Muungano wa TANU na ASP, si Tanganyika na Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano wa TANU na ASP, si Tanganyika na Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Head teacher, Apr 26, 2012.

 1. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukiutazama muungano huu kwa undani utagundua kuwa ni muungano wa vyama vya tanu na asp, uliozaa c.cm. Ukilinganisha na muungano wa vyama, ambao baada ya muungano vyama hivyo vilikufa rasmi, muungano wa tanganyika na zanzibar, ni utata mtupu. Nasema huu ni muungano wa tanu na asp kwa sababu baada ya ccm kuanzishwa 1977, ndipo katiba ya muungano ilifanywa rasmi, na imeendelea kutumika mpaka sasa.

  Hivyo basi, jaribio lolote la kuvunja au kuurekebisha muungano litahatarisha uhai wa ccm, ambapo ccm tanganyika watahitaji chama chao tanu, na zanzibar asp yao. Huo ndo utakuwa mwisho wa mkoloni mweusi kutunyonya.


  Jmt, mtupe hati ya muungano, au documenti yeyote waliyo kubaliana babu zetu. La sivyo nyerere alioa karume bila posa. Wakazaa watoto haramu watanzania
   
 2. O

  ONDIECK OTOYO JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2014
  Joined: Nov 28, 2013
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kinachosumbua ni upuuzi wa kitu batili kinachoitwa muungano bila kutafsiri maana hali ya ''MUUNGANO'' maana hali ya muungano ni vitu kuanzia viwili kuhungana na kuwa kimoja na siyo viwili kuhungana na kuwa mbili au tatu hapo hakuna muungano bali kuna urafiki, na kilichofanyika kati ya mwalimu nyerere wa tanganyika na shekhe karume ni kuunganisha vyama TANU +ASP=CCM NA AIKUWA KUNGANISHA SEREKALI ndiyo maana zanzibar ikabaki na rais wake na serekali yake na tanganyika ikaendelea na uongozi wake kwa mgogo wa muungano na jambo hili ilitengamaa kwa sababu chama kilikuwa kimoja ccm ambayo ilikuwa na kiongozi mmoja na ndiye alikuwa rais wa jamhuri wa muungano,na muungano huo hauna faida kwa wananchi wa tanganyika, unafaida kwa wazanzibari kupata nafasi za upendeleo, pamoja na haki ya kumiliki ardhi tanganyika wakati mtanganyika hana haki ya kumiliki ardhi zanzibar huu ni unyonyaji kama wakati wa ukoloni, swali ya kujiuliza nilini makamu wa rais, waziri mkuu ,pamoja na mawaziri waliyopewa nafasi kwa sababu ya uzanzibar wao walienda zanzibar kufanya kazi ya muungano kwa wananchi wa zanzibar moja kwa moja kama wanavyofanya hapa tanganyika huu ni unyonyaji usizingatia haki sheria na usawa kwa misingi ya kichama na kulazimisha kupindisha ukweli kama wanataka muungano ni serekali moja tu pemba na unguja zinakuwa mikoa mbona ccm imekuwa moja huu ni muungano wa kitapeli usiyo na faida kwa wananchi wa tanganyika zaidi ya viongozi wa ccm na ikajengwa mfumo wa upendeleo wazanzibari wanauziwa umeme ilitolewa tanganyika kwa bei na fuu huku wanganyika wakiuziwa ka bei ya juu, mali iktolewa tanganyika kwenda zanzibar ailipiwi kudi, lakini ukitoa mali zanzibar kuja tanganyika unalipia kodi huu ni muungano wa aina gani, zanzibar ina katiba yake, zanzibar ina bnendera yake, zanzibar ina wimbo waka, na ina rais wake anayepingiwa mizinga 21 na kukangua gwaride hapa kuna nchi mbili inayotawaliwa na chama kimoja ndiyo ukweli mchungu kwa wanyonyaji weusi,walijaa kiburi na ulevi wa madaraka, kwa kung'ang'ania kulazimisha matakwa yao kwa gharama yoyote hii aikubaliki akiungwa mkono na watumwa wachache wa kiuchumi na kifikra na kuogopa kupinga matakwa ya manyabara wa wakoloni hao kwa kuofu ya kukosa chakula
   
 3. F

  Falconer JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2014
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Ondieck Otoyo, aise, umeongeya. Kama wewe ni JARAMOGI, lazima nikuvulie kofia.
   
 4. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2014
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  acha uchafu wa baharini uende na bahari
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2014
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Nje ya muungano hamna CCM. Nje ya muungano ipo TANU na ASP, hili ndilo linatia hofu na kuwakosesha usingizi CCM. Mungu ibariki Tanganyika Mungu ibariki Zanzibar, Mungu barik ASP na TANU.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2014
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kama ilivyokuwa kwa TANU + ASP ikapatikana CCM iwe iwe hivyo TANGANYIKA + ZANZIBAR tupate TANZANIA

  Mbeya, Tanga, Unguja, Pemba etc ibaki kuwa mikoa ya Tanzania
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2014
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapo sasa watalazimika kuifufua TANU !!!
   
 8. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2014
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Keep on dreaming. Zanzibar shall not die.
   
Loading...