Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Mimi huwa naushangaa sana Muungano..ukiwasikiliza Wazanzibar utapata picha wanaona kwamba wananyonywa na Wabara na ukiwasikiliza Wabara utapata picha wanaona kama wanabeba mzigo wa Wazanzibari. Kiufupi hamna anayeona faida ya kuwa na mwenzake, kinyume chake kila mtu anaona kama " anavutwa shati " na mwenzake. Najiuliza huu Muungano upo kwa faida ya nani?
 
Mimi sina cha kusema lakini kwa Wazanzibar tusidanganyike kuwa tutapiga hatua tukiwa bila muungano but itabidi tufanye kazi ya ziada kupata maendeleo ni hayo 2
 
Mbona kule Tanganyika hajawahi kuchaguliwa Mzanzibar kuwa rais wa Tanzania? Alitaka kuja Dr. Salim A. Salim, kanisa lilimjia juu eti muarabu hafanani na watanganyika!

Heshima yako ustaadh! Hapo umepotea mkuu. Aliemfanyia zengwe sawa ni mkwere na mtandao wake. Sasa kanisa sijui umeliingizaje! Labda kama una chuki binafsi na kanisa.
 
yakhe Respect nyingi kwa SAS. nadhani angekuwa Rais wetu kama alivyotamani baba wa taifa leo hii tusingekua tunadidimia kwa kasi hii inayoendelea saivi.

aliyemuumiza salim ni mkwere akisaidiwa na kina salva rweyemamu. hawakumuumiza huyo tu bali pia mh Sumaye wakimuandika magazetini eti kaweka heka nyingi ughaibuni.

mkwere hiyo haikumtosha akaenda mbele kiasi cha kumyapa nyapa sumaye asisafishiwe njia na polisi akitoka kwake kibaha kwenda dar..sumaye wa watu akaamua kujiendea zake marekani kusoma kuliko kuteswa vile.
 
yakhe Respect nyingi kwa SAS. nadhani angekuwa raisai wetu kama alivyotamani baba wa taifa leo hii tusingekua tunadidimia kwa kasi hii inayoendelea saivi..

aliyemuumiza salim ni mkwere akisaidiwa na kina salva rweyemamu. hawakumuumiza huyo tu bali pia mh Sumaye wakimuandika magazetini eti kaweka hela nyingi ughaibuni...

mkwere hiyo haikumtosha akaenda mbele kiasi cha kumyapa nyapa sumaye asisafishiwe njia na polisi akitoka kwake kibaha kwenda dar..sumaye wa watu akaamua kujiendea zake marekani kusoma kuliko kuteswa vile...
 
Kuna mtu alisema Zanzibar ikijitenga itakuwa kama hong kong ndani ya miaka mitano! NLICHEKA SANA! Mwingine akasema Zanzibar ikijitenga itaanza kuchimba mafuta mara moja na raia wake wataanza kula na kulala kwani mafuta yaliyopo wanaweza kufanya kila mmoja kuwa billionea pasipo kufanya kazi yeyote!
YOTE HAYA HEWALA JAMANI
HEbu jitengeni ili mfanikiwe kama kweli imani yenu ni hiyo lakini angalizo moja kwamba:-
Mtakapojitenga na bara halafu hayo maendeleo yakashindikana, MTAJITENGA NA NANI?
 
I pray to godhead every day that this lopsided union should die in hell.

Mwenye Enzi Allah, Sub Hanna wa Taalah, tutasaidie hili li Muungano livunjike.

Tafadhali livunjeni.
 
Hata sisi hatuuhitaji huo muungano
nendeni zenu, wala hatutawahitaji, kwani mtu akikukataa huna haja ya kumkataa pia.
Lakini mkumbuke kuwa hata kama ktaondoka mtakumbuka tu mazuri mliyokuwa mkiyapata kutoka Tanganyika pamoja na hizo kejeli zenu.
We are tired of u.
 
@Nyandaigobeko,
wala usisumbuke na hao vipofu, wamekali tu udini na lawama zisizokuwa na msingi wowote.
Ninyi wenyewe mnabaguana, sijui mtafika wapi, ngoja tu tuwasubiri mjiitenge ndio mtapata adabu nzuri.
 
abdulahsaf,
Mkuu,

Waliomgeuka SAS walikuwa wazanzibar wenyewe wakisaidiwa na akina wana mtandao kwa msaada wa wazee wa Chama. Walijua fika akiingia SAS itakuwa muendelezo wa siasa za nyerere ambazo zitawabania mipango na plan zao za ufisadi. Hao hao wanafiki ndio walitaka kusiwapo na GNU kwani walijua itasafisha ufisadi wa viongozi wa zanzibar.

Wazanzibar lazima mfahamu huko huko zanzibari kuna mafisadi kibao na hata kama mkijitenga mtakuwa na tatizo zaidi kwani Zanzibar itakuwa ni nchi weak haina jeshi zito sasa kama serikali imewekwa mkononi na mafisadi nani atawakomboa wazanzibari?? Mie naunga hoja ya muungano ila kuwe na serikali tatu. Tanganyika, Zanzibar na Muungano na wazanzibari warudishiwe ukanda wao wa pwani utawasaidia kukwamuka kiuchumi.

Mkijitenga mtasambaratika kwani wenyewe kwa wenyewe mnabaguana kuna wamakunduchi, wandijani, wanyamwezi, wangazija, waoman, wapemba, watumbatu na hampatani hata kidogo ijapokuwa mmechanganyika. Hivyo msijidanganye kuwa mtakuwa salama.
 
Abdulahsaf,

..mimi napendekeza Muungano uvunjwe.

..serikali 3 haziwezi kuondoa manung'uniko ya wa-Tanganyika kwamba Muungano unawanyonya.

..badala yake napendekeza tushirikiane kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

..jinsi EAC inavyoimarika ndivyo ambavyo muungano wa Tanganyika na Zanzibar unavyokuwa redundant.

NB:

..suala la wa-Zenj[jumbe,mwinyi,hamad rashid,fatma maghimbi,mwakanjuki,bakhresa, ...] walioweka makazi huku Tanganyika napendekeza wapewe hadhi ya ukaazi wa kudumu, au ipitishwe sheria ya dual-citizenship.
 
Mdondoaji,

Kwanza niseme mimi nakubaliana na wazo la serikali tatu japo ningependelea zaidi serikali moja. Ninge pendelea zaidi serikali moja kwani hii ita jenga national unity na kuondoa hisia za Uzanzibari na Ubara. Kama unavyo ona sasa eneno lenye serikali yake (Zanzibar) ndiyo ina sisitiza zaidi mambo ya "wao na sisi". Bara kwa vile hakuna serikali basi hamna hisia za sisi Watanganyika bali sisi Watanzania. ANyway swala la serikali moja theoretically it's better ila for practical and political reasons I will settle for three governments.

Ila swala la Zanzibar kurudishiwa ukanda wa pwani napinga kwa nguvu zote. Eneno lile sasa lina julikana kihalali kama sehemu ya Tanzania bara. Japo Burundi na Rwanda zilikua sehemu ya Tanganyika hauwezi kusikia tuki dai maeneo hayo. Na kama nita kumbuka vizuri nilicho kisoma ni kwamba Sultan mwenyewe wa Zanzibar aliliuza eneno hilo kwa wakoloni na wakoloni wakaiweka kama sehemu ya himaya yao. Hivyo Zanzibar haina any legal basis ya kudai eneo hilo.

Kwa vile wao wana insist kwenye Uzanzibar wao sioni kwa nini watengewe kipande cha "Tanganyika". Na pili kama tuki wapa huo ukanda wa pwani ika tokea muungano uka vunjika huo ukanda wa pwani una rudishwa kwetu (kumbuka waliliuza hilo eneo kihalali)? Na kumbuka ukanda wa pwani uliokua wao nadhani ni mpaka Mombasa. Je na huko Mombasa wapewe eneo hilo?
 
..wanaoleta madai ya ukanda wa Pwani ya Tanganyika ni mali ya Zanzibar ni scaremongers tu.

..wanataka tuendelee na UTUMWA wa Watanganyika kuwabeba Wazenj miaka yote.
 
MwanaFalsafa1,
Uhalali unaodai ni upi na kwa sheria zipi za mipaka ya kimataifa. Umezungumzia burudi na rwanda lakini ufahamu Burundi na Rwanda zilikuwa chini ya mjerumani na hivyo walikuwa underthe charter of UN to be in British Protectorate. Sasa niambie Sultani wa Zanzibar alikuwa katika position gani hapo? Na kwanini Waingereza na Wajerumani hawakumshirikisha Sultani wa Zanzibar katika makubaliano yao instead walimnyang'anya kwa ubabe.

Kwanza tupatie evidence kuprove unachokisema otherwise mkuu there is a sufficient reasons and legal grounds hii ngoma ikianzishwa Tanzania Bara, Kenya na Msumbiji watalikosa hilo eneo tupo hichi ni kizazi kengine mkuu zungumza with a little bit of facts Mwanafalsafa.
 
JokaKuu,

Hahaha,
Naona una uhusiano na Gaddafi na Mubarak kuwatisha tisha watu hahaha subiri mkuu vijana wetu wanauchimbua huu muungano utakuja kushangaa wakishakuwa tayari time will tell mkuu.
 
zanziberi,mwataka kujitenga mayakheee
hata leo jitengeniii,maana nyie ni mzgo atiii,mkija huku shule zawashindaaaaa

Sio shule tu, kaibu kila kiitu hao jamaa ni wazembe, hawafanyi kazi
kisha kukaa tu na kupiga umbea wandhani maendeleo yatakuja kwa kupiga soga tu..
eti wandhani muungano ndio tatizo kwao, bila hata kujifikiria kwa sasa zanzibar ni kama nchi huru tu je ni nini walichofanya zaidi ya kubadirisha katiba, wamejaa unafiki tu.
 
MwanaFalsafa1

Naomba unitazame hii paragraph halafu unijibu:

In 1841, Sultan SAYYID SAID of Oman (1804-1856) moved his capital from Muscat to Zanzibar. In 1856, his Sultanate was partitioned, son MAJID inheriting the SULTANATE OF ZANZIBAR.

The Sultanate extended beyond the island of Zanzibar, including the islandof PEMBA further north. The Sultan's suzerainty was recognized along the coast of nearby East Africa, up north to the WITU REGION (modern Kenia).

Zanzibar was a trade center, slaves and ivory being the dominant commodities. The cultivation of CLOVES had been introduced in 1818, and it became the major plantation crop on the island. Cornevin describes mid 19th century Zanzibar as the world's largest market for cloves, ivory and slaves. Zanzibar became the prime outlet of a growing network of caravans which opened up Africa's interior. Imported wares, mainly rifles and ammunition, provided the owners of caravans with the means to establish and expand theur business and base of power.

In 1873 the British Navy compelled Sultan BARGASH to abolish slave trade).

The British have long played a role as advisers to the Sultan of Zanzibar. In 1877, Sultan Bargash, in communication with the Germans, refused a British protectorate; in 1880, Germany's chancellor Bismarck rejected a request by the Sultan of Zanzibar for a German protectorate. In 1886, Britain and Germany, both interested in the acquisition of colonies, agreed on partitioning the mainland territories of the Sultanate, ostensibly to suppress the slave trade the Sultan had nominally abolished and was unable to suppress, technically while respecting the Sultan's sovereignty. Britain would receive British East Africa (Kenya), while Germany would receive German East Africa (Tanzania).

Zanzibar, i.e. the islands of Zanzibar and Pemba, remained independent until 1890.

In 1886, Britain and Germany signed a treaty according to which the territory of the Sultanate of Zanzibar on the African continent was split up between the Germans and the British; the island of Zanzibar itself, with the island of Pemba was to remain independent.

In 1890, Germany and Britain signed another treaty. Germany recognized Zanzibar and Pemba as located within the British sphere of interest, and ceded German claims over WITULAND, BENADIR and UGANDA in exchange for the much smaller and less populated island of HELIGOLAND, located in the North Sea, as well as the CAPRIVI STRIP linking German South West Africa with the Zambezi river.


Mwanafalsafa sasa nionyeshe wapi Sultani aliuza hilo eneo??
 
Back
Top Bottom