Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Mbona dogo hilo ,ni rahisi unapoulizwa unatoka nchi gani ukasema ninatoka Tanzania na ikawa umemaliza na uliemjibu ikawa ameridhika ingawa hakuna Nchi inayoitwa Tanzania.Mwiba,
Kwanza napenda nikushukuru kwa uchambuzi wako yakinifu, ila mimi nilikuwa na swali moja tuu . Tafadhali nakuomba unipe maana( definition ) ya neno nchi .
Ila ikiwa suala hilo hilo umeulizwa na msomi anefahamu Jiografia atakuuliza Tanzania bara(MainLand) au Zanzibar (Visiwani ) na ninaposema hakuna nchi inayoitwa Tanzania ninamaanisha Nchi iliyopo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Tanzania ni kifupi ila sijui kama unafahamu kirefu chake ndio nikasema hakuna kitu hicho Nchi iitwayo Tanzania labda kwa vichwa mchungu.
Natumai umefarijika la unataka maana kwa kilugha basi ni eneo la ardhi na zamani kulikuwa na Sukuma land matebele Land na nyenginezo hizo zikimaanisha eneo la ardhi la jamii ya watu fulani ,unajua ukitazama ramani za zamani sana hutaweza kuiona Tanganyika ila Zanzibar ilikuwepo ,Tanganyika nafikiri ilianza kuitwa hivyo kati ya miaka aliyozaliwa Nyerere.
Ila sasa wameongezea ili Nchi iwe Nchi sijui uwe na jeshi,uwe na mahakama,uwe na chombo cha kutunga sheria na mambo kibao ambayo kimsingi hayahitajiki ili uweze kuwa Nchi kwani hayo yote ni mambu ya kisasa na kisiasa ,mgawanyiko wa Urusi nchi zilizojitenga hazikuwa na mambo hayo tena sio kuwepo japo moja lakini hayakuwa na hata kipande ya mambo ambayo unataka yakamilike ili uweze kuwa nchi ,kilichowasaidia ni kule kule kwa zamani kuitwa Sukuma Land au Matebele Land na leo hii nchi hizo zilizojimegua kutoka Russia zimeweza kutengeneza mambu ya kisasa ili ziweze kutambuliwa. Zanzibar inayo mambo kibao ambayo hawa wa urusi hawakuwa nayo sasa iweje wazuke wazushi waseme Zanzibar sio Nchi kama si dharau ni kitu gani.Au mpaka iwepo Tanganyika ndio mjue kama Zanzibar ni nchi ,yaani hata kudai kurudi kwa Tanganyika huru mnataka wawasemee WaZanzibari.