Muungano wa UKAWA hauna tofauti na Muungano uliopo, wanachokipinga hakieleweki.

kitambiheshima

JF-Expert Member
May 27, 2013
452
116
Ndugu wanajamvi nimetafakari kwa undani katika kujaribu kuona hoja na maantiki ya vyma vya upinzani kuupinga muungano uliopo wa serikali mbili. Ukiuchunguza kwa umakini aina ya muungano wa vyama vitatu vya upinzani vinavyounda ukawa, unagundua kuwa kinachpingwa na vyama hivyo ndicho kilichofanywa kwenye muungano wa vyama hivyo.

Muungano wa ukawa umetengeneza chama kingine kisichosajiliwa (ukawa) ambacho kimekuwa na nguvu kikivisuppress vyama vya cuf na nccr-mageuzi huku chadema kwa ustadi wa hali ya juu kikiendelea kujitanua. Mathalani kwenye mikutano ya ukawa unakuta bendera zinazotawala ni za chadema, salamu ya ukawa ni kama ya chadema ambapo watu wanakunja ngumi na kisha kuitikia kibwagizo cha "ukawaaaaaaaa,.............pamoja daima". Aidha mavazi yanayotawala kwenye mikutano ni ya chadema. Ikiwa haitoshi, angalia safu ya mawaziri vivuri kwenye kambi rasmi ya upinzani, wizara nyeti zote zimechukuliwa na cdm huku vyama vingine vikiambulia unaibu waziri na pengine uwaziri wa viwizara vidogo. Kama hiyo haitoshi pia, angalia safu ya uongozi, mbowe na Slaa,ndiyo the highest leaders wa ukawa....................... Ni mengi inachosha kuyaandika!
 
we ulizaliwa premature na ulichelewa kulia,na yale maziwa ya mama (ako)ya kwanza uliyakosa
 
Hivi kwa kuna wizara kubwa kama ya fedha,ujenzi na elimu? Hata kibajeti?
Kama wewe ni ACT au CCM leta sera na hoja.
Na hoja sio lazima iwe ya kuisambaratisha UKAWA.
Muundo wa serikali tatu sio wa ukawa ni wa Rasim ya wananchi.

Serikali mbili zimevurugwa na mabadiliko ya katiba ya Zanzibar na haiwezekani tena kufikia malengo ya waasisi ya kuwa na serikali moja imara ya Tanzania.Watanganyika hawawezi tena kuendelea kulipia nchi nyingine umeme na ulinzi halafu wao wapige siasa tu.
 
Back
Top Bottom