Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?

Sam

JF-Expert Member
Jun 6, 2006
415
88
Nimevumilia vya kutosha nikidhani kama kuna mtu anayekerwa na fumbuzi wa matatizo ya muungano yaliyotolea kwenye kikao cha pamoja kati ya Mh. Lowassa na Mh. Nahodha.

Kitu kinachonitisha ni kwamba yale mambo waliowaamulia wananchi yatapelekwa bungeni october kwa ajili ya "constitutional reforms".

Kwa upande wangu sikubaliana na ufumbuzi waliofikia kwa 100%
Check this out:

1) mineral and oil exploration be co-opted into the national debate on the future of the political federation.

-debate is good but mineral and oil exploration should not be political.

2)Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) should have an equal number of representatives from either side.

-Equal number kwa vigezo gani? Idadi ya watu? Tuelezene mlivyokuja na hiyo soultion equal number of people.

3)consultant on the distribution of wealth generated through mining and oil extraction be hired to advise the Union government on how it can be shared equitably.

-Please kama ni hivyo na huo muungano hatuutaki. For what?

4)It was decided that 50 per cent of the income would be used to finance the operations of the authority and the other 50 per cent be distributed on the basis of 60 per cent for the Mainland and 40 per cent for Zanzibar.

-Hivi hizo hesabu mnafanyaje? How did you come up with 60%, ardhi, watu,?????

Najua watanzania hawataki kuongelea muungano wakiogopa mizimu ya Mwalimu. Kwa upande wangu kuna mambo mawili tu hapa ambayo yanaweza kuleta ufumbuzi wa kudumu kwanza kuuvunja muungana na Zanzibar ikawa nchi kama ilivyo Kenya na tutaendelea kushirikian nao kama tunavyoshirikiana na Kenya, au Zanzibar uwe mkoa. zanzibar kuna watu wasiozidi 3 mil wakati mkoa wa Dar tu una watu 4 mil. Hapo utajiuliza ni kivitu tugawane nusu kwa nusu?

Kama watu hamtaki kuongela hili sual basi mwezi October linaingia kwenye katiba.

Mkataba wa makubaliano ya kuanzisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukisainiwa mwaka 1964.

Mkataba wenyewe (uliosainiwa) umeambatanishwa kama attachment.
 

Attachments

  • Muungano_1964.zip
    25.5 KB · Views: 1,323
Last edited by a moderator:
Hivi nyie watu humu haya niliyoandika ni upuuzi ama nini? Watanzania tumezoea mpaka kitu kitendeke ndiyo tuanze kulalamika. Haya mambo yataingizwa kwenye katiba ya muungano. Hivi ni kweli watu humu ndani mnayaunga mkono au hamna la kusema. Najua Mkandara unayaunga mkono how about the rest?
 
Hili suala hata mimi niliwahi kusema si suala la Lowassa na Vuai!

Hivi CCM na viongozi wake ni lini watakubaliana kuwa watanzania wana mawazo nao wanaweza kuchangia?

Kuhusu muungano ninakubaliana na wewe ni vema tuuvunje kwanza au iundwe serikali moja hata ukisoma kitabu cha Mwalimu uongozi na ... alishauri serikali moja kwa sababu alisema muundo wa muungano ni serilaki mbili kuelekea serkali moja baadaye. Lakini zanzibar cini ya CUF na CCM wenye we huko wanataka serikali tatu ili waendelee kutunyonya zaidi!!


Sawa haya ya (Lowaasa na Vuai )yakipelekwa bungeni yakapitishwa yatakuwa mabaya zaidi kuliko hata ya Nyerere na Karume . Hawa watu wa bara wataumia zaidi lakini hao hao wa bara wamekuwa kama

walinyweshwa dawa kuhuu muungano hawataki kabisa kuungolea!!!


Hapa ndipo huwa ninakubaliana na Mtikila!
 
Sam,

Inasikitisha sana kusoma huo mswada unaotegemewa kufanywa sheria katika siku za usoni , swali langu mimi ni moja tuu Watanzania ni nani aliyetuloga ? Kwa nini atufikirii kabla ya kufanya maamuzi ?

Kweli , kuna haja ya kuwa rocket scientist kujua ya kuwa huo mswada ni ujinga na ni kuwatukana wazalendo ? Yaani mapato ya madini yagawanywe katika uwiano wa 60% bara na 40 % zanzibar ....Ni vigezo gani wametumia kupata hizi figure ? kwanza zanzibar ina population ya watu wangapi .

Sam , naona utakuwa unaumiza kichwa tuu . Hawa viongozi awajali watu wa kawaida wanachodai ni masilahi yao binafsi ! siasa za bongo ni upotevu wa muda kwani wananchi wako so dormant na mara nyingi wanaishia kulalamika tuu .kikifika kipindi cha uchaguzi wanapitishiwa mswada wa kuwapa pilau " wanahongwa pilau " then wanawachagua kwa asilimia 80%.
 
sam,

si kweli kwamba watu wanapenda hayo makubaliano kati ya EL na SVN.

Hapa wengi wetu tumeshikwa na butwaa, maana pa kusemea hatuna zaidi ya hapa TEF.

Hii ni chokochoko ambayo nahisi Wabara wakishtuka na kupiga kelele tu Zenji nao watadai kwa NGUVU ZOTE kuwa VUNJA MUUNGANO, kwani wanajua (wazenji) fika kuwa wao ndio wanafaidika zaidi na hayo makubaliano, tena kuliko hata ilivyokuwa mwanzo. Na Wazanzibari wao wanatumia UDHAIFU wa Wabara (wapenda Muungano) KUFAIDIKA. In short kama mifano ya Mh Mkandara, Wabara sasa tunampenda sana MWALI na inabidi MLIPE MAHARI ZAIDI, KAMA HAMTAKI, MWALI NAYE ANASEMA BASI.

Whether we like it or not, this is very serious issue na very sensitive

sam, maswali yako ni ya msingi kabisa, sasa basi

1.Ni nani atakayejitokeza kwa nguvu zote na kusikika KUPINGA HAYO MAKUBALIANO beyond hapa TEF?
2.Hizi ni kampeni za kisiasa ndani ya CCM, naanza kuamini kuwa EL anaandaliwa kuchukua nafasi ya JM. hivyo basi hiyo ni kampeni ya EL kupata kura toka CCM ZNZ
3.Inabidi tuendelee kupiga kelele, ili uelekeo wa maamuzi ya Muungano uwe zaidi kutokea kwa WANANCHI WA PANDE ZOTE na si watu wawili
 
Sam,
Acha uhuni weee! sema umetaka kusikia comment zangu kuhusu swala hili.
Kumbuka mshikaji mimi hutazama shilingi kwa vigezo vya reality kisha correct way ya kumaliza tatizo bila kuingia mkenge. What's right or wrong haiwezi kusaidia kitu kwani dunia hii haina sheria za kanisani wala msikitini.

Kwanza kabisa lazima tukubali kwamba nchi yetu tunatawaliwa. Hilo nawaunga mkono sana Chadema, na Kama alivyodai Mbowe tunahitaji viongozi wa kutuongoza kulinda uhuru wetu na kutupeleka mbele kufikia kujitegemea... Hizi ni nyayo za Nyerere ambazo hata mimi nazikubali.

Swala la Muungano ni zito sana. Sipendi kuona muungano umevunjika kwa sababu ya mirathi na kubwa zaidi - eti sababu Zanzibar ni mtoto wa nje.

Nadhani Zanzibar wana kila haki ya mirathi hiyo ndani ya muungano lakini sio kwa kipimo ambacho kimetumika. Pili, sikubaliani na mirathi yeyote iliyokuwa sawa ikiwa mtoto huyu bado anadai mirathi toka kwa baba yake mzazi (Uchumi wa serikali ya Zanzibar), hali Bara hatuna serikali ndogo isipokuwa Federal. Hapa zilitakiwa serikali tatu kuweka mgao na serikali ndogo zote ziwe na mapato yake yatakayokuwa yakilipa kodi kwa serikali kuu.

Utoaji wa fedha zaidi kwa seikali moja Utakubalika tu pale penye miradi ya kitaifa. Mathlan, Ujenzi kwa uwanja wa ndege wa kimataifa Zanzibar.

Tatu na kibaya zaidi sikubaliani na hatua hii kwa sababu Zanzibar wanaamini kabisa ni nchi inayohitaji kujitenga. kwa hiyo hatua ya kwanza ni kufanyika kwa referendum ifahamike wazi wananchi wanapendekeza kitu gani. Wakichagua kijitenga hakuna haja ya muswada huu kupelekwa bungeni. Wakichagua kuendeleza Muungano basi, muswada huu ufikishwe bungeni pamoja na ule utakao unda serikali ya tatu bara. Na sheria ipitishwe swala hili la muungano halitazungumziwa tena na jina Wazanzibar lifutike ktk kamusi... sote Watanzania.

Sam,
Nilikaa kimya kwa sababu nyingine ya reality!

Toka lini sisi wananchi tukawa na sauti ktk maamuzi ya mikataba?.. Hiyo Gas, Petrol, Madini na mengineyo tunapokea ruzuku tu na hakuna kati yetu anayefahamu mikataba hii.

Unajua hivi majuzi nilishangaa sana nilipoona kuwa mwaka 2003 Songas imeuzwa kwa Mu-ingereza toka Kwa Mu-Australia baada ya miaka mitano ya uuzalishaji.... mmhhh! kuna harufu mbaya hapa lakini ukweli umesimama Songos imeuzwa na leo hii soko lake limehamia Uingereza toka Ausie sio DSE.

Umesikia mwenyewe walivyomsimamisha Zitto kuhusu mikataba kwahiyo hata hili halina maana kwani bungeni wamejaa CCM. Upinzani mkubwa bado upo Zanzibar na ndio pekee wanaoweza kuwaharibia jina kwa sababu ya KULA.
 
Mzee Mkandara,
Mimi naamini hakuna kitu kitachotutengenisha kati yenu na Zanzibar kijamii, sisi ni wamoja na tunashirikiana vizuri sana kijamii. Muungano wa kiuchumi na kisiasa unaturudisha nyuma sana kimaendeleo. Ni kitu ambacho hakiingii akilini kwa nini Zanzibar iwe na serikali yake ndani yamuungano wakati Dar es Salaam ambayo wakati wake ni mara mbili ya wakazi wa visiwani na bado wanataka wachukua 40% for what. Kama hawataki Zanzibar uwe mkoa basi muungano wa kisisa na uchumi ufe, ni gharama kubwa kwa serikali ya Muungano.
 
Sam,
Unajua Wamarekani walivamia Hawaii, wakamwua mfalme wake, wakaiburuza katika USA, mambo kwisha. Hakuna hata siku moja unasikia Hawaii wanapiga kelele hiki au kile. Mwalimu alikuwa mwuungana sana. Angekuwa Nkrumah, Zanzibar hivi sasa ingekuwa mkoa tu. Hakuna kelele. Chagueni gavana wenu, mbunge wenu lakini katika Federal govenment kura yenu inalingana na idadi ya watu wenu. We should have done the same.
 
Sam,

Maneno ya Jasusi ndiyo yangefunga kazi, lakini ndo...YANGE!

Zanzibar hatukumzaa sisi ni nchi ambayo inatakiwa kutambulika ndani ya muungano. Swala la Siasa lazima liongozane na Uchumi ktk muungano wowote wa nchi mbili, hii ni ndoa na huwezi kuleta mpango wa kienyeji. Tumeisha kula Yamin na haivunjiki bila kuwekwa ubani. Na ubani wenyewe ndio hiyo referendum. Kama bwana tunaweza kuwa na matumizi zaidi lakini haiwezekani tuseme hawana sauti kabisa. Tumefunga ndoa wenyewe tena kanisani ama msikitini, kilichotakiwa kilikuwa kuvuta ndani tu huku wake wa ndoa (mikoa) wakiwa na madaraka yao ya kiuchumi toka enzi zile za madaraka mikoani. Kwa hiyo Kisiasa ingejulikana tofauti na nje ya madaraka ya kiuchumi.

Nadhani swala hapa ni njia gani bora ktk muungano huu inapofikia kugawana mali. Kama ulivyosema asilimia 40.... toka wapi?.. hatuna serikali tatu. Mshikaji CCM sasa wanachemsha bara! Kama wanataka JM aonekane bingwa wa utawala basi hii ndiyo kaburi lao na kusema kweli nimepata habari za ndani kwamba wanaodai hasa kuwepo na wagombea binafsi wanatoka ndani ya CCM, hao mnaowasikia nje ni watu waliopandikizwa tu. Sii kazi mkasikia uchaguzi Ujao JM, Salim na Sumaye wanapigania kiti nje ya CCM kama wagombea binafsi. Kazi ipo na cheche za moto wanazianzisha wao wenyewe CCM. Habari hii ya 60 kwa 40 haikubaliki katu na vumbi litatoka bara.....Hiyo mikataba wananchi wapo radhi kuifumbia macho kwa sababu hawana elimu ya kufahamu hiyo mikataba lakini Mpango wa bara na visiwani hili swala jingine kabisa!
 
Mkandara,
Aaah! ndiyo maana Sumaye anakwenda Harvard, ili arejee na digrii ya utawala bora akijiweka sawa kwa 2010 au 2015? Kweli ndani ya CCM kuna mengi.
 
Muungano ni faraja kwa Z'bar - Mbunge

Na Esther Mvungi, Dodoma

MBUNGE wa Koani, Haroub Said Masoud (CCM), ametetea Muungano wa Tanzania na kusema Wazanzibari wananufaika nao.

Haroub aliyasema hayo jana alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka 2006/07 yaliyowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Profesa Mark Mwandosya.

Alishauri mapungufu yaliyopo yajadiliwe na wananchi, wakiwemo wao wabunge, na si kusema iundwe serikali moja au kwamba watu kutoka Bara wanataka kuingia katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Haroub alisema kasoro zilizopo katika Muungano ni vizuri kukaa na kuzirekebisha na kwamba kuwepo kwa wabunge Dodoma inaonyesha kuwa Muungano ni bora.

Alisema anakumbuka kwamba alifika Tanzania Bara kwa mara ya kwanza mwaka 1965 alipokwenda kushiriki mashindano ya riadha mjini Moshi.

Pia alikumbusha kwamba zamani Zanzibar ilikuwa ikinunua chakula kutoka Misri, lakini leo inapata chakula Tanzania Bara, tena si kwa fedha za kigeni.

"Ukitaka mchele kutoka Mbeya unachofanya ni kuagiza tu, ukitaka viazi unapata," alisema Haroub na kwamba hayo ni matunda ya Muungano.

Akitoa mfano wa kinyonga anayekwenda mbele hatua mbili na kurudi nyuma hatua moja, alisema binadamu anapaswa kujifunza kutoka kwake na kwamba Muungano unapaswa kuangaliwa "kwa kuzingatia tulikotoka na tulipo sasa".

Alisema tangu miaka ya 1800 walikuwapo watu toka Bara wakiishi Zanzibar na si sahihi kusema kuwa watu wa Bara si wakazi wa Visiwani Pemba na Unguja.

Akichangia hotuba hiyo Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, ambaye Spika Samuel Sitta, alimpa nafasi ya kuchangia wa kwanza kwa kuwa jana alikuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa (ana miaka 50), alisema mambo ya afya na elimu yaongezwe kwenye masuala ya Muungano.

Kwa upande wake, Mbunge wa Chalinze, Ramadhani Maneno (CCM) akiwasilisha maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, alisema licha ya dosari zilizopo, wananchi wanaupenda Muungano na kutoa ushauri kuwa mgawo wa fedha za msamaha wa madeni ni jambo linalopaswa kufanyiwa kazi zaidi.

Kambi ya upinzani, ikitoa maoni yake yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Omar Juma (CUF), ilisema utatuzi wa kero za Muungano ufanywe kama sehemu ya mapitio ya Katiba ya Tanzania.

Alisema uboreshaji wa Muungano uzingatie hali ya baadaye ya Tanzania katika ushirikiano wa kimataifa kama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
 
SMZ yaigomea Serikali ya Muungano kuhusu mikopo

*Yataka wanaopata daraja la tatu nao wafaidike
*Yasema sheria ya sasa inakosesha fursa wengi

Source: Tanzania Daima News Paper

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) hatimaye imeibuka na kutoa msimamo juu ya wanafunzi wanaonufaika na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini, ikipinga msimamo uliotangazwa na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla aliyeungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete siku chache baadaye akiwa Mwanza.

Wakati Serikali ya Muungano imeweka viwango vya daraja la kwanza na la pili kwa wanawake kuwa ndio sifa ya kunufaika na mfuko huo, SMZ insema utaratibu huo unapaswa kuangaliwa upya.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman amewaeleza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi msimamo wa wizara yake ni kuona wanafunzi wenye sifa za daraja la tatu pia wananufaika na mfuko huo.

Alisema kwamba Serikali ya Zanzibar tayari imechukua hatua ya kuwasiliana na Serikali ya Muungano kuangalia utaratibu utakaowawezesha vijana waliopata daraja la tatu kujiunga na vyuo vikuu nchini.

Alisema hatua hiyo lazima izingatiwe kwa vile ndiyo njia pekee ya kuwasaidia vijana ili waweze kuingia katika soko la ajira.

"Tumeshawasiliana na Serikali ya Muungano kwa kuwaandikia barua na hawa vijana wa daraja la tatu wafikiriwe katika kunufaika na mkopo huo, kama wana sifa," alisema.

Alisema ni jambo la faraja kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete ameongeza fedha katika kuinua uwezo wa mfuko huo.

Kauli hiyo ya SMZ imekuja huku wanafunzi wengi Zanzibar waliopata daraja la tatu katika masomo ya kidato cha sita wakiwa wameshindwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kutokana na ugumu wa masharti ya Mfuko wa Bodi ya Elimu ya Juu.

Waziri Haroun alisimama na kulazimika kutoa ufafanuzi huo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini Zanzibar, baada ya wajumbe wa Baraza kuhoji masharti yaliyowekwa katika kunufaika na mfuko huo.

Naye Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Dk. Mwinyihaji Makame alisema Serikali ya Zanzibar imeshindwa kuingiza fedha katika mfuko wake wa elimu ya juu Zanzibar kama ilivyotarajiwa kutokana na uhaba wa fedha.

Alisema kwamba ni kweli Mfuko wa Elimu ya Juu Zanzibar ulitarajia kutumia sh milioni 400, lakini kiwango hicho hakikuingizwa katika bajeti, kama kilivyoombwa kutokana na uhaba wa fedha serikalini.

Waziri Mwinyihaji alisema serikali inajiandaa kuweka mikakati ya ukusanyaji mapato, ili kuhakikisha mfuko huo unapatiwa fedha za kutosha.

Hata hivyo, alisema wanafunzi wengi kutoka Zanzibar waliweza kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali na kupunguza ukubwa wa tatizo la kupata mikopo kutoka Bodi ya Elimu ya Juu nchini.

Wakati huohuo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekiri kuna madaktari wamekuwa wakiondoka na kwenda kujiunga na mashirika ya kimataifa, ili kupata maslahi zaidi.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Shwana Buheti Hassan amesema hivi karibuni madaktari wawili walitimkia Botswana na Ethiopia na kuomba likizo bila malipo.

Alisema serikali imeamua kuweka mkakati wa kuimarisha maslahi ya madaktari, ikiwamo kuangalia viwango vya mishahara na marupurupu pamoja na huduma nyingine ikiwamo za usafiri.

Mapema, Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Ali Abdallah Ali alisema hivi sasa kuna wimbi kubwa la madaktari bingwa kuondoka Zanzibar, wakati Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja inakabiliwa na uhaba mkubwa wa madaktari.

Aliitaka serikali ieleze ina mikakati gani ya kupunguza ukubwa wa tatizo ikiwamo kuboresha maslahi ya wafanyakazi hao wa sekta ya afya.

Madaktari wengi Zanzibar wanalalamika kwamba wanafanya kazi katika mazingira duni, ikiwamo ukosefu wa vifaa, usafiri, makazi na kulipa viwango vidogo vya mishahara chini ya sh 250,000, kinyume na viwango wanavyolipwa madaktari wa nchi za Kusini mwa Afrika, SADC.
 
Hii thread imekuwa inspired from MMKJJ ya Tanzania kujiunga na OIC na zinginezo zinazohusu hali ya kisiasa huko Visiwani

Juzi ilipostiwa document ambayo ni 3 page MS WORD DOCUMENT amabyo mimi sinamini kuwa ni genuine kwa sababu iko so simple na haina mambo mbali mbali kama GET OUT CLAUSE

Maswali:

Kwa nini hii document inafichwa namna hii?

kama inamambo ya muhumu yanayohusu maisha ya wanadamu zaidi ya Milioni moja huko Zanzibar kwa nini watu washitaki ndio inaonekana?

Je Muungano unaweza ukawa ILLEGAL?

Na kama ni LEGAL ni based on what?

Je hii legality inaweza ikawa kwa sababu zipi?

Na kwanini mnaogopa kuliongelea hili?

Jamani huu mjadala ni kuhusu MKATABA WA MUUNGANO na sio MATATIZO ya Muungano kwani yako mengi na yanahitaji separate TOPIC
 
MABADILIKO ya baadhi ya mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki yametokana na mawaziri hao kushindwa kufanya kazi kwa kasi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Sema Usikike’ kinachorushwa na televisheni ya ITV.

"Mabadiliko hayo ninaweza kusema yametokana na baadhi ya viongozi kushindwa kufanya kazi. Mfano, bado kuna kero zinazowasumbua wananchi kwa kipindi cha miezi kumi, lakini hazijapatiwa ufumbuzi, hivyo anahofia imani kwa wananchi, kuwa serikali itawaletea maisha bora itapungua," alisema.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni matatizo ya umeme, maji, njaa na ajira.

"Baada ya matatizo kuendelea kuwa ni kero kwa wananchi, tulitegemea kuona uwajibikaji kwa viongozi husika, kwani kipindi cha miezi kumi kinatosha kutatua matatizo, lakini wameonekana kushindwa kwenda na kasi, ingetakiwa kuwajibishwa, si kuwapangua," alisema.

Dk. Mvungi pia alidai kuwa Rais aliwateua mawaziri hao bila kuangalia taaluma zao.
 
Hali ya kisiasa Zanzibar: Bomu linalosubiri kulipuka

Na Salma Said, Zanzibar

HIVI karibuni, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad alizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Mtoni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kutoa tathimini yake juu ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, aliyeapishwa Novemba 2 mwaka jana baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuwa ndiye mshindi wa kiti hicho kufuatia matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 30, 2005.

Katika tathmini yake, Maalim Seif alilenga kuzungumzia mambo mawili makuu: Hali ya kisiasa ilivyo katika visiwa vya Unguja na Pemba na pili hali halisi ya uchumi wa Zanzibar.

Alianza na hali tata ya kisiasa ilivyo akiishabihisha na bomu lililotegwa likisubiri kuripuka wakati wowote kutokana na wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba kuchoshwa na migogoro isiyokwisha ambayo kwa maoni yake, anaamini inachochewa na wanasiasa walafi.

Amekiri kuwepo kwa mpasuko wa kisiasa ambao unavitafuna visiwa viwili hivi huku akitahadharisha kwamba iwapo mpasuko huo hautatafutiwa ufumbuzi wa haraka Zanzibar inaweza kupata maafa makubwa.

Huku akiunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa nyakati tofauti ya kuwaahidi Watanzania kwamba mgogoro wa Zanzibar atautafutia ufumbuzi wa kudumu, Katibu Mkuu huyo alisema chama chake kimetiwa moyo sana na kauli ya Rais Kikwete kwanza kwa kukiri kwake kuwa upo mpasuko wa kisiasa Zanzibar ikiwa ni kinyume na imani za viongozi wengi wa CCM hapa Zanzibar wanaolikataa hilo.

Pili ni kule kusema kwamba mpasuko huo utatafutiwa ufumbuzi alisema ni hatua nzuri na inajenga matumaini kwa Wazanzibari wengi lakini hakusita kutoa tahadhari kwa vile siku za kusubiriwa hatima ya mgogoro huo zinasonga mbele na vijana wanakata tamaa.

Maalim Seif anasema mara kadhaa yeye na viongozi wenzake wamekuwa wakiwataka vijana kupunguza jazba na kuwaomba wafuasi wao wazidishe subira na waheshimu hatua inayotaka kuchukuliwa na Rais Kikwete.

Anasema wanasiasa waliopo madarakani wengi wana uchu wa madaraka na kuogopa kuondolewa katika nafasi walizonazo hivyo wanafanya kila bidii kuhakikisha wanawagombanisha wananchi wa Unguja na Pemba ili kuwatenganisha.

Anasema wananchi wa Unguja na Pemba ni wamoja na hakuna aliye tayari kutenganishwa. Anasema si rahisi
kumuona mwananchi anayetoka Pemba akawa hana jamaa Unguja na ni vigumu mwananchi wa Unguja kukosa jamaa Pemba.

Maalim Seif anasema wananchi wa Unguja na Pemba wanatakiwa kuwa kitu kimoja na kamwe wasikubali kuruhusu kuwepo kwa tofauti zinazoweza kuwaweka mbali kimahusiano yao. “Tumepata matatizo na misukosuko mingi nadhani sasa huu ni wakati mzuri ambao wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba waunganishe nguvu zao na kuwa kitu kimoja na si wakati tena wa kurudi nyuma,” anasisitiza Maalim Seif.

Anasema zipo kauli za kutaka malumbano, wapo watu wanaoona malumbano ndiyo yatakayowaweka madarakani lakini wanapaswa kufahamu kuwa suala la kuwepo kwa amani na utulivu si la kulifanyia mzaha. “Amani na utulivu ni suala muhimu sana na hili halitaki mzaha kabisa kabisa” anasisitiza.

Maalim Seif anasema chama chake kwa ujumla kimetoa mapendekezo matatu ambayo yamepelekwa kwa Rais Kikwete kwa lengo la kupatikana ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar ambao aghlabu huibuka kila unapomalizika uchaguzi mkuu. Maalim Seif anayaainisha mambo ambayo yanapaswa yazingatiwe katika kuondosha mpasuko wa kisiasa Zanzibar;
Kwanza suala la uchaguzi mkuu wa mwaka jana haukuwa huru na haki kulikuwa na vikosi vingi vya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, vikosi ambavyo viliogopesha wananchi, hivyo wananchi wengi haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Pili, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar licha ya kuwa na wajumbe kutoka CCM na CUF, ilitawaliwa zaidi na wakereketwa wa CCM kwa vile wajumbe wawili tu ndio kutoka CUF na watano kutoka CCM ingawa ilipendekezwa na Tume ya Mwafaka kuwa sekretarieti ya Tume ipangwe upya jambo ambalo halikutekelezwa na Rais Karume.

Maalim Seif anasema ili uchaguzi uwe huru na haki ni lazima kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Pendekezo la kwanza la CUF kuhusu uchaguzi uliofanyika Oktoba 30, 2005 ni kuwa uchaguzi urudiwe, pendekezo ambalo limekuwa likipingwa kwa nguvu zote na CCM Zanzibar.

Pendekezo jengine ni kuwepo kwa serikali ya mpito ambayo itaongozwa na Mzanzibari yeyote anayekubalika na kuheshimiwa na pande zote mbili za vyama vya siasa akimaanisha CCM na CUF na kwamba mzanzibari huyo si lazima awe Maalim Seif au Karume na lengo kubwa ni kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi mkuu.

Na pendekezo la tatu ni kuunganisha nguvu kwa pamoja kwa kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa.Kwa upande wa Chama Cha Wananchi (CUF) waliliona hilo mapema na wameliingiza katika sera zao tokea mwaka 1995 kwa kueleza bayana kwamba iwapo CUF itashinda, itaunda Serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwa ndio njia pekee ya kuondosha matatizo yaliyopo visiwani.

Maalim Seif amewataka viongozi kuangalia maslahi ya taifa mbele kwa ajili ya kujenga Serikali ya watu wote itayokuwa imara kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Unguja na Pemba huku kila mtu akiweka pembeni tofauti zake na kusahau yaliyopita bila ya kulipiziana visasi.

Aidha Maalim Seif amezungumzia slogani ya ‘Mapinduzi Daima’ kuwa haisaidii katika kuondosha minyororo ya historia na kuendeleza chuki na uhasama Zanzibar. Anasema ni kweli mapinduzi yalifanyika lakini hayawezi kuwa ya daima, hayo sasa ni historia. Anasema slogani kama hizo zinachangia kukwamisha juhudi za kufikia demokrasia ya kweli.

Maalim Seif anasema CUF imejitahidi sana kuwatuliza wafuasi wao na kuwataka wasubiri hatua zitakazochukuliwa na Rais Kikwete katika kutatua mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar kwa maslahi ya wananchi wote.
 
Hali si shwari ZANZIBAR

KUJIUZULU kwa Amina Salum Ali kutoka nafasi ya uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kumeelezwa kubeba ajenda nzito katika upangaji wa mustakabali wa baadaye wa baadhi ya wana-CCM Zanzibar.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili kwa muda sasa unaonyesha kwamba, kuwa ni maandalizi ya mwanasiasa huyo kujenga mazingira ya hatimaye kupata nafasi ya kuwania urais ifikapo mwaka 2010 visiwani kupitia kambi ya Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Juma.

Mpango huo pamoja na mambo mengine umemuweka katikati ya utekelezaji wake, kada huyo wa siku nyingi wa chama hicho ili asiweze pengine kuguswa na 'mawaa' ya ndani ya serikali ya Karume.

Mtazamo huo ni kinyume kabisa na mawazo ya kambi kadhaa ambazo zimeibuka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar zinazojipanga na kujiandaa kwa kinyang'anyiro hicho cha kuwania urais wa visiwa hivyo kwamba kambi ya Dk. Salmin imeanza kumomonyoka baada ya kumpoteza Amina kutokana na kujiuzulu kutoka serikalini wiki moja iliyopita.

Amina ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho katika hatua za awali mwaka 2000, aliomba kujiuzulu ili apate nafasi ya kutumikia nafasi ya kuiwakilisha Afrika katika Tume ya Umoja wa Mataifa (UN) inayoshughulia masuala ya bara hili, yenye ofisi yake New York nchini Marekani.

Wachambuzi wa masuala ya siasa za Zanzibar wameiambia Mwananchi Jumapili kuwa kuondoka kwa Amina katika serikali ya Rais Aman Karume kumekuja wakati muafaka na kwamba kwa kuwa ndiye mtu ambaye anatazamiwa kuwania kiti cha urais kwa mtazamo wa kambi hiyo, basi kazi hiyo huko nje mpya itampa uzoefu wa kimataifa.

"Kambi yake (kambi inayomuunga mkono Dk. Salmin) walitoa baraka kwa Amina kuondoka, kwanza ili aweze kujiweka mbali na serikali na la muhimu kwao wanadai kuwa ni Amina kujenga uzoefu wa kimataifa na kutafuta uungwaji mkono wa kimataifa," chanzo kimoja cha habari kimedokeza wiki hii.

Amina ambaye mbali ya kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Kiongozi pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ya CCM. Ndiye alikuwa kiongozi pekee ambaye ana ushawishi mkubwa katika kambi ya Dk Salmin licha ya kuwa katika SMZ, awamu ya sita chini ya Rais Amani Karume.

Mwananchi Jumapili imeelezwa kuwa kambi hiyo ya Dk. Salmin inaona kuwa Amina anayo nafasi kubwa ya kuweza kuiwakilisha katika kinyang'anyiro cha urais ifikapo mwaka 2010 kwa vile mtu mwingine aliyekuwa akitegemewa zaidi, Dk. Gharib Bilal, Waziri Kiongozi Mstaafu hadi kufikia wakati huo umri wake utakuwa umesogea zaidi kiasi cha kutokuwa na mvuto kwa wapiga kura ndani ya CCM.

Wakati Amina akipata nafasi ya kujitangaza kimataifa, kambi nyingine zinazolenga kuweka wawakilishi wake katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka 2010 nazo zinaendelea kujiimarisha jambo linazozua mivutano ya uongozi ndani ya SMZ na hata CCM kitaifa.

Kitendo cha Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kuonekana kuwa ameanza kumpigia debe mtoto wake, Dk. Hussein Mwinyi ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano kuwania urais Zanzibar kinaelezwa kuwa kimemuweka njia panda Rais wa Muungano, Jakaya Kikwete.

Rais Kikwete ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa CCM inadaiwa kuwa anaonekana kuwa kama anamwandaa au kumtayarisha Naibu Waziri wa Usalama wa Rais, Mohammed Abood kuwania nafasi hiyo, kiasi cha kushindwa kumshawishi Mzee Mwinyi kuachana na harakati zake, hivyo kujikuta njia panda.


Mwanasiasa mwingine, Ali Juma Shamhuna, Naibu Waziri Kiongozi ambaye hivi karibuni amekuwa na sauti katika serikali ya Rais Karume ni mtu anayedaiwa kujiandaa kuwania urais 2010 huku akiwa kama vile ameasi kutoka kambi yake ya zamani, ile ya Dk. Salmin.

Habari kutoka ndani ya CCM Zanzibar zinaeleza kuwa Shamuhuna kwa sasa haungwi tena mkono na kundi lolote na kwamba kukubali kuwa msemaji katika masuala ambayo yanakinzana na CCM makao makuu, ni jambo ambalo linaondoa uwezekano wa yeye kuweza kupata nafasi ya kuwania kiti hicho.

Shamuhuna ambaye awali alipanda chati akiwa katika kambi ya Dk Salmin kwa kuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali ya awamu ya sita ya Rais Karume alibadilika muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa waziri katika hiyo hiyo serikalini na kutumika kuwa msemaji katika masuala yenye utata.

Wafuatiliaji wa masuala ya Zanzibar wanatoa mfano wa hivi karibuni ambapo Shamuhuna alikuwa mtu wa kwanza kujitokeza wazi wazi kupinga mpango wowote wa kuangalia uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya mseto baina ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF) visiwani humo.

Pamoja ukweli wa Shamuhuna kutumiwa na Rais Karume katika kuzungumzia hadharani masuala yenye utata, inadaiwa kuwa si miongoni mwa watua wanaopendekezwa na kambi ya kiongozi huyo kumrithi.

Watu walio karibu na Rais Karume wameiambia Mwananchi Jumapili kuwa chaguo lake ni Waziri Kiongozi wa serikali yake, Shamsi Vuai Nahodha, mtu ambaye anaaminika kuwa amekuwa mtiifu na inaelezwa kuwa tayari 'wazee' walio karibu na uongozi wa SMZ wameonyesha kumkubali.

Maelezo ya ndani kutoka serikali ya Zanzibar na ya Muungano pamoja na CCM ni kwamba suala la urais katika visiwa hivyo, ingawa bado lina zaidi ya miaka minne mbele kabla ya kufika kwa muda wake linaweza kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama tawala, ikiwa Rais Kikwete hataweza kutumia vizuri kete yake ya uenyekiti.
 
Mimi sina wasiwasi na Zanzibar maadam wote ni wana mapinduzi!... Salmin ni Komandoo, huyu kiboko yao kwa hiyo hakitabadilika kitu. Hata hivyo nakuhakikishia kuwa Bi Amina hatakwenda kokote!... utakuja nambia.
 
Wazanzibari wanasema wabara wanawaburuza,wabara wanaona wanawalipia kila kitu wazanzibari

je tuuvunje muungano?

NDIO

HAPANA
 
Tunachohitaji ni marekebisho, technically ndani ya muungano, bado Bara tuna-responsibility ya kuwabeba kiusalama ndugu zetu weusi wa huko visiwani, hiyo statement hapo juu ni very irresponsible kijana, ndio faida ya amani kwa wingi hata mnasahau ilikotoka!

Tunasema muungano ufanyiwe marekebisha kupunguza kero za pande zote mbili, sio kuuvunja!, Hayo maneno yako ya kuuvunja sio msimamo wa hii forum I must m,ake that clear kabla mtu hajafikiri wote tunakuunga mkono, HAPANA, na hakuna kura bro!

Halafu wewe si upo London, JM yuko hapo kwa mapumziko mpigie,

kwenye hii namba # 44-789-983-0670,

piga kwa adabu uliza kiungwana utapewa majibu murua kuhusu huu muungano acha ngebe ngebe hapa!, pia Mzee mwenyewe RO naye yupo hapo!
 
sasa mbona mnajichanganya nyie si ndio mliokuwa mkikataa wasijiunge na OIC na wao wanaona kuwa hiyo ni haki yao vile vile walipotaka kurekebisha katiba yao wakakataliwa sasa inamaana kuwa hakuna way out...
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom