo mezwa. Viongozi wa vyama hivi vidogo hawata taka kumezwa lakini pia hawata kuwa na sauti kubwa kwenye huo muungano.

4. Different leaders: Vyama vikiungana ina maana lazima kuna watakao kuwa viongozi wakuu wa vyama binafsi. Sasa kwa mfano mwenyekiti wa chama kimoja ata kuwa na cheo gani kwenye huo muungano? Ata kubali hicho cheo?

5. Presidency: Hii ndiyo sababu kubwa ya kuto kuungana. Mkiungana na tuseme by some turn of events mnashinda nani anakuwa raisi? Nani atakua kwenye baraza la mawaziri? Kila kiongozi mkuu wa upinzani ana utamani uraisi sasa una fikiri atakua tayari kuunganisha nguvu na kumpa mtu mwingine uaisi?

Kuna sababu zingine nyingi lakini hizi mimi ndiyo nimeona ndiyo kuu na obvious kwa kuangalia haraka haraka.
 
Nafikiri sababu kubwa ni hii posho/ruzuku. Chama kinachokuwa na wabunge wengi ndicho kinachopata ruzuku nono. Kwa hivi vyama havina njia nyingine ya mapato ya kukidhi, kila chama kinawania kupata wawakilishi/wabunge wengi iwezekanavyo. Wanachama michango yao ni ya kusuasua. Mara nyingi hawatoi kabisa. Wanakuwa washabiki tu. Sasa hivi vyama vitajiendeshaje? Kwa hiyo lawama si ya vyama peke yake. Halafu na njaa na uchu wa madaraka vinachangia navyo.
 
Kwa concept yako basi ruzuku ndiyo ingekua incentive ya kuungana. Kama usemavyo wingi wa wabunge ndiyo una determine ruzuku. Kwa maana hiyo basi wabunge wote wa upinzani wa sasa wangekua wa chama kimoja ina maana ruzuku kubwa zaidi. Am I right?
 
zile harakati za kuwa na muungano ama ushirikiano wa vyama vya siasa katika chguzi umekwama wapi?

Wapinzani walivyoanza kuzungumzia swala hili nilikuwa na matumaini makubwa sana kwamba sasa tutakuwa na ushindani wa kweli wa siasa.

Nikiwa kama independent nilifarajika, sasa sisikii lolote. What happened?
...what a fuckken suggestion!!!
 
...what a fuckken suggestion!!!

Chama pekee chenye uwezo wa kutikisa na kung'oa CCM visiwani ni CUF, katika Muungni hakuna hata chama kinacjoweza kuapata hata 20%.

Bila ya alliance CCM lazima ipete na ndio maana wagombea wake wanasema hawajui chanzo cha umasikini na bado wanapeta.
 
Palikuwa na katuni niliiona mwaka 2000, ilikuwa inauliza suala hilihili. Ikiwaonyesha viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani:

"Kuweka mgombea mmoja maana yake ni mimi" -- mmoja anasema.

"Nisipogombea Urais nji hii mwaka huu basi nimelogwa!" -- mwingine anasema.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom