Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

I agree and it goes as far as failing to determine whether a party can be part of the Governiment in Zanzibar and the opposition in Mainland!
 
Henge,
Unachoongea hata mimi nilikiafiki tatizo ni wanasiasa mf leo hii ni rais wa Tanzania. Leo Tanzania ikifa, atakuwa Rais wa nchi ipi?
Rais wa Zanzabar ataendelea kuwa Rais wa Zanzibar kwa sababu Zanzibar ipo hapo ndipo wenzetu walipojitambua

Unaona ilivyo kaa vibaya hiyo
UFUMBUZI NI KATIBA MPYA.
 
mgen,
Asante sana kwa mchango wako. Hasa hapo kwenye red. Ukweli unabaki palepale kwamba, Zanzibar wameanza kujipambanua kidogo kidogo na Watanganyika tutakuja kutokwa na tongotongo machoni kila kitu kikiwa tayari. Sasa hivi wanatafuta loop hole ya kujiunga na OIC.
 
Old ManIF,
Asante kwa post yako nzuri. Muungano ni makubaliano ya pande zote mbili. Ni mzuri lakini utaratibu uliotumika wa Kuiua TANGANYIKA na Kubakiza ZANZIBAR halafu ikaliwa Nchi ya JM TANZANIA, hapo kuna walakini. Nazidi kusema ndiyo maana hata wanaJF wengine hawaoni ulazima wa kuchangia post hii, kwani hawaoni tatizo currently lakini je in future what will happen.

Ni haki yetu kuhoji jambo hili. Ni wakati sasa mwafaka wa kuliingiza katika mjadala wa Katiba inayokuja. Lakini je, mfumo wetu wa kisiasa ukoje? Vyama vya upinzani vina nguvu hiyo? Wananchi wenzetu wanaelewa hili?
 
1. Hoja ya Zanzibar ni Nchi au Si nchi ina maslahi kwa WAZANZIBAR lakini kwa Watanganyika ni kuamsha hisia tofauti za kujiuliza maswali mengi. Tanganyika iko wapi??

2. Hoja ya Zanzibar ina Katiba nzuri kiasi gani au la, haituhusu watanganyika. Swali ni je Katiba ya Tanganyika iko wapi??
 
Kabla ya muungano Wazanzibar walikuwa na dola yao kama ilivyokuwa Tanganyika. Wazo la kuwa na muungano lilitoka Tanganyika likaenda Zanzibar na kupokelewa kwa mikono miwili na marehemu Karume. Si wananchi wa Tanganyika wala Znzibar waliotakiwa kutoa maoni ya kuingia au kutoingia katika muungano. Ni hivyo hivyo kuhusiana na sura na muundo wa muungano. Toka mwanzo kulikuwa na masuala waliyoyafanya ya muungano na yasiyo ya muungano. Kadili muda ulivyozidi kwenda masuala menge yaliyokuwa nje ya muungano yalifanywa kuwa ya muungano bila kurekebisha Mkataba wa Muungano ambao kimsingi ulikuwa ndio msingi wa muungano.

Sababu na faida za kuwa na muungano amezizungumzia mwalimu katika maandiko yake mengi. Zipo sababu za kihistoria ambazo kwa mtizamo wa karibu tunaweza kusema zimepitwa na wakati bali kwa mtizamo wa mbali hapana. Suala la usalama wa taifa kwa wakati ule lilikuwa linazungumziwa kwa kuhusishwa na vita baridi. Suala la usalama kwa upande mwingine lilihusishwa na uhusiano wa kihistoria kati ya Zanzibar na dola ya kusulutani ya Omani. Wasi wasi ulikuwa kwamba kama Zanzibar ikiachwa peke yake dola ya Sultani inaweza kuja kwa mlango wa uani. Yote haya yaliunganishwa na geografia ya Zanzibar na Tanganyika. Kwamba kama taifa kubwa adui likichukua Zanzibar kigeografia Tanganyika ingesalimika? Suala la kijegrafia halijabadilika na ubepari bado unakuwa na kubadilisha sura kuendana na hali ya hewa.

Kuna hili suala la umoja. Ni suala ambalo lipo na linazidi kuwa na nguvu. Kihistoria na kibailogia watanganyika na wanzazibar tunahusiana kwa karibu sana. Haitakuwa busara baada ya miaka karibu 50 ya muungano tukafikiria hasara za muungano wakati Rwanda na Burundi wameshaingia katika Shirikisho la EA? Suala ambalo tunaweza kuzungumzia ni kuboresha muungano kwa kuondoa vikwazo vya kisheria na utekelezaji tulivyo navyo. Kubwa zaidi ni kuweka wazi sura na muundo wa muungano. Suala hilo linaweza kufanyika kwa uraisi katika mabadiliko ya katiba yaliyokwisha pata baraka ya dola na vyama vyote vya siasa
 
Rev mi naweza kutunga kitabu juu ya faida za Muungano, lakini siweza hata kujaza katasi moja ya A4 kwa hasara za Muungano:

Lazima ujue zinazoongelewa kama kero za Muungano ni mambo ya kisiasa tu, na mimi sijui kwanini kila tukiongelea muungano tunafinya akili zetu katika eneo la siasa peke yake; Maisha ya Binadamu kwa maana ya maendelo siasa sio kitu muhimu, ingawa sisi kwa ujinga wetu tumeifanya Na.1 na ndio pia Na.2 na 3. Muungano haujapewa nafasi katika nyanja muhimu kuu tatu, yaani : -

  1. Social Development = Maendeleo ya jamii husika, nadhani kuna fursa nyingi sana ukitaka kuzijua onana na wapemba watakwambia wanapata fursa zipi hapa bara ambazo kama wangefinywa zenj wasingezipata
  2. Economic Development = Maendeleo ya kiuchumi, ni kwasababu tumejikita katika siasa peke yake na kujadili madhara ya Muungano na faida zake kwa kuangali Nyimbo za taifa, vyeo vya viongozi, nani atapata cheo gani nk, ndio maana tumekuwa vipofu kuangalia fursa za kiuchumi katika ardhi hizi mbili, tumeshindwa kuwekeza viwanda vikubwa vya kusindika samaki zenj na kuuza Bara, afrika (Kongo, Burundi, Rwanda Nk) na kumfanya mzanzi bar kuishi kwa tende-alwakutoka Uarabuni kama tungali watumwa.
  3. Tourism na Ecology, tukiunganisha vyema utalii uliopo Zenj na bara kulikuwa hakuna haja ya mtaali kuteremka Nairobi ndipo aje ngorongoro. Lakini kuna wafanyabiashara wengi wanafanyabiashara zenj za Hotel nk Lakini hata hii bado inaathiriwa sana na siasa watu wanadai faida za kisiasa zaidi!!!

Mi nasema faida ya Muungano ni lukuki tuache siasa tuwekeze katika hayo mambo matatu ndio tutajua tutakapo na tuendapo.
 
kwa wapemba/waunguja wao faida kibao tuu. si mnawaona bungeni kwenye ma wizara ardhi yetu ya tanganyika wanapewa wanajenga huku nk lakini sie wa bara mbona hatupewi nyadhifa huko kwao ardhi sijui km utapewa. mie naona sisi tunawabeba sana hawa wazenji. hakuna faida yoyote kwetu sie wa bara
 
Rev. Kishosha,

Ukiona watu wanajikanyaga kujibu swali rahisi kama hilo ujue limeshakuwa swali gumu tayari.
Kwa mwananchi wa kawaida hasa wa Tanganyika naweza kusema hakuna faida za muungano mbali na kudumisha undugu baina yetu.
Waunguja/wapemba wanafaidi zaidi matunda ya muunga ingawa hawaridhiki bado. Wazanzibar wanapata faida zote za kisiasa, kiuchumi, kijamii na utamaduni.

Binafsi sipendi tutengane lakini ningependelea tuwe na serikali moja kama hilo ni gumu basi iwepo serikali ya Tanganyika pia.
 
Zanzibar ni wakoloni wa tanganyika. Hawana faida yoyote na sisi zaidi ya kutufanyia unyonyaji mchana kweupe. Muungano uvunjwe leo kila nchi ihangaike kivyake.
 
Chimunguru,
Nyazifa wanapewa katika Wizara zinazohusiana na mambo ya muungano ambazo ofisi zake zote ziko huku bara. Sisi hatuwezi kupewa nyazifa katika Wizara za Zanzibar kwa sababu hamna hata moja ambayo ni ya muungano.

Wapo watanzania bara wanaomiliki ardhi na biashara Zanzibar. Wao wanaweza kuonekana wengi huku na sisi wachache kule kwa sababu Zanzibar yenyewe ni nchi ndogo.
 
RealMan,
Hamna mtu anayejikangaga kujibu swali lako labda majibu yanayotolewa ni tofauti na wewe ulivyotaka yawe. Kama ulivyo wewe na mimi pamoja na wengine wanaoniunga mkono ni wananchi wa kawaida labda pawepo na tafsiri tofauti ya nani ana sifa ya kuwa mwananchi ya kawaida. Hapajawahi kupigwa kura ya wananchi wa kawaida na wengi wakasema muungano hauna faida. Hata katika Tume zote zilizowahi kuundwa kuzungumzia masuala ya katiba wengi walionesha wanataka muungano uwepo lakini wakashauri mabadiliko kuondoa mapungufu.

Kuwepo au kutokuwepo serikali ya Tanganyika sio tatizo la Wazanzibar na wala hamna Mzanzibar anayepinga. Suala ni utashi wa watu. Kama watu wengi watasema tunataka serikali ya Tanganyika ndani ya muungano itawezekana. Bahati nzuri mjadala wa katiba mpya bado mbichi ukiwa na baraka za dola na vyama vyote vya siasa
 
@hmethod,

Ni lini Zanzibar walianza kuwa wakoloni wa Tanganyika mpaka leo karibu miaka 50 ya muungano unataka muungano uvunjwe? Ni mamlaka gani Wazanzibar waliyonayo dhidi ya watanganyika yanayowapa sifa ya kuwa wakoloni? Kama ni Wizara ya Mambo ya Nje ipo katika serikali ya Tanganyika kwa niaba ya serikali ya Muungano.

Ni hivyo hivyo kwa Wizara nyingine za Muungano. Toka muungano uanze miaka karibu 50 iliyopita maraisi toka Zanzibar wameshatawala kwa kipindi cha miaka kumi tu ikiwa karibu asilimia ishirini ya umri wa muungano. Hapa kama kungekuwa na uhusiano wa mkoloni na mkoloni ni nani angestahili kuitwa mkoloni?
 
Muungano una faida zake na nyingi zimekwishapatikana na kuonekana

Muungano una matatizo yake mengine yanajulikana na yanawezekana kumalizwa

Muungano upelekwa kwa wenye nchi, mkataba uchunguzwe upya kwa maslahi ya pande mbili

wakati ni huu,

Kwa habari ya Faida za Muungano,Wazanzibar ndiyo wanao nufaika na muungano kwa zaidi asilimia 100,kiuchumi,kisiasa na Kijamii.
 
Sisi wa bara hatutaki Muungano. Kwanini katiba ya Zanzibar inasema Nchi? Wenyewe hawataki. Nasi hatutaki. Wanaupigia debe ni wabunge wa Zanzibar akina hamad Rashid na majina yao bandia ndo wanaupigia debe. Ama wapemba wanaofaidi huku bara. Vinginevyo Tusidanganyane muungano ni hasara kwa bara.
 
Naona watanganyika mnajikanyaga tu kuhusu huu muungano kawaza wazanzibar hawautaki nyinyi ndio mnaulazimisha. Kwawale watanganyika wenyeakili wanajua faida waipatayo kktk muungano na jinsi wanavyoikandamiza znz. Ukiona mtanganyika anapiga kelele kuhusu muungana eti unahasara kwa tanganyika basi ujue huyo hajui alifanyalo na ni mpiga debe tu.

Hakuna hata mzazibari mmoja anotaka mfumo wa serekali mbili ulowekwa na tanganyika ili kuimeza zanziba na kuwa koloni la tanganyika, wazanzibari 99% wanataka kuwepo na serekali 3 yani ya tanganyika, zanzibar na ile ya muungano. Na kula upande uwe na maamuzi yake bila kuingiliwa na upande mwengine. Na kwenye hiyo serikali ya muungano kila upande ujue unachangia %? Za faida na hasara, au kama vipi uvunjwe kisha wote zanzibar na tanganyika zijiunge na jumuia ya afrika mashariki bila mmja kumtegemea mwezake.
 
Arafat,
kama ni swala la muungano Tanganyikia na visiwani wanatakiwa wote wanufaike-naona umeeleza jinsi Wapemba wanavyonufaika huku tanganyika-inawezekana watanganyika hawanufaiki na kitu visiwani
kuliko huu muungano uwabebe Wazanzibari-ni bora uvunjwe hata leo
 
Heshima kwako Rev Kishoka,

Muungano una fadia zaid kwa Wazanzibar kuliko Watanzania bara.

Zanzibar waliungana na Tanzania bara kwaajili ya usalama wao kipindi cha vita baridi.Mazingira ya wakati huu siasa za vita baridi hazipo tena na pengine ndiyo maana tunashuhudia wazanzibar wakitaka sauti zaidi kwa kutambua kitisho cha miaka ya sitini na sabini hakipo tena.

Muungano wa Tanzania bara yenye idadi ya watu 44 milioni na eneo lenye ukubwa wa 945,087 sq km dhidi ya Zanzibar yenye watu 1 milioni na ukubwa wa eneo 2,461 sq km tu ni baadhi ya chamgamoto kubwa zinazosumbua muungano.Ukizingatia ukubwa wa Tanzania bara na idadi ya watu wake ukilinganisha na ukubwa wa Zanzibar na idadi ya watu wake tayari mgongano wa kimaslahi [kisiasa,kiuchumi na kijamii] ni sababu tosha za kuyumbisha muungano.

Muundo wa muungano wa serekali mbili uliandaliwa na Mwl J Nyerere kwaajili ya kuaccomaodate kanchi kadogo sana "Zanzibar" [hakana ukubwa wa mkoa wa Tanga au Mbeya] ndani ya muungano wa nchi mbili moja kubwa "Tanzania bara".Kinachotokea sasa ni nchi moja ndogo kutaka usawa na nchi moja kubwa sana kugawana madaraka ya kisiasa na kiuchumi.Zanzibar ina wabunge zaidi ya sabini [70] ndani ya bunge la JMT, mkoa wa Dar es Salaam hakuna zaidi ya wabunge kumi [10] lakini ina idadi ya watu zaidi ya 3 milioni amabayo ni idadi ya watu mara tau zaidi ya Zanzibar.Mkuu hiki nikipengele kimoja tu, ukijaribu kuangalia vipengele vingine utabaki kinywa wazi ni kwanini tulazimishe muungano.

Mkuu wazanzibar wanatumia fursa kubwa za kiuchumi zinazopatikana Tanzania bara.Ushahidi uko wazi kabisa siku ikatokea wapemba wakaambiwa wafungashe warejee kwao hakika wangewalaumu sana wapinga muungano.Zanzibar haina rasilimali nyingi kama Tanzania bara bado wanaota mafuta amabyo mpaka sasa hakuna dalili za kuwepo mafuta ya kutosha kwaajili ya biashara.

Zanzibar haichagii uendeshaji wa serekali ya JMT,Mahakama ya rufaa na Bunge la JMT.Utashangaa wazanzibar wanadai nyongeza ya mgao wa mapato ya misaada lakini wanasahau hawachangii senti tano ya uendeshaji wa serekali ya JMT.


Ipo hasara moja kubwa sana iwapo Tanzania itaamua kuvunja muungano leo hii au siku za usoni,Ni rahisi sana magaidi kujipenyeza Zanzibar isoyopenda kufanya kazi ya kuwakomboa wananchi wake kiuchumi na badala yake inajikita kuota uwepo wa mafuta kwenye pwani yake.Tanzania itajikuta ikipokea wakimbizi wa kizanzibar maelfu kwa malaki kama ilivyotokea Burundi na Rwanda.Zanzibar wakijitenga leo tujiandae kukaa na Somalia nyingine kilometa chache kutoka Dar es Salaam na Tanga.
 
Ngongo,

Mkuu Ngongo, heshima mbele, hili bandiko limeshiba ukweli na uhalisia. Asante sana umenichosha ama kunifurahisha hapo kwenye red utanitendea haki pamoja na wengine wanaofuatilia mada hii ukitoa angalau ufafanuzi kidogo tu kuhusu sentensi hii.
 
Back
Top Bottom