Muungano wa Tanganyika na Zanzibar upoje? Mimi huwa sielewi chochote

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
663
1,676
Hivi ndugu zangu hivi huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar upoje huu mimi ua sielewi chochote kuhusu huu Muungano.

Mimi naishi katika nchi ambayo ina Muungano wa nchi mbali mbali. Sitokwenda mbali nitachukuwa mfano wa Quebec na Canada.

Quebec ilikuwa nchi ambayo walijiunga na Canada na Quebec ndo mkoa pekee wa Canada ambao watu wake wanazungumza Kifaransa ila sijawahi kusikia sijui timu ya Taifa ya Quebec au Rais wa Quebec au mengine kuhusu nchi huu wa Tanganyika na Zanzibar ukoje?
 

Satu

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
253
460
Kama ulivyoshauriwa hapo juu, soma historia ya Tanganyika na Zanzibar utaelewa. Pia, usikariri kwamba Muungano wetu lazima ufanane na muungano wa nchi zingine huko. Mwisho, jitahidi kujifunza Kiswahili. Hilo neno "huliza" sio Kiswahili
 

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
3,274
8,009
Huu muungano niwa kimchongo ndio maana kuuliza maswali au kuhoji mambo ya muungano ni kama najisi na kujitakia matatizo,sababu hata wanao utetea muungano ukiwauliza dhima kuu ya muungano ni nini jibu la pekee utaambiwa

"Muungano utalindwa kwa nguvu zote"

Hivyo hushindwa kujenga hoja zenye mashiko kuhusu muungano wa Tanzakiza na Zenjibia zaidi ya kutoa matamshi yenye utata kuhusu uhalali wa muungano na mwisho hutumia vitisho kwa wale wanao hoji kuhusu muungano badala ya kujenga hoja zenye mashiko na Usha wishi kwa wananchi wa pande zote mbili.
 

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
3,274
8,009
Mkuu, mwambie akajifunze kiswahili kwanza ndo aje aulize hayo maswali. Kama hata lugha yenyewe inampiga chenga, hizo hoja zetu atazielewaje kweli?
Mkuu ni vema kujibu hoja aliyo leta kuliko kujifanya mjuaji wa lugha maana hoja isha eleweka cha kushangazaa umeacha kujibu hoja na kumshambulia yeye binafsi hii sio tabia ya GT.

"Akili kubwa hujadili hoja akili ya wastani hujadili matukio akili ya chini kabisa hujadili watu"Socrates
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom